Nipo kwenye ndoa kwa miaka 3 sasa na
nimefanikiwa kuzaa mtoto mmoja. Lakini kabla
sijaolewa nilikuwa na mchumba aliyehitaji kunioa ila
tulipotezaga mawasiliano miaka mingi sana. Tatizo
linalosaababisha niombe ushauri ni huyu mchumba
wangu wa zamani maana kwa sasa amerudi, kusema
kweli bado nampenda sana na yeye pia amesema
ananipenda anataka niombe talaka kwa huyu mume
wangu wa sasa ili tuweze kuoana. Huyu mume
wangu wa sasa nilikubali tu kuolewa naye kwakuwa
anajiweza na nilichoka kukaa nyumbani, ila yeye
anaonesha ananipenda kweli. Naombeni ushauri
wenu niendelee tu na huyu mme japo simpendi au
niende kwa mtu ninayempenda