Mapenzi utata, naomba umshauri huyu dada

First Born

JF-Expert Member
Jul 11, 2011
5,310
1,473
Nipo kwenye ndoa kwa miaka 3 sasa na nimefanikiwa kuzaa mtoto mmoja.

Lakini kabla sijaolewa nilikuwa na mchumba aliyehitaji kunioa ila tulipotezaga mawasiliano miaka mingi sana.

Tatizo linalosababisha niombe ushauri ni huyu mchumba wangu wa zamani maana kwa sasa amerudi, kusema kweli bado nampenda sana na yeye pia amesema ananipenda anataka niombe talaka kwa huyu mume wangu wa sasa ili tuweze kuoana.

Huyu mume wangu wa sasa nilikubali tu kuolewa naye kwakuwa anajiweza na nilichoka kukaa nyumbani, ila yeye anaonesha ananipenda kweli.

Naombeni ushauri wenu niendelee tu na huyu mme japo simpendi au niende kwa mtu ninayempenda
 
Chanzo cha mauaji HAWA, pressure HAWA, ujambazi HAWA, kila unapoenda unakutana na kina HAWA, mateso yote ya mwanaume ni kwa ajili ya HAWA...sijui kwanini HAWA waliitwa HAWA!

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums
 
wewe anza kutangatanga uje ukose mwana na maji ya moto!!!!
hasara ya kupoteza mawasiliano ndio hiyo, amekuta mzigo umemilikiwa.

ene wei ufuate moyo wako unachokuelekeza manake hata ukifaidi ama ukipata hasara ni moyo wako ndio uta feel the test.
 
pole ila unapofanya maamuzi ya ndoa sio mchezo ndoa ni mara moja.c mara mbili kumbuka c kila unachokipenda utakipata thats y hukumpata toka mwanzo heshimu ndoa yako ifanye kitu kitakatifu achana na huyo wazamani.
 
Mmmmnh....Nimejikuta namuonea huruma huyo mumeo maana muda si mrefu utamuumiza..!! Ndoa hizi..!!!
 
Huyo mpenzi wako wa zamani alikuwa wapi kukuoa hadi ukaolewa na mtu mwingine?? Ulidhani ndoa ni fashion ndugu yangu? Sasa omba talaka kama hiyo talaka itatolewa, rudi kwa ex wako afu siku akikumwaga ndo utafurahi vizuri.... Umeshaolewa kwa ridhaa yako mwenyewe, so tulia tu my dear.
 
Huna msimamo na maisha yako, unaolewa kisa mtu anajiweza? Huoni hata aibu kwa miaka yako 3 ya ndoa na kwa mwanao? Kweli haya maneno "Ishini nao kwa akili" yanajithibitisha.
Mtaka yote kwa pupa.....
 
Acha kuchezea roho na furaha ya mmeo, umekiri kuwa anakupenda na pia uwezo anao sasa wataka nini tena?..sio siri ninyi dada zetu ujinga umewazidi..najiridhisha kusema utakuwa UMESHACHEPUKA na huyo jamaa, wa wapi wewe?..au jamaa anakulipa ukiwa mtupu mbele yake?..afu kwanini mpaka leo hii mnatumia moyo kupenda?..yaani basi tu ungekuwa karibu ungepata makofi ushike adabu.
 
Kila siku tunawaambiaga hela sio kila kitu katika maisha
mnalia lia ooooh....mwanaume hela sura tutavumiliana
sasa umezifata hela na unaishi kama upo
guantanamo....
Ndio imeshatokea tena haina jinsi....komaaa na icho kibabu
mpaka kife na presha au sukari ili urithi mali
 
Nipo kwenye ndoa kwa miaka 3 sasa na
nimefanikiwa kuzaa mtoto mmoja. Lakini kabla
sijaolewa nilikuwa na mchumba aliyehitaji kunioa ila
tulipotezaga mawasiliano miaka mingi sana. Tatizo
linalosaababisha niombe ushauri ni huyu mchumba
wangu wa zamani maana kwa sasa amerudi, kusema
kweli bado nampenda sana na yeye pia amesema
ananipenda anataka niombe talaka kwa huyu mume
wangu wa sasa ili tuweze kuoana. Huyu mume
wangu wa sasa nilikubali tu kuolewa naye kwakuwa
anajiweza na nilichoka kukaa nyumbani, ila yeye
anaonesha ananipenda kweli. Naombeni ushauri
wenu niendelee tu na huyu mme japo simpendi au
niende kwa mtu ninayempenda

Toka shetani katika jina la Yesu.
wewe
tatizo linakusumbua pepo la ngono, unamuacha mumeo coz, of ngono

au elimu yako iko fyatu.
 
Back
Top Bottom