Mbavu mbili
JF-Expert Member
- Apr 25, 2011
- 1,457
- 874
Wakuu habari,
Jana nikiwa nimejipumzisha sebuleni majira ya saa moja na nusu nilisikia sauti za kujiapiza kupitia dirishani. "Nitakumaliza, usinichezee, wewe hunijui vizuri, endelea kunizingua"Nikachungulia dirishani kijana mtoa vitisho akazidi kujiapiza.
Kuna nyumba ya jirani inayotoa chemba ya maji machafu ya bafuni. Jamaa akatembea kama hatua kumi na tano.
Akachota maji kwa mikono miwili akayanywa.
Mwili ukasisimka. Ikabidi nitoke nje, kuniona tu jamaa akatimua mbio. Kwa bahati mbaya au nzuri jamaa ninamfahamu. Nilichojifunza hisia za kimapenzi zina nguvu za ajabu.
Swali langu;
Je hizo nguvu za ajabu hazizuiliki kimaamuzi?
Ni kwanini watu walioathiriwa na nguvu hiyo huchukua hatua zisizo kuwa na tija?