Mapenzi nusu yanitoe uhai

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,699
9,778
Nusu yanigeuze chizi, Ilibaki kidogo niwe teja!

Nakumbuka kipindi hicho 2019, Hakuna mwanadada niliewahi kumpenda kama Modesta, Mama yangu alilifahamu hili,
Wazazi wake hawakuwa na kipingamizi chochote cha mimi kuwa karibu naye, Kwa kuwa nilikuwa mfano wa kuigwa katika jamii,
Mwenye tabia njema, Mpole, mkimya!

Mwanzoni mapenzi yetu yalitaradadi, Mtaa mzima ukafahamu, Hakuna mwanaume mwingine aliyejaribu kumsogelea Modesta,
Kwa kuwa baba yake alikuwa mwanajeshi, Ambaye hakupenda kuona vijana wakimshambulia mwanae, Isipokuwa mimi, ambaye nilianza kama msaidizi wake kwenye masomo

Mabinti wa mtaani walinitupia sana jicho, Lakini sikuwa na muda nao, Sikuruhusu yeyote zaidi ya Modesta, Maake kwake nilikufa, nikaoza, nikazikwa, nikafufukia kwake, nikazama moyoni mwake, Haikuwa kawaida kumkuta Modesta kasimamishwa na mwanaume njiani

Nakumbuka hata siku niliyomchakata mbususu, Alikuwa sawa na biskuti yenye vipande kumi ndani, ikafunguliwa, kipande kimoja tu kikaliwa, Nili enjoy sana Modesta, Kwa hili sitokusahau!

Pindi aliporudi toka shuleni, Alikuwa ni mtu wa kukaa ndani tu, Mzazi wake yupi angeliruhusu atoke nje aonwe na wala tunda kimasihara? Hata kama angelihitaji kwenda wapi, Mama yake angenipigia simu nije kumchukua nimpeleke, Waliamini kuwa nitakuja kumuoa, Na mimi nilifahamu hilo fika, Baba yake aliniambia, kwa heshima yangu, ningejinyakulia kombe bure kabisa! Free of Charge!

Mtoto Modestor, Binti aliekuwa na msimamo, Mpole, Mwenye macho ya kusinzia flani hivi, angavu na meupe pe!
Kama nakuona vile, na hilo shape lako, Kwa jinsi huo mzigo ulivyoujaza, Nilitamani kuyaazima nikayafanye mto (foronya) chumbani kwangu, Sauti yako Modesta, Dah! Nilivyokuwa nakupapasa shingoni, Nakushika kiuno, Wewe kimya! Huku unazisumbua nywele za kichwa chako kwa kidole chako cha mkono wa kushoto, huku kiwiko kikiwa juu ya p*ja tulivu! Narudia tena kukuita kwa mara nyingine, Modesta! Modesta! Ewe Modesta!

______________________________________
Kuna siku nilimuomba Modesta kumchakata mbususu, hakuwa na hiyana, badala yake alinipanga ingelipendeza kama tungefanya Jumapili jioni! Hivyo siku ya ijumaa nilienda kumuombea ruhusa kwa mama yake, nikamwambia,"kama hutojali, siku ya jumapili nitahitaji kutoka na Modesta! Kuna mahali nataka niende nae". Hata hakukataa, akasema kama Modesta amekubari, haina shida! Kisha akanambia, "Siku ya jumapili jioni, Modesta hatokuwa na kazi hivyo utakuja umchukue tu, na mkitoka hakikisha amefunga geti langu".

Siku ya Jumapili ilifika! Mwanaume nikajipanga kwa ajili ya maangamizo! Nikapiga maji, nikaingizana kwa Modesta kumchukua, nilivyofika tu, akanambia anaumwa hivyo tupange siku nyingine! Nikaona ni sawa! Lakini kipindi natoka nje ya geti! Kuna mhuni mmoja akaingizana mle ndani, ni mvuta bangi kwanza, kijana asiyeeleweka, kila siku ni yeye na visa pale mtaani, utasikia kapita na jiko la gesi la mama fulani, mara kamtoboa mtu miguu, mara kanusurika kuvikwa tairi la gari! Na visa kibao, kutembea kwake tu, anatembelea huku kaegamia upande mmoja!

Nilikaa kwa mbali kidogo nikitazama kinachoendelea, muda si mrefu waliingizana ndani ya nyumba kufanyia mapenzi kwenye nyumba ya mama yake! Niliduwaa pale nilipokuwa mpaka mida ya saa moja kasoro ambapo yule mhuni alitoka akitizama kushoto na kulia, kisha kufungua geti na kutokomea kusiko julikana! Modesta alinikuta nikiwa nimedandia kwenye vyuma vya fensi kama nyani mwenye mawazo! Aliduwaa tu na kanga yake alojifunga! Niliamua kuondoka zangu huku machozi yakinibubujika!

Mwezi mmoja baadae, Modesta aligundulika kuwa ni mjamzito! Ingawa mwanzoni alinisakama mimi na kusema kuwa huo ni ujauzito wangu, baadae alinionea huruma tu na kuusema ukweli! Wazazi wake waliniomba msamaha kwa hatua walizokuwa wakifanya kuhakikisha napata kinachonistahili!

Dah! Dunia tambala mbovu! Mhuni alitokomea kusikojulikana! Ngoja nikuulize Modesta, Sasa huyo mhuni ulimpendea nini!!
Kama hukunipenda, ungelitafuta hata mwanaume mwenye mwonekano na utu kama niliokuwa nao mimi
Sawa tu Modesta, Karma imekuripa, mtunze mwanao Modesta!

Kiukweli, nilikupenda sana!!
 
Mimi mapenzi hayajawahi kunitesa na sio kama naongea kwa sifa hapana nasema ukweli na naomba Mungu aniepushie hilo

Yaani nikiachwa naona kawaida
 
Nusu yanigeuze chizi, Ilibaki kidogo niwe teja!

Nakumbuka kipindi hicho 2019, Hakuna mwanadada niliewahi kumpenda kama Modesta, Mama yangu alilifahamu hili,
Wazazi wake hawakuwa na kipingamizi chochote cha mimi kuwa karibu naye, Kwa kuwa nilikuwa mfano wa kuigwa katika jamii,
Mwenye tabia njema, Mpole, mkimya!
Hahaha,wakati wewe unasubiri embe liive,lianguke ndio ule,kuna wenzio wanakula na chumvi likiwa changa huko huko juu ya mti. Pole,amka,ustaarabu wako haukusaidii chochote kwa mapenzi ya dunia hii ya sasa.
 
Maisha ya mwanamke siku zote ni ya majuto pia naweza kusema mwalimu wa mwanamke ni kipofu always kwa iyo wacha kumlilia modesta amechagua njia sahihi ambayo ameona inafaa don't cry kjana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom