Mapenzi ni utoto unaofanywa na watu wazima...

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,855
1,117
Ukiyatazama mapenzi kwa jicho la tatu utagundua kwamba ni utoto unaofanywa na watu wazima. Ebu wachunguze wanawake, wanapenda kuambiwa maneno mazuri, yenye kila aina ya ahadi ndani yake hata kama ni uongo. Wanaume nao wanapenda waambiwe maneno matamu yanayohusu mapenzi hata kama ni ya ulaghai na hayana ukweli, wao huamini tu kwasababu ni matamu" ....mwisho wa siku vilio.
 
Imejini hayo maneno matamu yasingekuwako...............yangeitwa mapenzi kweli?
 
mapenzi si utoto,hivyo vionjo unavyoviita utoto ndio vinaitwa mapenzi lol grow up
 
Mapenzi siyo utoto 2, bali ni makubaliano baina ya wapumbavu wawili, ukiwa na akili zako timamu huwezi penda. Ndo maana wale wanaojiona wako smart huishia kuumizwa tu, sababu ya kumegwa na kuachwa.
 
Ukiona hivi ujue umetendwa ama unasifiwa na Mpenzio lakini huamini wastahili hizo sifa.... Ironically ukute anamaanisha kabisa ila tu sababu wanaume mna mtindo wa kutaka jua hasa kama kweli na mara nyingi kushindwa amini ndio mana inakuja negative attitude. Ingawa somehow nakuungua mkono life would have been so simple kama Mapenzi yasingekuwepo.
 
Umesahau kudeka na kudekezana.....

Nadhani maisha ilitakiwa iwe vile sema tu shetani kaingilia hapo katikati ndio maana tunaita utoto!
 
Mapenzi siyo utoto 2, bali ni makubaliano baina ya wapumbavu wawili, ukiwa na akili zako timamu huwezi penda. Ndo maana wale wanaojiona wako smart huishia kuumizwa tu, sababu ya kumegwa na kuachwa.

Aiseeee!!
 
Mapenzi ni mchezo wa watu wazima.
Tatizo watoto mnaingilia na hata kuharibu fani.

Hebu angalia mwenyewe(wala usiende mbali) namna watoto wanavyoliharibu jukwaa la MMU.
 
Unataka tuambiane maneno machungu?

Mai waif, ana maana maneno kama mf. wa yale nnayokwambiaga - "Husny una sura nzuri kuwazidi malkia Nelepta na Sorais !
- Husny una shingo ya upanga! - Husny hatua zako za hesabu , na macho yako mng'aro wa mbalamwezi.
- Kiuno cha Nyigu!
- Mguu wa bia !
N.k n.k
 
ooh mme, ongea taratibu utajiongezea competitors.
 
Back
Top Bottom