Mapenzi ni ujinga. Yaani ni mambo ya kustaajabisha sana

pancho boy

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
5,518
2,000
Kwa kweli mapenzi ni upumbavu sijui kwanini yaliletwa duniani .

Nimeshuhudia watu wakiteseka na kudiriki kujiua kisa tu mapenzi. Baba mkubwa huko kijijini alikuwa na mke mkubwa baadae akafariki kwahiyo ikabidi aoe mke mwengine ambaye alikuwa binti mdogo.

Yule binti kazi yake ilikuwa kuwatesa watoto wa mzee mkubwa yule huko kuwatumikisha makazi mengi. Na bado mzee huyo akirudi anapewa kesi za uzushi kuwa wanae wamemtukana huyo mama yao wa kambo

Mara wamegoma kufanya kazi. Kwahiyo anawaadhibu vibaya pasipo kutambua anawaonea wanae wa kuwazaa.

Yule binti kwa kuwa alikuwa ni dam changa na aliolewa kutokana na tamaa ya maisha. Basi akawa anagawa uroda kwa vijana wadogo hapo kijijini na tetesi zinasambaa. Ila baba mkubwa yeye alikuwa alikuwa hasikii wala haoni.

Niishie hapa kwa sasa yule binti yupo morogoro huko kaolewa na kijana mwenzie. Watoto wa baba mkubwa tuliwachukua mmoja kamaliza mtihani wa kidato cha 6.

Baba mkubwa yuko huko kijijini alipoumwa sisi ndo tulimpeleka hospitali wakati alipomuoa yule binti ,aliwahi kuwakana ndugu zake na kusema wanamuharibia ndoa yake kwani ameoa binti mbichi hivyo wanamuonea wivu.

Mapenzi ni ujinga yanaficha vitu hasa uovu mwingi. Na ushetani mwingi. Tusilipize mabaya kwa mabaya .bali tulipe kwa mema kwani hujui kesho yako ni ipi. Na atakuokota nani.
 
pancho boy

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
5,518
2,000
Ukianza kutafuta kwanza chanzo cha wewe kuzaliwa ni matokeo ya nini hasa utapata jawabu sahihi juu ya mada yako ndugu

Nimependa namna ulivyomalizia kwa ushauri mzuri wa kujenga jamii bora na imara zaidi
Hilo nalijua na ndo maana nasema ingewezekana labda kungekuwa na njia nyingine ya kuzaliwa
Kuna watu wamejeruhiwa vibaya mioyo yao na kuishia pasikostahiki sababu kuu ni mapenzi
 
pancho boy

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
5,518
2,000
Mapenzi ni upofu mkuu mapenzi yana siri ndani yake so kuna wakati unaweza jikuta ndugu wako wa damu kabisa unaona anapotea kwenye mapenzi lakini yeye aelewi kitu chochote
Hapo ndo huwa inaumiza kwa kweli na mwenzio unakutaka kashikwa haelewi kabisa niwe mkweli .

Mzee wangu kabisa enzi hizo aliwahi kuhonga kiwanja kwa mchepuko wake na nilikuwa najua Mimi tu wakati Niko secondary
 
walitola

JF-Expert Member
Nov 28, 2014
3,899

Si umeona mkuu mtu sijui anapewa kitu gani mpk anaonga kiwanja tena mchepuko ndio mana waswahili wanasema mapenzi ni upovu
 
pancho boy

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
5,518
2,000
Si umeona mkuu mtu sijui anapewa kitu gani mpk anaonga kiwanja tena mchepuko ndio mana waswahili wanasema mapenzi ni upovu
Na walishaachana zamani na kiwanja huyo mwanamke alishakiuza nae watu wamejenga nyumba hapo tena alikiuza kwa bei ya hasara akaenda pata bia baridii
 
walitola

JF-Expert Member
Nov 28, 2014
3,899
2,000
Mapenzi sio ujinga bali mpende ataye kupenda ndo utaona sio ujinga.
Yaani unakata undugu kisa mke. Hapo utakuwa hauna akili.
Ukifa atakuzika nani. Vitu vingine bana
Mkuu ndio mambo yanayotokea kwenye jamii yetu kuna watu wengi sana wamefukuza ndugu na wengine wamediriki hata kukana ukoo kisa mapenzi
 
pancho boy

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
5,518
2,000
Mapenzi sio ujinga bali mpende ataye kupenda ndo utaona sio ujinga.
Yaani unakata undugu kisa mke. Hapo utakuwa hauna akili.
Ukifa atakuzika nani. Vitu vingine bana
Ni kweli ila asilimia kubwa ni utampenda MTU ila yeye yuko kimaslahi

Ama upate anakupenda ila wewe moyo haupo hapo
 
Kunguru wa Manzese

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
3,157
2,000
Huwa nawaona watu wa ajabu wanaoteswa na mapenzi since nipo chuo nilishawaambia washikaj ktk vitu ambavyo havitokuja kunitesa ni hicho wakabisha Mara ooh hayajakukuta Mara ooh hujapenda

Mpaka sasa nilipo hayajawahi niendesha ni mwendo wa hit and run ukini convince nakaa sana

No offonse
 
Nami nakazia hayajakukuta
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom