Mapenzi ni kusaidiana katika majukumu....

kabanga

Platinum Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
37,649
Reaction score
19,042
DSC_0003_78f1f.JPG

Mara nyingi sisi wanaume tukishaoa, hatutaki tena kuwa saidia wake zetu kwa baadhi ya majumu ya ndani, hasa kufua nguo, kuonsha vyombo au kutandika kitanda kama sio kupika.

Kwangu mimi naamini kuwa saidia baadhi ya majukumu wake zetu na mahala zetu kwa wale wenye kukaa kinyumba bila kurasimisha. mimi sio mtaalamu sana ila naamini wenzangu ni wajuzi mwaweza kutiririka tukapata uzoefu zaidi....
 
Ni kweli inatakiwa kusaidiana lakini cha ajabu wakirudi wanachukua rimoti kontrol miguu juu ya stuli
 
kabanga nimependa sana mawazo yako,
Wanaume wanatakiwa kuwa hivyo!
Hata dada yangu Sista kakuunga mkono
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli inatakiwa kusaidiana lakini cha ajabu wakirudi wanachukua rimoti kontrol miguu juu ya stuli

Mengine .ni kujisahaulisha, nawewe ukisema amechoka jamaa anajiachia mazima ....
 
Duh! Kukaa uswahilini kunahitaji moyo...
 
sie ndo tunapapenda huko, kila kitu unapata.. alafu bei rahisiiiii.....
ukiwa na buku moja, umemaliza budget ya siku nzima...lol:smile-big:
 
Mkiwa na kipato cha chini atakusaidia na bajeti mtapanga subiri apate hela ya maana.......
 
DSC_0003_78f1f.JPG

Mara nyingi sisi wanaume tukishaoa, hatutaki tena kuwa saidia wake zetu kwa baadhi ya majumu ya ndani, hasa kufua nguo, kuonsha vyombo au kutandika kitanda kama sio kupika.

Kwangu mimi naamini kuwa saidia baadhi ya majukumu wake zetu na mahala zetu kwa wale wenye kukaa kinyumba bila kurasimisha. mimi sio mtaalamu sana ila naamini wenzangu ni wajuzi mwaweza kutiririka tukapata uzoefu zaidi....

hii imekaa vema mkuu japokuwa binafsi huwa ni mvivu sana wa kufua na kuosha vyombo but huwa namsaidia waif kulea.mfano mtoto anapokuwa ameharibu mambo huwa nachukua jukumu la kumsafisha,huwa nambeba mgongoni kumbembeleza alale na usiku huwa naamka kumpa maziwa,kumbadilisha nepi etc.namwacha waif apumzike
 
si dhani kwa mazingira yoyote yale mme akisha oa anatakiwa kuosha vyombo na nguo.....haitakiwi kabisa kama tunakuwa wakeli kabisa.....hakuna mwanamke anaye jitambua atakuwa nataka mme wake amekaa anafua au kuosha vyombo................lakini hii kama mwanamke anajitambua...ila kama ndo wale wengine utaona natetea mambo kama haya....
 
Mhhhh...Hata mtume muhammad(S.A.W)alikuwa akiwasaidia wake zake katika majukumu ya nyumbani!Sembuse wewe Dr.Mo
 
Last edited by a moderator:
hii imekaa vema mkuu japokuwa binafsi huwa ni mvivu sana wa kufua na kuosha vyombo but huwa namsaidia waif kulea.mfano mtoto anapokuwa ameharibu mambo huwa nachukua jukumu la kumsafisha,huwa nambeba mgongoni kumbembeleza alale na usiku huwa naamka kumpa maziwa,kumbadilisha nepi etc.namwacha waif apumzike

mwezio ikifika ijumaa jioni nikiingia home, kutoka labia kuwe na dharula kubwa, vinginevyo mwanzo mwisho kimtindo....
 
Me nampenda sana wa hiv..alhamdullilah!
 
Back
Top Bottom