Mapenzi ni fadhila?

nafikiri sio njaa ila nafikiri ni kukosa upeo wa kuelewa tu mpendwa wangu.
yaani unakuta mtu ana matarajio makubwa ilihali mwisho bado hajaujua.
 
Katika mapenzi its best to travel light.

Too much expectations compromise love.

Mapenzi sio fadhila.
 
mkuu umenikumbusha neno hili kwamba

'Tumshukuru Mungu kwasababu mambo haya aliwaficha wenye hekima na busara na kuwafunulia watoto wadogo'
 
sioni kuwa mstaarabu hata kidogo ambae anataka kutenda unyama kisa hajapewa huduma-fadhila!
tena sisi vijana ndio kabisa......
ni kweli kabisa vijana wanaongoza kwa kulipa visasi kisa tu penzi walilonyimwa.
kwangu mimi inabidi vijana wadogo tuanze kuwafunza kwamba maisha hayalazimishwi manake ukilazimisha yatakuja kukuumiza baadae.
 
kuna jambo moja la msingi sana ambalo wanaume wanasahau nalo ni huwez kumpata mke wa kweli kwasababu ya kumfadhili. yapo mambo mengine chungu nzima unayotakiwa ku-consider kabla kuamua nani awe mke.
 
Dah... Kongosho umenitachi screen aisee!!!

Nway ngoja tu niendelee kufanya nifanyayo ikitokea sawa na isipotokea ni sawa pua make hata mie nishasaidiwa saana tu na sina kitu ambacho ninaweza kuwalipa wale wote walionifikisha hapa nilipo!!!

Dada mkubwa gfsonwin sina cha kuongeza katika uzi huu ngoja nibaki msomaji tu.....
 
Last edited by a moderator:
hahahaha huku juu ni paradiso tu kwa kwenda mbele

shukrani kwa kupenda signature yangu be blessed
 
usijali Mungu naye husema hivi
'nitakutumia msaada toka patakatifu pangu'
 
Hahahaa.. Hapo alikumaliza kabisa. Huo ndio mtazamo sahihi hakuna malaika duniani.

Nadhani ungekua huu ndio mtazamo wa wengi kuvumiliana kungekuwa kupo kwa kiasi kikubwa sana... siku hizi mahusiano mengi yanadoda kwa kuwa na Mr Right/ Mr Perfect wengi na vile vile Ms Right/Perfect wengi... au kama hawako perfect wanataka kupata watu perfect ambao kiuhalisia hawapogo Duniani. aliwahi kuishi mmoja tu tena kwa miaka 33 pekee.
(hata huyu japo alikuwa perfect kwa watu wasio perfect bado walimuona naye ni tatizo) hope am not confusing

Shemeji Kaizer kwema?

 
na Mungu mwenyewe alishasema kwamba sote tumepungukiwa na utukufu wake alokuwa mtakatifu aliakuwa ni Kristo tu.
swlai linakuja kwamba vijana wengi wadogo hawajui maisha bado wanadhan wanayoish ni maisgizo na kwamba ipo siku maisha halisi yatakuja kumbe si kweli. kwasababuw anayoish ndio maisha halisi.
 


Wakati mwingine mapenzi na kitendo cha kufanya ngono hutumika kumaanisha kitu kimoja. Kama maana yako ndio hiyo, mapenzi hutumika kulipa fadhila katika mazingira fulani. Hii hasa hutokea kwa baadhi ya akina dada ambao huona hawana njia nyingine ya kulipa fadhila zaidi ya kuwa tayari kufanya ngono na mwanaume kama ishara ya shukurani. Na kwa kweli haiwi na wala hawasemi moja kwa moja bali huonyesha kila dalali ya kuwa tayari kwa hilo na inabidi mwanaume ang'amue hilo ili aweze "kuomba"

Mara nyingi bila hata kulipa fadhila, mwanamke akimpenda mwanaume hutengeneza hayo mazingira ili mwanaume amtongoze. Lakini asipokuwa na uwezo wa kusoma ishara hizo, baada ya muda mwanamke ataamini pengine jamaa hana interest naye na mwishowe husepa.
 
nafikiri sio sahihi kusema mapenzi ni kitendo cha kufanya ngono.......manake neno 'kufanya mapenzi' hili humaanisha ngono.
 
Kweli kabisa dadaangu.

Tuna shida kubwa ambayo nadhani wengi hawaiangalia katika mtazamo huo.... Vijana wengi wengi (wa mjini) role models wao wamekua wale waliopo kwenye soko la music america (akina Jiga and likes).... wanaona kuishi maisha ya uhalisia ni ushamba na huendi na wakati.... usipoongea ongea matusi kadhaa, hip hpo kidogo.. usipoongelea habari ya kuwa na msururu wa mademu (kama wanavyowaita wenyewe).. usipoongelea mambo ya Betting (kamari)... Mambo ya clubbing... Mambo sijui ya Roney na Messi, ulevi uliopitiliza.. mambo ya kuiba (kupiga madili kazini)...Sodomization.. unaonekana wewe ni wa kizamani saaana... Damn it. ukionekana unaongea ongea sense watakutenga ''eti unaboa''

Wanasiasa wetu wameiharibu jamii na mitaala ya shule hata wale role model tuliokuwa tunawasoma kwa vitabu hawapo tena, hata watendaji serikalini ambao tungetamani kuwa kama wao.. wameacha akili yao pembeni linapokuja swala la madaraka... sasa tunategemea nini?

Mungu atuokoe tu apa. Miaka kumi ijayo ambapo hiki kizazi kichanga ndio kitakuwa kimetamalaki sijui maadili yatakua ni yepi aisee....
 
hongera kwa kuwa tofauti na kuona si vyema kutumia shida za mwenzio ili akulipe kwa ngono ki kweli baadhi ya wanaume hutumia shida za wanawake kwa kuwasaidia ili baadae wawalipe kwa ngono nimeishuhudia hii kitu kikweli inaudhi sana
 
Karibu sana...

Pole sana.. Nadhani ni Laana kwa kweli kumlazimisha mwingine kuridhia asiyoyapenda ili tu umtatulie shida yake.... Kuna furaha ya ajabu sana unapomsaidia mtu kitu au namna fulani then ukaona anasogea au anafanikiwa.. ina furaha isioelezeka. ''Mithali 19:17 Amhurumiaye MHITAJI (masikini) humkopesha BWANA, Naye atamlipa kwa tendo lake jema''

Mapenzi ni ya wawili... Kwangu mimi nafurahi na kuona nimefanya kitu upande wapili unapofurahia nachokifanya... katika swala ambalo haitakiwi liwe na harufu ya ubinafsi ni hili.



hongera kwa kuwa tofauti na kuona si vyema kutumia shida za mwenzio ili akulipe kwa ngono ki kweli baadhi ya wanaume hutumia shida za wanawake kwa kuwasaidia ili baadae wawalipe kwa ngono nimeishuhudia hii kitu kikweli inaudhi sana
 
ni kweli kabisa vijana wanaongoza kwa kulipa visasi kisa tu penzi walilonyimwa.
kwangu mimi inabidi vijana wadogo tuanze kuwafunza kwamba maisha hayalazimishwi manake ukilazimisha yatakuja kukuumiza baadae.
sana tu, siwaona wakipata kitu kidogo fujo wanazofanya....?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…