tupo pamoja brodah!!mapenzi si fadhila, ila japo kuna watu wakike kwa wakiume wanafanya kuwa ni fadhila, sasa ukiyafanya nifadhila hadi kufikia kuoana mwishowe unakuwa sio mzuri naamini hivyo.....
sasa kama wanaume ni watu wa kupima kwann wao ndio0 wahanga wa kulia kila siku kwamba wamepigwa chini na waliowafadhili?Mapenzi hayawezi kuwa fadhila. Inategemea nyinyi 2 mawasiliano yenu yapoje, wanaume mara nyingi ni watu wa kupima au kujaribu, sasa yale majibu yako wakati huo wa kupimwa au kujaribiwa ndiyo huleta muafaka upande wa mwanaume na wakati huu ukianza kuleta misimamo yako ndiyo majanga hutokea.
same dear!!
umenikumbusha msemo wa wahenga kwamba wema haulipwi.
zamani wakati tunaolewa ilikuwa tunaangalia zaidi utayari ama wa kwako binti ama wa wazazi wako.......Mapenzi sio fadhila, mapenzi ni utayari na hiari ya mtu kuingia katika mahusiano na mtu mwingine, bila kujali anapata/atapata nini kutoka kwa mwenzake...hayo yalikuwa mapenzi ya miaka iliyopita.
Mapenzi (kwa asilimia kubwa) ya sasa yapo kwa kulipana fadhila. Fikiria wapenzi wengi wanasomeshana, wanapeana vito vya thamani, huku wakitegemea kupata kitu baadae. Wengine husema kabisa, simpendi ila namuoa/ananioa kwa sababu fulani, maana yake nini...kwamba huyo mwenza asingefanya hivyo asingepata nafasi kwenye moyo wake.
Ndio maana mtizamo wangu ni kuwa, ukiwa na mpenzi, kama umeamua kufanya kitu kwa ajili yake, iwe kumpeleka shule au kumnunulia kito cha thamani, ufanye hivyo kwa vile umependa na si kwa kutegemea kulipwa fadhila (kuoa/kuolewa)
ina maana mdogo wangu Eiyer kuna mikataba ambayo watu wengine hujiwekea ili waweze kuwa na mahusiano??Hapana,mapenzi sio fadhila
Nasema hayo kwasababu kwanza mapenzi ni kitendo cha kukubaliana kati ya watu wawili wa jinsia tofauti,wanakubaliana kuyafanya hayo mapenzi [sio ngono pekee] yaani mambo yanayohusiana na mapenzi kama vile kutoka out,kununuliana zawadi,kufanya ngono,kushare masuala ya kimaisha [kiuchumi] n.k
Watu au mtu hulalamika kwasababu ule ni mkataba ambao wanakuwa wamekubaliana na mmoja anaukiuka
Tatizo huanzia hapo!!
ni kweli mpendwa wangu wema halipiki.Mtu anawezaje kulipa wema mamii? Achana na material help mtu apatayo, ule moyo wa mtu kujitolea kwaajili yako, kukufikiria na kufurahia kuwa msaada kwako ..yaani huwezi kabisa zaidi ya kushukuru na upande wa pili uelewe hivyo pia, kuwa si lazima itokee kama wanavyo tarajia.
wewe unaonekana kukomaa na kukua kiakili zaid.Mapenzi ni muunganiko wa hisia na pia ni makubaliano ya kutimiza jambo au kitu fulani katika maisha,na endapo mmoja wenu hakutimiza makubaliano basi kunakuwa na malalamiko ya kutotendewa haki.
Cha msingi unapoingia kwenye mapenzi na mtu yeyote especially kwa sisi wanawake usijiaminishe kuwa lazima huyo jamaa yako atakuoa,Subiri wakati utasema kama ikitokea basi ni kheri,isipotokea maisha yanasonga mbele.
Hiyo ndio principle ambayo naitumia siku zote,na hata kama nikihisi sijatendewa haki huwa najipa moyo kuwa pengine it wasn't meant to be na ni hatua ya kujifunza na kukomaa kihisia.
sasa kama wanaume ni watu wa kupima kwann wao ndio0 wahanga wa kulia kila siku kwamba wamepigwa chini na waliowafadhili?
Inaonekana neno mkataba limekustua sanaina maana mdogo wangu Eiyer kuna mikataba ambayo watu wengine hujiwekea ili waweze kuwa na mahusiano??
Unasonga mbele ........ Lakini unaonaje/ama utajiskiaje pale makubaliano mliyokuba-LIANA YASIPOTEKELEZEKA??
sasa kama wanaume ni watu wa kupima kwann wao ndio0 wahanga wa kulia kila siku kwamba wamepigwa chini na waliowafadhili?
wewe unaonekana kukomaa na kukua kiakili zaid.
Lakini unaonaje/ama utajiskiaje pale makubaliano mliyokuba-LIANA YASIPOTEKELEZEKA??