Wana MMU herini ya mwaka mpya!!
Nawapenda sana............
Haya naombeni mnijibu swali langu hili kama mapenzi/upendo ni fadhila?. Sijui kama mtanielewa lakini naombeni mnielewe tu manake nimekuwa nakosa jibu juu ya swali hili.
Kila siku utakuta mtu analalamika mie bwana fulan nilimfanyia hivi bi fulan ama mie bi fulan nilimtendea hivi bwana fulan nikijua atakuwa mume/mke lakin mwisho wa siku kaniacha kaoa/kaolewa na mwingine.
sasa je wewe ulitenda hayo ili ulipwe fadhila??
ina maana msingeyafanya asingekuoa sio??Sometimes yes, mi nakumbuka siku moja niliambiwa "kwa tuliyoyafanya nisipokuoa ntakuwa sijakutendea haki"
ukweli from my heart nilifurahi kuona mupenzi anaona atleast afanye hivo kushow appreciation sijui ndo fadhila hapo.
Eeeka mbee!!Heri ya mwaka mpya nawe ''Neambatso baana''
Hii kitu imekuwa kama kulipa fadhila. Baadhi ya wanawake pia wameweka akili yao hivyo... Nimewahi kung'ang'aniwa kulipwa fadhila kwa namna hio na wasichaa tofauti... kila mmoja nilikua msaada kwake kwa namna flani hivi. Na mamna waliodhani kunishukuru waliona kusema asante haitoshi ni hadi ngono maana wengi wanafikiri tunaithamini sana (si kweli).... Hii dunia hii!!..... Pia baadhi yetu wanaume tunatumia shida za wanawak kujinufaish kingono au kimahusiano.... Hii ni mbaya
Nachojua ni kitu kibaya sana kutumia SHIDA au MATATIZO Ya mwanadamu mwenzako kujinufaisha kwa jina la MSAADA.
Ila ikawa kupitia msaada mengine yametokea na hayakuwa msingi wa huo msaada... well and fine.
Eeeka mbee!!
Mie ninachojiuliza ina maana mtu ategemee kulipwa fadhila ya ndoa baada ya msaada aloutoa?? manake kwa jinsi niwazavyo mimi haipaswi kuwa hivi.
imagine mtu anadai nimemsomesha binti fulan nikijua atakubali kuolewa na mimi............kweli??
You know what?? was about to call you connie manake nilijua utakuja na nyanga za kutosha.Mapenzi ya fadhila ni utumwa wa kujitakia. Hata mtu akupe nini, kama humpendi ni bora kumwambia mapema kuliko kuja kumchana chana hisia zake hapo baadae.
Mapenzi si fadhila, mapenzi ni mateso/furaha ya hiari, ukiona unajilazimisha sepa fasta.
Ukiona mtu analalamika hukumpenda ni kuwa bado yuko kwenye 'denial' ya penzi lake kutorudishwa kwake. Sasa hilo si tatizo lako, ni tatizo lake. Hta yeye anaweza kuwa anapendwa na mtu fulani na kamkataa sababu hiyo hiyo.
exactly Kongosho..........Ndoa sio fadhila ni hairi. Mkiishi muda mrefu pamoja uvumilivu na pretence zote huisha, mask zote huvunjika na hapo ndio masimango huanza.
Mtu aliyempenda kwa dhati afadhali, huwa kuna ka heshima fulani kanabaki. Ambaye hukumpenda kila kitu anakuwa anakukera, hata salamu yake tu waweza mwona ana uso kama kwa nyumbu, kumbe ni hasira zako mwenyewe ulizonazo dhidi yake.
nimejaribu kusoma kwa makini sana lakini sijakuelewa hata kidogo.Wanaume ndo wenye hulka hiyo kwa sana yaan akckia tu unakjishda au mambo yako ya pesa ya meza yamekaa ovyo kdgo ukute ndo bdada unavyo vtoto vwil nakuendelea vnalia njaa ndo hvyo tena walazmika kulipa fadhila coz hujui ya kesho.
You know what?? was about to call you connie manake nilijua utakuja na nyanga za kutosha.
Lakini mamito unachukuliaje pale ambapo mtu anajitoa kwa hali na mali either kwa kusema ama kimya kimya juu ya mwingine af mwishowe anaambiwa kuwa siwez kuwa na wewe kisha analalamika kwamba nilijua kwamba angekuwa wangu??
same dear!!Heri ya mwaka mpya na kwako pia...tunakupenda na tulikumiss!!
Mapenzi si fadhila, waswahili wanasema tenda wema nenda zako, usisubiri au kutegemea urudishiwe au ulipwe kwa ulilotenda. Ikitokea ni vema ila si vizuri kutumia mapenzi kama njia ya kurudisha fadhila au kuonesha shukrani.
Upendo uhusishe kutoa bila kutegemea chochote kama malipo, kwasababu umempenda mtu na upo tayari kufanya awe na furaha maana furaha yake ni yako pia..bahati mbaya sana siku hizi maana hiyo imebadilika kiasi...
sasa hapo connie umesema kitu ambacho wengi hawakikumbukagi kwamba huwez kulazimsha penzi abadan........Gfsonwin
Ukiumizwa ni kawaida kulalamika, iwe una hoja ya maana ama huna hoja ya maana. Mapenzi ni trial and error hadi utakapompata amabaye anakupenda wewe na wewe unampenda.
Wee gf katika umri wako huu hujawahi kuumizwa? Ni kawaida kuumizwa na kulalamika ni haki yako. Mtu unakuwa unalalamika tu sababu ya yale maumivu na kuona kile ulichokitamani kimeshindwa kutokea. Ila ukija kupona ndio unajicheka tu ni jinsi gani ulikuwa unaumia na kulalamika hovyo. So mi naona ni stage ya kawaida ya maumivu ya mapenzi.
Bora anayelalamika tu, kuna wengine wanaenda mbali na kutaka kuwaumiza waliokataa kurudisha upendo huo kwa njia yoyote.
Lakini point hapa ni kuwa, huwezi lazimisha mtu akupende, haipo. Hata akiamua kuwa na wewe itakuwa kwa muda tu baadae anasepa, na hapa ndio unaumia zaidi.