Mtoto wa watu nimeenda chuo mtu mwema kabisa,
Semester ya kwanza nikakaa hostel kwa hiyo nikaishia kuwa na friends tu basi.
Semester ya pili nikaingia maghettoni.
Hapa ndo shida ilipoanzia,siku moja nikakutana na mtoto mmoja rusha nyavu imoo.
Siku aliponitembelea maghettoni kaacha vitu kadhaa.
Mwisho wa siku kahamia kabisa sema uzuri wake nikikwama kwenye ishu za kodi ananipiga tafu.
Huyu alikuwa kanitangulia chuo.
Nimeishi naye mpaka kamaliza akasema akasalimie kwao atarudi ikawa mazima.
Nikimcheki naona kama mawasiliano yanapungua.
Nikamchana tu "distance relationship tunadanganyana" tubaki marafiki tu.
Mwaka wa pili vuta chombo nyingine nikaishi naye mwaka wote.
Mwaka wa tatu nikaruka na mwingine mpaka mwaka ukakata.
Mwaka wa mwisho(wa nne) nikasema sasa hivi nahitaji kutafuta wife sasa mambo ya kurukaruka nayaacha.
Nikaiibukia pisi moja hivi ikawa inanizungusha tu"eti tubaki kuwa marafiki tu"
Nikampotezea nikahamia mtaani kwa dada mmoja muuza bucha la nyama
Mpaka tukaja kuoana.
To cut the long story short yule dada aliyeniambia tubaki marafiki alipojua nadate na yule mdada wa buchani akaniambia eti alikuwa ananipima kama nina mapenzi ya kweli ila ndo hvyo sasa alikuwa kashachelewa.
Ila sikulaza damu nilitia chapa kabla sijamuoa yule demu wangu wa buchani na tukabaki marafiki kama alivyotaka