Wakuu...
siku za karibuni nimeona rafiki zangu wawili wakivunja ndoa zao baada ya kutoswa na wake zao, hao wadada ni wa shoka, elimu A, na kazi walizopata ni za kimataifa
Cha kushangaza mmoja wao hakuwahi kuwa na issue na mkewe zaidi ya kuburuzwa kwenye maamuzi tangu mama amalize PhD yake; sasa nimesikia mama kapata kazi nje ya nchi, kaondoka bila kumuaga jamaa na amepeleka watoto wote boarding na jamaa hajui afuate njia ipi
Sasa najiuliza, hivi kuna uhusiano kati ya mafanikio ya mwanamke na kuvunjika kwa ndoa??? Nafahamu humu ndani kuna matawi yote na nategemea msaada maana mie nasomesha mke na nimeshaanza kuogopa
Please advice
Ha-ha-ha-ha MTM unasomesha mke?...Pole! that's all i can say,,,subiria akisha graduate atataka talaka...Nimeshaona watu wengi (tena washikaji wa karibu sana)walisomesha hivyo hivyo mke kamaliza shule kachukua chake mapema...kamuacha mume anatoa macho!....but you never know labda wako mstaraabu...siyo wanawake wote though wako hivyo ila you never know....hahahahaha mnyalu umeula hahahaha pole in advance!
mwanamke bora utamuona mapema!!! chake ni chako,chako ni chake.....inamaana kama wewe una pesa inakuwa ukimpa ufikirii sana hata yeye akiwa na pesa akikupa inakuwa sawa,ila si wala wanawake wanaotaka pesa za waume zao,za kwake ukichukua lazima urudishe.hii ni noma....mimi si pendi
Mh, mbona wanipasua moyo we binti!???
Yaani kuna mtu amenionya maana nasomesha kwa kasi sana... Ni mtu mzima akaniambia kaka angalia unasafisha talaka!! I never had those feelings before
Ngoja niangalie indicators nyingine
Bwana eh, tuliumbwa tusaidiane... aki-abuse support yangu basi, ilimradi alee watoto maana hilo ndo la msingi
Inatia presha hii bana!!
bwana eh, tuliumbwa tusaidiane... Aki-abuse support yangu basi, ilimradi alee watoto maana hilo ndo la msingi
inatia presha hii bana!!
Thanks, nina wasiwasi kwamba hiyo hulka inakua mno, au ni haya mawazo yangu hasi?
Kwanini na wewe usiitafute hiyo PhD? Just asking kwa nia nzuri tu lakini. Samahani kama nimekukwaza mkuu.
cjui kwanini wanawake wa kisasa wamekuwa na tabia hii, nimeshaona pia kwa frnds zangu wawili nao wamewaacha waume mmoja alisema huyo sio level yake kwasasa lakini wana watoto wawili, mwngne yeye ndio alichemsha mana alimmwaga mume alikodhania mambo yakaenda mrama akarudi kuomba radhi ikawa too late, mkaka maisha bomba, mke mzuri/makini...ameishia kujilaumu tu...cjui inakuwagaje hapo kwa wanawake wenzangu jamani.
mh hii mada ni nzito si ya kujadili kijuu juu mm yamekuta live na nimegundua linachangiwa na vitu vingi wengi na nitatizo la mtu mmoja na lakifamilia kwa mfano umemsomesha mke amekwenda shule kule anakutana na marafiki wanambadilisha anaanza dharau anona nimesoma kazi nzuri nitashea vp na huyu mume ajasoma kama mm anatafuta msomi mwenzake ili aendane nae kwakweli ni hulka ya baadhi na ulimbukeni na ukatili na kujisahau