Mapenzi Matamu Jamani, Mungu Tuongoze

Mapenzi Matamu Jamani, Mungu Tuongoze

Habari ya saa hii wana JF

Ni kuhusu penzi langu na huyu star wa bongo movie (jina kapuni) alofanikiwa kuniteka roho mpaka mwili kiukweli mapenzi ni matamu tena sana tu,japo naamini sisi wote ni binadamu kuna wakati tunakosea na tunaelewana kwa mambo madogo madogo.

Mwanaume huyu akikosea hajui kuficha kabisa hata kama yupo mbali utamjua tu kupitia ongea yake kwenye simu inabadilika anapata kigugumizi au anaongea haraka haraka mpaka unamgundua,(sijui kama wanaume wengine wapo hivi?) na hata akiwa karibu kama anajua amenikwaza atanibeba, anibembeleze mara afanye hivi mpaka hasira zote zinapotea.

Napenda tu anaposema Am Sorry Honey, nimekosa na muombea kwa mungu asije akabadilika. Navyoandika huu uzi, nasumbuliwa na maumivu ya tumbo kidogo hadi nimeshindwa kula. Ila nipo na hubby hapa, katoka kuniogesha kanifuta maji,kanivalisha pichu na night dress, kanifunika shuka nilale!! amekaa pembeni kuna kitabu anasoma sijui ni nini ila ndo namuangalia tu hata simalizi.

Nawaza mengi juu yake nampenda sana.
Kajomba kanakuja, hongera sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom