mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,666
Leo TBC waliendesha kipindi chao cha "Duru za Kiswahili" wakiongelea maudhui ya kitabu cha Marehemu E. Semzaba "Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe".
Maudhui ya kitabu hichokwa sasa yanagusa maisha, matendo na tabia za viongozi wetu, hasa watumishi wa umma, kwa maana "CHEO NI DHAMANA".
Nakumbuka aliyoandika kilimasera, mwanaJF humu jamvini Dec 22, 2010, akitoa husia kwa wanasiasa, nanukuu baadhi;
" Niseme mapema kuwa kama hujawahi kusoma tamthiliya hii au kuisikiliza au kama umekwisha isahau nashauri ujipatie nakala yako popote kitabu hicho kinakopatikana na mnaweza kujisomea kwenye familia (kama waigizaji role playing) au na washirika wako kazini au hata kijiweni! Na kama ningekuwa na uwezo kidogo ningehakikisha wabunge wote wanapata nakala yake, na wale mawaziri ningewataka wakisome kwenye semina yetu Ngurdoto!
Tunapoendelea na vita dhidi ya ufisadi tunaweza kuona mfanano mkubwa kati ya yale aliyokuwa akiyafanya Ngoswe (mhusika mkuu katika tamthiliya hiyo) na yale ambayo baadhi ya watawala wetu wanayafanya leo. Ingawa katika tamthiliya hiyo kuna migogoro mingi, mgogoro mkubwa ni ule uliotokea kati ya Ngoswe (afisa wa Sensa) na Mzee Mitomingi na familia yake hasa baada ya Ngoswe kumdondokea Binti wa Mitomingi aitwaye Mazoea".
Kimsingi Serikali ya awamu ya tano inasisitiza uwajibikaji katika mahala pa kazi. Ubinafsi uwekwe pembeni lengo liwe kutumikia kwa kujituma. Haki iende sambamba na wajibu.
TAFAKARI CHUKUA HATUA