Mapenzi kabla ya ndoa je ni zinaa ! Ninawasiwasi

Msamiati

R I P
Mar 6, 2011
1,068
0
Kwa kweli nimejikaza sana lakini nimeona ni kheri ni hoji...... Kwa muujibu wa imani zote za dini hususan ukristo na uisilamu kufanya mapenzi kabla ya kuoana ni uzinzi, wakati huo huo tunafundishwa kuhusu uchumba kuwa ni kipindi cha kuangalliana, kuchunguzana, kuelewana na kuridhiana kabla ya kuoana
swali
Je kuchunguzana huko kunakamilikaje bila kuthibitisha background ya mwenzi wako kwenye mahusiano? inakuwaje kama umemuoa halafu unakuja kugundua kuwa amesha sex zaidi ya mara 5000 ukizingatia kuwa kwetu wakristo ukioa hutakiwi kuacha.

mimi ni mkristo ninamashaka na mafundisho tunayopewa kwenye imani yetu juu ya hili.

HOJA
Luka 16:18 "kila amuachaye mke na kuoa mke mwengine azini naye amwoaye yeye alieachwa na mumewe azini"

hapa najifunza kuwa uzinzi/zinaa ni kuacha na kuoa mwingine au kuoa alieachwa na sio kufanya mapenzi kabla ya ndoa.

SWALI Ukiwa kama mzazi, mlezi, ndugu au mshauri mwenye mapenzi mema kweli kabisa kutoka moyoni utamshauri kijana anaetaka kuoa
(a)
achunguze vyote lakini asimguse mwenzi wake mpaka atakapomuoa,,,,,,,!
ama
(b) asithubutu kuoa kabla ya kufanya nae mapenzi?

mwisho wa hoja yako andika jibu a au b tafadhali 

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,030
2,000
Kufanya tendo la ngono kabla ya kuhalalishwa ndo dhambi (Zinaa)
Kufanya tendo hilo na mtu mwingine ambaye si mke / mume wako ni dhambi pia (Uzinzi)

Kwa kuwa dhambi zote mbili zinahusisha kuharibu hekaru la Bwana; (mwili) kama kweli wewe utakuwa unaongozwa na ROHO MTAKATIFU; kabla hujaoa utaikimbia zinaa kama biblia inavyokushauri. Ila kama utakuwa unaongozwa na ROHO MTAKAVITU; unaona ni halali kufanya zinaa na mchumba wako!
Jibu sahihi ni a
 
Katufu

JF-Expert Member
May 8, 2012
523
500
Kama una mashaka na fundisho hilo basi una mashaka na imani nzima ya Kikristo, na ukiwa na mashaka na imani ya Kikristo basi wewe sio Mkristo (yaani anayemilikiwa, kutawaliwa na kuongozwa na Neno la Kristo). Na katika hoja yako hayo yanaonekana dhahiri na utafuta namna ya kuhalalisha uasherati kwa wachumba kwa kisingizio cha kuchunguzana. Ndoa za wazazi wetu kwanini zimedumu, wakati wao walikuwa hata hawafahamiani, bali waliangalia tabia za familia zao? Kwa ufupi angalia sana utaishia kuhalilisha dhambi
 
PetCash

JF-Expert Member
Mar 20, 2012
1,993
2,000
Kufanya tendo la ngono kabla ya kuhalalishwa ndo dhambi (Zinaa)
Kufanya tendo hilo na mtu mwingine ambaye si mke / mume wako ni dhambi pia (Uzinzi)

Kwa kuwa dhambi zote mbili zinahusisha kuharibu hekaru la Bwana; (mwili) kama kweli wewe utakuwa unaongozwa na ROHO MTAKATIFU; kabla hujaoa utaikimbia zinaa kama biblia inavyokushauri. Ila kama utakuwa unaongozwa na ROHO MTAKAVITU; unaona ni halali kufanya zinaa na mchumba wako!
Jibu sahihi ni a
RED - haliitwi tendo la ngono kwa sababu ukishasema 'ngono' tayari pana judgement attached hapo na ngono ni tendo baya. Wanandoa huwa hawafanyi ngono wanafanya 'mapenzi' ama 'tendo la ndoa'.
Ukifanya 'tendo la ndoa ' kabla ya ndoa then ndio ngono ama wazungu wanasema 'fornication'
Ukifanya 'tendo la ndoa' na mtu ambaye si mkeo/mumeo uku we uko ndani ya ndoa huo ndo 'uzinzi' ama wazungu husema 'adultery' au 'infidelity'
 
Suprise

JF-Expert Member
Nov 2, 2012
2,697
2,000
wewe nawe hilo ni swali au, we kama unataka jilipua jilipue tu lakini hakuna justification jina lolote utakaloita itabaki kua ni kinyume na taratibu na maagizo
 
Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,030
2,000
RED - haliitwi tendo la ngono kwa sababu ukishasema 'ngono' tayari pana judgement attached hapo na ngono ni tendo baya. Wanandoa huwa hawafanyi ngono wanafanya 'mapenzi' ama 'tendo la ndoa'.
Ukifanya 'tendo la ndoa ' kabla ya ndoa then ndio ngono ama wazungu wanasema 'fornication'
Ukifanya 'tendo la ndoa' na mtu ambaye si mkeo/mumeo uku we uko ndani ya ndoa huo ndo 'uzinzi' ama wazungu husema 'adultery' au 'infidelity'

Mi nafikiri tuko pamoja; mtoa uzi nafikiri anaogelea tendo hilo wakati hajafunga ndoa; nimekosea wapi kuliita hivyo?
 
EXTERMINATOR

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
344
0
Kumbe kuna cronometer ya kupima kitu imeingiliwa mara ngapi? Bado sikia miye.... 5000 times hahaaaaa. Na wewe utakuwa umeongeza 5001 hapo balaa kabisa.
 
Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,030
2,000
Kumbe kuna cronometer ya kupima kitu imeingiliwa mara ngapi? Bado sikia miye.... 5000 times hahaaaaa. Na wewe utakuwa umeongeza 5001 hapo balaa kabisa.

Anahesabu idadi ya miche iliyoingia au idadi ya pumping?
 
Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
53,967
2,000
Kufanya kabla ya ndoa ni uasherati...
usinnunue mbuzi kwenye gunia..........!!!!!
 
adakiss23

JF-Expert Member
Jan 23, 2011
3,831
2,000
Uasherati 2. Ndo maana Holy Quran inapinga sana hiyo kitu. Hata mtoto akizaliwa nje ya ndoa hatambuliki kisheria.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,374
2,000
I always believe in "SHAKING WELL BEFORE USE"...
lazima utest mzigo bana kabla ya kuutumia...hilo la uzinzi naona ni kama kubaniana tuu.......
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom