Huyu shost ni mwalimu wa primary, alifunga ndoa na mpenzi wake wa tangu secondary, walipomaliza form four A, mmoja alikwenda teaching mwingine alikwenda chuo cha Polisi Moshi. Baada ya kumaliza mafunzo walianza kazi na kutimiza ndoto yao ya kufunga ndoa.
Sasa bwana wamehamishiwa Dar kutoka mkoani, maisha wamepata watoto wanne. Mwanaume ameanza kuwa kijogoo, mara haonekani nyumbani wiki, shost anajiangalia na mshahara wake na watoto wanne haviendi. Mwisho mwanaume amemwambia yamekwisha kati yao atakua anasaidia matunzo ya watoto tu.
Shost kulia akajifijiria jiji la Dar hili na watoto wanne hajui ataanzia wapi, alipangisha vyumba viwili sehemu maisha yakaanza. Siku moja yuko kituoni anasubiri basi aende kazini kuna benzi imesimama, anapewa lift, kumbe yule baba alikuwa anaumoa kila siku akipita asubuhi, waliongea na kumpeleka mpaka shuleni kwake.
Baba yule alikuwa na maisha yake, aliishi nje ya nchi muda mrefu ndiyo amerudi nchini, hata mazingira hayajui vizuri lakini alijenga nyumba maeneo yale akiwa ughaibuni na ndiko anakokaa. Shost kumueleza maisha yake, basi mwanaume amefika bei, amemhamishia shost na watoto nyumbani kwake. Shost ananiambia kwa mara ya kwanza anapelekwa dinner 5* hotel na watoto wake wanabaki kushangaa.
Mwanaume amefika anataka kuoa, kasheshe mama wa mwanaume kusikia huyo mchumba wa mwanao ana watoto wanne amesononeka sana. Lakini ndiyo mtoto wake ameamua.
Kwa wale waliokata tamaa za maisha, hujui Mungu amekupangia nini mbele, wewe pigana tu.