Mapendekezo ya Kambi ya Upinzani katika hotuba

Aug 1, 2012
35
27
HOTUBA YA KAMBI YA UPINZANI IMEJAA MAPENDEKEZO KUHUSU SHIRIKISHO NA KUWADANGANYA WATANZANIA KWAMBA WAPINZANI HAWANA WAPENDEKEZO.
HAYA NI MAPENDEKEZO YA KAMBI YA UPINZANI YALIYOMO NDANI YA HOTUBA.

Kambiya Upinzani inashauri ifuatavyo ili Bunge hili liweze kuwa na taarifa zakina kuhusiana na kila hatua ambayo tunapiga kuelekea shirikisho la kisiasa laJumuiya ya Afrika Mashariki:

a. Iundwe kamati mpya ya kudumu yaBunge ambayo itakuwa inapokea na kujadili miswada, itifaki na mwenendo mzima wa Jumuiya na iwe nawajibu wa kutoa taarifa yake kwenye vikao vya Bunge mara kwa mara ili tuwezekuzijadili na kuishauri serikali kikamilifu. Aidha, Kamati hii iwe na jukumu lakushughulikia nidhamu ya Wabunge wa Afrika Mashariki.

b. Pawepo na vikao vya pamojabaina ya wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wanaotoka Tanzania na kamati hiiya Bunge ili kuweza kutoa taarifa za mara kwa mara kuhusiana na utendaji wao wakazi na masuala mbalimbali ya Jumuiya.

c. Tuwe na utaratibu wa kutoaelimu kwa wananchi kuhusiana na kila hatua ambayo imefikiwa ili kuepusha kuwana Jumuiya ya viongozi na badala yake iwe ni Jumuiya ya wananchi kwani watakuwana taarifa za kina kuhusiana na kila hatua iliyofikiwa.

d. Kabla ya itifaki mbalimbalikuridhiwa ni vema serikali ikaziwasilisha kwenye Bunge ili ziweze kujadiliwa nakupitishwa au kukataliwa na Bunge kama ambavyo tumekuwa tukifanya kwa zile zaKimataifa.

4.0 MAPENDEKEZO YA JUMLA KUHUSIANA JUMUIYA YAAFRIKA MASHARIKI
Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwaJumuiya ya Afrika mashariki inafanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuhakikisha kuwanchi yetu inakuwa sio kikwazo katika kufanikisha biashara kwenye Jumuiya, Kambiya Upinzani tunapendekeza hatua zifuatazo ziweze kuchukuliwa:

i. Ukaguzi wa mizigo mbalimbali unaofanywa na vyombovya dola kama vile Polisi na Mamlaka ya Mapato uwe unafanyika kwenye kituokimoja na sio kufanyika kila eneo kama ilivyosasa.

ii. Wataalamu wa masuala mbalimbali kama vile afya,ubora wa mazao, mifugo, samaki na bidhaanyingine mbalimbali wawe wanakaa kwenye vituo husika vya mipakani na sio kukaamaeneo ya makao makuu ya mikoa kama ilivyo sasa. Hili litapunguza usumbufu nakuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingia ndani ya mipaka zina ubora unaotakiwa.

iii. Vibali vya kuuza mazao mbalimbali viwe vinatolewakwa wakati na urasimu uondolewe ili kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wetuwanaweza kusafirisha mazao yao kwa wakati na hasa yale ya ndizi, matunda nambogamboga ambazo huharibika haraka kama yakicheleweshwa.

iv. Tozo ya dola za marekani 200 kwa kila gari yamizigo ambayo inaingia nchini kutoka miongoni mwa nchi za Jumuiya iondolewekwani huku ni kwenda kinyume na mkataba wa Afrika Mashariki kuhusu soko lapamoja na hali hii imekuwa ikilalamikiwa mara kwa mara kwenye vikao na kuifanyanchi yetu ionekane kama inakubali ila haitekelezi kama inavyopasa kuwa.

v.
Serikali iandae mazingira mazuri kwa wafanya kaziwa vituo vya mipakani kama vile kuwapatia nyumba, vifaa vya kazi, mahitaji muhimukama vile upatikanaji wa maji safi na salama, chanjo dhidi ya magonjwa kamaEbola na mengineyo ili kuwafanya waweze kuwa na ufanisi katika utendaji wao wakazi.

vi. Serikali iandae miundombinu mizuri na mazingirabora ya kibiashara ili kuhakikisha kuwa wananchi wanaweza kufanya biashara kwaurahisi zaidi kwenye maeneo ya mipakani.Kuhusu Majadiliano ya Ubia wa Kiuchumi (EPA) na Jumuiya ya Ulaya (EU)

Mheshimiwa Spika, kuhusu mwelekeo, hali na athari za Mkataba wa Ubia wa Uchumi kati yaJumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Tanzania kwa upande mmoja na Jumuiya yaUlaya (EU) kwa upande mwingine, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikalikuendelea kukumbuka kuwa sera yoyote ya uchumi ikiwa pamoja na Sera za Uchumiza Kimataifa, lazima zizingatie maendeleo endelevu, ukuaji ulio sawia(equitable growth) na unaoleta faida kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom