Elections 2010 Mapendekezo kwa CCM kufuatia "the Walkout"...

Unajua hili suala siyo kubwa wala gumu kiasi hicho; ninaamini mzigo wa jinsi gani litaisha ni kwa CCM. Wasipotumia hekima wanaweza kutengeneza mashujaa wengine tena wengi zaidi. Walipomfungia Zitto kwenye Buzwagi lilikuwa dogo kwenye hili itakuwa vurugu sana.
 
nimefuatilia kwa kina mwitikio wa watu mbalimbali na hususan wa viongozi wa ccm kufuatia the "walkout" a.k.a "kutoka nje" kulikofanywa na wabunge wa chadema jana. Hata hivyo nimejitolea kutoa ushauri ufuatao kwa viongozi wa ccm maana mwitikio wao hadi sasa unalenga kukoleza (escalate) mgongano wa kisiasa nchini. Ninaamini katika hali iliyopo mzigo wa busara na hekima unawaangukia ccm zaidi kuonesha ukomavu wa kisasa na demokrasia. Nina mambo kadhaa ya kushauri kupunguza (diffuse) hali ya utete iliyopo:

1. Ccm itambue mkorogano wa uchaguzi mkuu na hususan matatizo yaliyotokea katika utengazaji wa matokeo. Hadi hivi sasa inaonekana ccm hawajaonesha hata mara moja kutambua utata na mvurugano wa matokeo ya uchaguzi. Hii inawafanya waonekane hawajali jinsi gani uchaguzi unaendeshwa au matokeo yanatangazwa. Hivyo, jambo la kwanza ni kukubali kuwa utangazaji wa matokeo (hata kama umewanufaisha wao) haukuwa katika hali ya kujivunia. Wakubali tatizo ambalo mamilioni ya watanzania waliliona kufuatia uchaguzi mkuu.

2. Ccm ioneshe kutambua tatizo letu la tume ya uchaguzi ilivyoendesha utangazaji wa matokeo ya ubunge na urais kiasi cha kusababisha maelfu ya vijana wetu kurundikana katika vituo mbalimbali "kulinda kura". Kama taifa hatuwezi kwenda kwenye uchaguzi mwingine na mfumo huu kwani haumnufaishi yeyote zaidi ya kuweka msukumo katika jamii wakati wa uchaguzi ambao ungeweza kuleta madhara makubwa. Ccm ioneshe na yenyewe inataka tume inayofanya kazi kwa ufanisi, uhuru na uwazi. Ni kwa maslahi ya vyama vyote kuwa na tume iliyo huru, wazi na ya kisasa.

3. Ccm ioneshe kutokana na 1 na 2 hapo juu kuwa ipo haja ya kufanyia mabadiliko ya katiba hasa kwenye suala la kuzuia au kupinga matangazo ya kura za rais. Kwa wakati huu mfumo uliopo unaonekana kuinufaisha ccm. Lakini ni mfumo mbaya siku hali ikiwa kinyume na ccm. Kumbe ni kwa maslahi ya ccm na vyama vingine vyote kuweka utaratibu ambapo kura za rais haziwezi kuonekana zinapandikizwa au tume kulazimika kutangaza kwa sababu ikishatangaza basi hakuna wa kuhoji na wote wanatakiwa kupiga magoti kukubali matokeo hata kama kuna dalili ya upotofu. Ninaamini kwa chama kikongwe kama ccm ambacho kinajivunia kuwa ni "baba ya demokrasia" ni muhimu kuonesha kuwa hakiogopi mfumo mzuri na wa kisasa wa utangazaji wa kura za urais.

4. ccm isijaribu kwa namna yoyote kutekeleza tishio lake la kuwafukuza wabunge wa chadema bungeni. Tayari taifa limeshagawanyika na kitendo chochote kitakachoonekana kuwa ni cha kibabe (wengi tunakumbuka suala la zitto na buzwagi) kitakoleza mgongano wa kisiasa nchini. Kuwafukuza chadema hakutasababisha watu wakubali isipokuwa kama watawapeleka mahakamani watanzania wote ambao hawako tayari kutambua ushindi wa kikwete na kuwalazimisha kukubali ushindi huo chini ya tishio la kifungo. Vinginevyo, hekima kubwa inatakiwa kutumika na mimi ninaamini hekima hiyo inaanzia na:

- uongozi wa ccm uanzishe mazungumzo na uongozi wa chadema kujaribu kusikilizana. Nilitoa pendekezo la wagombea kukutana kabla ya uchaguzi kwani niliamini wakati ule ndio ulikuwa wakati muafaka wa kufanya hivyo kabla hatujafika hapa tulipofika, na wakiendelea kuringishiana mapembe watajikuta wanalazimishwa kukaa chini huku machozi yanatoka. Tusifike huko.
- kanuni za makubaliano zitengenezwe ili maridhiano yaanze; lakini ni lazima ziwe kanuni zenye kukubali hali halisi na zenye msingi wa haki na uwazi. Mazungumzo yasifanyike katika masharti kabla ya mazungumzo (pre-conditions).

5: Endapo ccm haitaona ulazima wa kufanyia kazi mapendekezo hayo kwa sababu "wameshinda" na kuwa hawako tayari kukubali kufanya mazungumzo na chadema kwa kisingizio au sababu yoyote ni wazi kuwa wanalazimisha watu wenye dhamira tofauti kutii dhamira zao kuliko vitisho. Vitisho, mikwara, au hatua ambazo zitaonekana kuwalazimisha watu kupiga magoti kwa kutii kunaweza kuwatisha baadhi ya watu lakini kamwe hazijawahi kufanikiwa mahali popote duniani kuwatiisha watu wote wakati wote. Ndio maana nasema hekima inahitajika kuliko nguvu au vitisho vya nguvu.

6. Ni matumaini yangu kuwa chadema nao hawajafunga mlango wa mazungumzo na watakuwa tayari kuwasikiliza ccm katika hali ya udugu, na uelewano wa kisiasa. Vinginevyo kidemokrasia ninaamini mgawanyiko uliopo ni mzuri na unakoleza tofauti za kisasa na hivyo kutuletea mapendekezo tofauti kabisa ya mwelekeo wa taifa. Katika demokrasia hatuwezi wote kuimba wimbo mmoja, kucheza ngoma moja na wote kukubaliana mtazamo mmoja. Ni muhimu kutambua kuwa ni katika tofauti zetu ndio demokrasia hukolezwa, na kudumishwa. Lakini ni muhimu tofauti hizo zisifikie uhasama wa kisiasa (political hostility) kitu ambacho ninaamini kinategemea kwa asilimia 100 maamuzi yatakayofanywa na ccm.

Ndiyo hoja zangu na ninazisimamia.
Mmm
hawana ubavu wa kutekelza hilo kwemye red hapo juu. Hata spika mahiri sitta amewaambia kuwa hawana ubavu wa kuifanya chadema chochote.
 
- Uongozi wa CCM uanzishe mazungumzo na Uongozi wa CHadema kujaribu kusikilizana. Nilitoa pendekezo la wagombea kukutana kabla ya uchaguzi kwani niliamini wakati ule ndio ulikuwa wakati muafaka wa kufanya hivyo kabla hatujafika hapa tulipofika, na wakiendelea kuringishiana mapembe watajikuta wanalazimishwa kukaa chini huku machozi yanatoka. Tusifike huko.

MMM

Mie naona lengo la 'WALK OUT' ilikuwa kufikisha ujumbe na dunia imeshaona picha inaishia hapo.

Suala la kushauri mazungumzo ya CCM na Chadema unamaana uanzishwa muafaka wa Tanzania Bara? Haielekei kama watawala wanakubali kwenda mezani kirahisi namna hiyo, kwani tuliona CUF wakisusia Bunge kwa miaka 3 na wakati huo walikuwa na mtaji wa kutosha kule Zanziba.
Mie nashauri kwanza Chadema kwanza wakusanye mtaji wa kisiasa wa kutosha na hapo tutayaona mabadiliko ya kweli. Hili la 'WALK OUT' ni sawa na kurusha jiwe kwenye kichaka kuona kama kuna chochote?
 
Pamoja na yote CCM watambue kuwa gharama ya kurudia uchaguzi ni ndogo kuliko kurudisha amani ambayo wanataka kuipoteza (QUOTE)

Yaani CCM wanataka kupoteza amani? Nani anasema CCM ndio waliolikoroga hili. CHADEMA ndio wnaolikoroga lengo la CHADEMA ni kuleta uasi katika nchi ili ionekane this country cant be governed. CHADEMA ni lazima waombe radhi.
 
4. CCM isijaribu kwa namna yoyote kutekeleza tishio lake la kuwafukuza wabunge wa Chadema Bungeni. Tayari taifa limeshagawanyika na kitendo chochote kitakachoonekana kuwa ni cha kibabe (wengi tunakumbuka suala la Zitto na Buzwagi) kitakoleza mgongano wa kisiasa nchini. Kuwafukuza CHADEMA hakutasababisha watu wakubali isipokuwa kama watawapeleka mahakamani Watanzania wote ambao hawako tayari kutambua ushindi wa Kikwete na kuwalazimisha kukubali ushindi huo chini ya tishio la kifungo. Vinginevyo, hekima kubwa inatakiwa kutumika na mimi ninaamini hekima hiyo inaanzia na:(QUOTE)

CHADEMA ni lazima wafukuzwe BUNGENI halafu tuone watakachofanya. Baadhi ya viongozi wa CHADEMA hawana busara hata kidogo. Wengi wao hawafai hata kuongoza kata. Wameukwaa ubunge kutokana na makosa ya CCM yenyewe. Lengo la CHADEMA ni kutaka amani ivurugike. Sasa kuiomba CCM eti itumie busara wakati kuna wana-CHADEMA wanataka siasa za ubabe ni kutaka kuionea CCM. CHADEMA wamelianzisha na sasa wawe tayari kukabiliana nalo. Wamelilia wembe na wembe huo wataupata. Tuone huyo Mbowe atafanya nini, Tuone huyo LISSU atafanya nini.
 
.............Watanzania wote ambao hawako tayari kutambua ushindi wa Kikwete na kuwalazimisha kukubali ushindi huo chini ya tishio la kifungo..............(QUOTE).

Hatutaki unafiki hapa. Je, unasemaje wale milioni tano na ushee waliomchagua KIKWETE?
 
Hakuna cha kufukuzwa bungeni inawauma sana. Mmezoea kula kiulaini safari hii ni shike mshike mtindo moja. hapo kwenye red sijui ilitoa wapi ujasiriw wa kuwataja, ukitaka kujua watafanya nini ccm iendeleze kuraise hiyo issue ya ku walk out.
 
.............Watanzania wote ambao hawako tayari kutambua ushindi wa Kikwete na kuwalazimisha kukubali ushindi huo chini ya tishio la kifungo..............(QUOTE).

Hatutaki unafiki hapa. Je, unasemaje wale milioni tano na ushee waliomchagua KIKWETE?

Mwacheni huyu, hajui asemalo! Hajawahi kuona utamu wa vurugu! Walk out ile ni badala ya CHADEMA kuingia majukwani na kuishitaki tume kwa watu! Ingefanyika hivi, madhara yake yangekuwa makubwa mno na ya mateso. Kwa kufanya walichofanya wananchi na wale wachadema ambao walitegemea action kutoka kwa chama chao wamepata faraja, na hivi kupunguza hasira zao. CCM akiamsha tena hasira za hawa, laana itabaki kwake. CHADEMA kwa upande wao, wamefikisha ujumbe na wakae tayari kushiriki katika mazungumzo ya nini hitima ya Tume na matokeo.

Inaniuma sana ninaposoma na kuwasikia CCM wakitishia amani yetu kwa kutumia mlango wa nyuma. JK amekuwa akichochochea hisia za dini katika hotuba na matendo yake,huku akiwatuhumu wengine, na sasa nasoma JF eti pia na ukabila umo. Hizi ni mbinu za kuhalalisha hali ya hatari katika taifa hili. Ni CCM atakayeingiza NChi hii katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe! CCM watumie busara sasa, wapate kuchukua medali ya kuendeleza utamaduni wa utulivu na amani wa taifa hili, kwa vingine wao ndio wa kulaaniwa kwa lolote libaya likitokea kutokana na kauli na makusudio yao!
 
CCM leo wamefunga Macho na kusema hakuna kitu kipya ila huko mbele kwe kizazi hiki cha dot.com itakuwa na kazi kubwa sana kwa ajili ya mambo kama haya, hivyo kuna kila ulazima wa CCM kufanya mazungumzo na CHADEMa na siyo kufanya kama vile hakuna kitu,
 
CCM watatekeleza hilo hapo juu hadi hapo wafadhili watakaposimamisha misaada yao kama walivyomfanyia Mzee Moi pale kenya..............
SMZ ilisurvive , licha ya kususiwa na wafadhili baada ya CUF kutomtambua Komandoo. 1995-2000.
 
4. CCM isijaribu kwa namna yoyote kutekeleza tishio lake la kuwafukuza wabunge wa Chadema Bungeni. Tayari taifa limeshagawanyika na kitendo chochote kitakachoonekana kuwa ni cha kibabe (wengi tunakumbuka suala la Zitto na Buzwagi) kitakoleza mgongano wa kisiasa nchini. Kuwafukuza CHADEMA hakutasababisha watu wakubali isipokuwa kama watawapeleka mahakamani Watanzania wote ambao hawako tayari kutambua ushindi wa Kikwete na kuwalazimisha kukubali ushindi huo chini ya tishio la kifungo.

MMM
Hili la kuwafukuza wabunge wa CHADEMA lina mzizi gani katika sheria na kanuni za bunge au katiba yetu? sioni namna ambayo wabunge wa ccm wanaweza kutekeleza hili. sana sana kwa kutumia wingi wao wangeweza kutoa adhabu ya kuwasimamisha kwa muda kama walivyofanya kwa zitto, lakini sio kuwafukuza. kufukuza ni kufukuza kwelikweli hivyo tuwe makini na lugha. naona ccm wanatumia tishio ili kuwatisha CHADEMA. na wakijaribu kutekeleza nia hiyo, basi watakuwa wamelihakikishia taifa kwamba wao ni mufilisi katika ukomavu wa kisiasa. wanaweza kuambulia majeraha makubwa zaidi ya haya waliyokwishapata katika ulingo wa siasa
 
Something terrible is going to happen in TZ coz CCM still thinks hii ni TZ ya 1947!!! we know our rights and we are fighting for it. CHADEMA sio wajinga kuamua kutomtambua raisi, lazima kuna kitu na hicho kitu CCM wanakijua sema kwa vile wameshika makali ndo maana wanawaonea wapinzani. Kwanini wasiweke wazi hasa kilichojiri hadi CHADEMA kususa??? Kama Kikwete anaamini alishinda anaogopa nini kurudia uchaguzi??Nahisi anajua ataambulia 2% ya kura zote kwa vile wananchi wengi hawamtaki tena kwa kuendekeza mafisadi na undugunization na udinization serikalini......!

UCHAGUZI URUDIWE KAMA CCM WANAJIAMINI WALISHINDA KIHALALI
 
4. CCM isijaribu kwa namna yoyote kutekeleza tishio lake la kuwafukuza wabunge wa Chadema Bungeni. Tayari taifa limeshagawanyika na kitendo chochote kitakachoonekana kuwa ni cha kibabe (wengi tunakumbuka suala la Zitto na Buzwagi) kitakoleza mgongano wa kisiasa nchini. Kuwafukuza CHADEMA hakutasababisha watu wakubali isipokuwa kama watawapeleka mahakamani Watanzania wote ambao hawako tayari kutambua ushindi wa Kikwete na kuwalazimisha kukubali ushindi huo chini ya tishio la kifungo. Vinginevyo, hekima kubwa inatakiwa kutumika na mimi ninaamini hekima hiyo inaanzia na:(QUOTE)

CHADEMA ni lazima wafukuzwe BUNGENI halafu tuone watakachofanya. Baadhi ya viongozi wa CHADEMA hawana busara hata kidogo. Wengi wao hawafai hata kuongoza kata. Wameukwaa ubunge kutokana na makosa ya CCM yenyewe. Lengo la CHADEMA ni kutaka amani ivurugike. Sasa kuiomba CCM eti itumie busara wakati kuna wana-CHADEMA wanataka siasa za ubabe ni kutaka kuionea CCM. CHADEMA wamelianzisha na sasa wawe tayari kukabiliana nalo. Wamelilia wembe na wembe huo wataupata. Tuone huyo Mbowe atafanya nini, Tuone huyo LISSU atafanya nini.

Ukibishana na mnywa togwa........!!!!

Haya bana 1954 uwanja wako:peace:
 
WEWE 1954 unajua unachokiandika au Wewe ndi zao la Makamba baada ya kumbaka Mwanafunzi na kumtia mimba.Ni wabuge gani makini wenye busara CHADEMA au ccm?Mbunge mmoja wa CHADEMA =Wabunge 70 wa ccm hawana busara na wala hawajui wanachokiwajkirisha bungeni CCM kuongozwa na watu kamaMakamba Chilingati na huyo Kikwete ni maafa makubwa kwa taifa letu hawa ni chaguo lamafisadi.Mafisadi sio wajinga ili waendelee kutunyonya lazima watafute viongozi dhaifu.CHADEMA ni wabunge 49! lakini baada ya kumtolea nje JK na sisimu wanakosa usingizi kwanini wakose usingizi?Bunge la mwaka huu ni tamu WEWEW unwedwi CCM iwafukuze wabunge wa CHADEMA nafahamu watawanyima usingizi wabunge wa ccm bungeni ambaowamezoea kulala na wanapoamkawanapiga kura hata bila kujua nini wamekipigia kuara!Na hata wakiamka hawana cha kufanya kwani hapo sio mahala pao.Mbunge wa ccm anapogombea ubunge wa SADC bila hata kujua kirefu cha SADC1??Wapo wengi ambao hata hawafahamu majina ya majibo yao!!!!????!!!!MUNGU IBARIKI TANZANIA
4. CCM isijaribu kwa namna yoyote kutekeleza tishio lake la kuwafukuza wabunge wa Chadema Bungeni. Tayari taifa limeshagawanyika na kitendo chochote kitakachoonekana kuwa ni cha kibabe (wengi tunakumbuka suala la Zitto na Buzwagi) kitakoleza mgongano wa kisiasa nchini. Kuwafukuza CHADEMA hakutasababisha watu wakubali isipokuwa kama watawapeleka mahakamani Watanzania wote ambao hawako tayari kutambua ushindi wa Kikwete na kuwalazimisha kukubali ushindi huo chini ya tishio la kifungo. Vinginevyo, hekima kubwa inatakiwa kutumika na mimi ninaamini hekima hiyo inaanzia na:(QUOTE)

CHADEMA ni lazima wafukuzwe BUNGENI halafu tuone watakachofanya. Baadhi ya viongozi wa CHADEMA hawana busara hata kidogo. Wengi wao hawafai hata kuongoza kata. Wameukwaa ubunge kutokana na makosa ya CCM yenyewe. Lengo la CHADEMA ni kutaka amani ivurugike. Sasa kuiomba CCM eti itumie busara wakati kuna wana-CHADEMA wanataka siasa za ubabe ni kutaka kuionea CCM. CHADEMA wamelianzisha na sasa wawe tayari kukabiliana nalo. Wamelilia wembe na wembe huo wataupata. Tuone huyo Mbowe atafanya nini, Tuone huyo LISSU atafanya nini.
 
Pamoja na yote CCM watambue kuwa gharama ya kurudia uchaguzi ni ndogo kuliko kurudisha amani ambayo wanataka kuipoteza (QUOTE)

Yaani CCM wanataka kupoteza amani? Nani anasema CCM ndio waliolikoroga hili. CHADEMA ndio wnaolikoroga lengo la CHADEMA ni kuleta uasi katika nchi ili ionekane this country cant be governed. CHADEMA ni lazima waombe radhi.

Amekuambia nani kuwa CHADEMA iatomba radhi? Democrasia haipimwi kwa kijiko walichofanya CHADEMA ni haki yao ya kiraia. Mbona Kawawa alipiokwenda kule machame kuwaleza wanachi kuhusu uanzishwaji wa vijiji vya ujamaa(centralization) mwaka 1975 wananchi walimgeukia na kumwonyesha ****** na wanawake wote walivua nguo. Ina maana huwezi wewe ukaamka asubuhi na kujitwalia utawala unavyotaka. Kambarage alimwita na kumweleza kuwa umewakosea wale wananchi. Ilibidi wizara iandike barua kuomba msamaha.

Sasa chadema leo hii wanayarudia yale ya kile kipindi wao wanamakosa. Je NEC wao waliotangaza kuwa mrema wa TLp kapanda ktk asilimia za kura alizopata hilo sio kosa kwa NEC na hili halionekani. Haya ndo CHADEMA wanayolilia na sio Rais ila kura alizopata utaratibu sio vile ulivyokusudiwa. Kuna shida gani CCM ikasema turudie uchaguzi?
 
4. CCM isijaribu kwa namna yoyote kutekeleza tishio lake la kuwafukuza wabunge wa Chadema Bungeni. Tayari taifa limeshagawanyika na kitendo chochote kitakachoonekana kuwa ni cha kibabe (wengi tunakumbuka suala la Zitto na Buzwagi) kitakoleza mgongano wa kisiasa nchini. Kuwafukuza CHADEMA hakutasababisha watu wakubali isipokuwa kama watawapeleka mahakamani Watanzania wote ambao hawako tayari kutambua ushindi wa Kikwete na kuwalazimisha kukubali ushindi huo chini ya tishio la kifungo. Vinginevyo, hekima kubwa inatakiwa kutumika na mimi ninaamini hekima hiyo inaanzia na:(QUOTE)

CHADEMA ni lazima wafukuzwe BUNGENI halafu tuone watakachofanya. Baadhi ya viongozi wa CHADEMA hawana busara hata kidogo. Wengi wao hawafai hata kuongoza kata. Wameukwaa ubunge kutokana na makosa ya CCM yenyewe. Lengo la CHADEMA ni kutaka amani ivurugike. Sasa kuiomba CCM eti itumie busara wakati kuna wana-CHADEMA wanataka siasa za ubabe ni kutaka kuionea CCM. CHADEMA wamelianzisha na sasa wawe tayari kukabiliana nalo. Wamelilia wembe na wembe huo wataupata. Tuone huyo Mbowe atafanya nini, Tuone huyo LISSU atafanya nini.
mMitanzania ya leo bana?
 
MWANAKIJIJI UMEIFANYA SIKU YANGU IWE NZURI. Mawazo yako ni "simple and clear" but with very heavy message.

Unajua mabavu hayawezi saidia kitu na hawa CCM wamesahau yaliyotokea PEMBA miaka ya nyuma ambapo watu walitiliana sumu hadi visimani!

Hali hii hatutaki itokee TZ na sie ni nchi kubwa kulinganisha na visiwa vya Pemba na Unguja patakuwa hakuna pa kukimbilia. Majirani zetu karibu wote wamepitia misukosuko ya umwagaji damu sababu ya ubabe tu wa mtu mmoja na mifano tunayo vichwani mwetu.

Jambo la hekima ni kukaa pamoja na kujadili kuondoa kasoro au hata CCM kuomba radhi kuliko kujifanya eti wao ni wenye nchi peke yao.

Kitendo cha wabunge wa CCM kuwazomea wenzao wa CDM kilionyesha wazi jinsi gani wabunge hao wasivyotumia akili zao kuchambua mambo na kufanya kitendo cha kitoto kama hicho. Wangetumia busara, wangekaa kimya wakawaacha wenzao watoke bila zogo.

Kitendo cha raisi kurusha vijembe kuwakebehi CDM kinaweza kucost taifa, maana watu bado wana vidonda vya uchaguzi sasa kukebehi na kusema eti hawana pa kwenda ni kuamsha hasira zaidi kwa wapiga kura.

Najua vijembe ni sehemu ya siasa, lakini havikustahili kusemwa siku hiyo sababu ilikuwa ni issue very serious siyo ya kukebehi.
Kwani Mzah mzaha hutumbua usaha!

CCM wakumbuke pia kuna kundi kubwa la watu wamekata tamaa na maisha na wako tayari kufanya lolote bila kujali lina gharama gani kwa maisha yao kwa ujumla.

Nilitegemea wakongwe wa CCM km kina Mzee Malechela wangetoa busara zao kuliko kuwaachia kina Chiligati ambao wanazidi kukasirisha Wapenda Demokrasia hapa TZ na duniani kwa ujumla.

Napenda wahusika wayachukue maoni ya Mwanakijiji na kuyafikisha kwa wahusika yaweze kufanyiwa kazi.

Nawasilisha.
 
You don't ask for your tights rather you demand your rights, sasa Chadema wamekuwa waungwana sana na pia wanaonyesha kuweka maslahi ya taifa mbele sana, kwa lile vugu vugu iliyokuwepo wakati wa kutangaza matokeo wangeamua kuwatangazia watanzania kuingia mtaani kudai haki yao hivi hata hilo bunge leo lingezinduliwa!! tuwe wakweli CCM wamefanya wizi na hakika wanajua kama ni wezi!! don't tell me kwamba hawana hata akili ya kujua kuwa watanzania wanajuwa kuwa wamepokonywa haki yao!! Hivi nani mkosaji kati ya hawa wawili yule anayepiga kelele au ukunga wa mwizi, mwizi, mwizi ama ni yule mwizi aliyeiba? anachofanya chadema ni kumpigia ukunga mwizi, you can't have it both ways huku unakwiba na huku unataka ustaarabu wa kutokuitwa mwizi. CCM waache udhalimu , mabaya waliokwisha kutufanyia watanzania yametosha wasitake mengine, Lakini lawama kubwa zaidi ni hawa watu wanaofanya kazi bila kufuata ethics za kazi zao watumishi wa umma ama watumishi wa taasisi za serikali wanapogeuka kuwa vibaraka wa CCM!! Maana kama Tume ya uchaguzi wangekataa kata kata kutumiwa na CCM kufanya waliofanya haya yote yangetokea wapi, hapa lawama wala si katiba , hapa lawama na laana zielekwezwe kwa watu wa tume na taasisi nyingine zilizopelekea uchaguzi kutokuwa huru na haki, inakuwaje watu wameona yaliyotokea kenya kwa makosa ya Tume ya uchaguzi ya kenya leo hii Tume ya Tanzania inafanya yale yale!! hawa watu wa Tume sioni hata adhabu wanayostahili ukiwacha kuwanyonga adharani maana uroho wao unataka kusababisha taifa liingie katika kukosa amani yake. Mimi siwalaumu CCM sana maana Tume hawakuforciwa kuiba at gun point!! wangeweza kuwa wakweli au wakasema tunajiuzuru we would not be talking about this today.
Nashauri watumishi wa serikali na taasisi zake watambue kuwa wanalipeleka taifa kubaya kwa kuacha kufanya kazi kwa mujibu wa taratibu na kugeuka kuwa vibaraka wa CCM hawa ndo wanastahili adhabu kwanza alafu ifuatie CCM kwa kuwashawishi watumishi wa serikali, na mwisho CCM at least waoneshe kuwa dhamira inawasuta kwa wale waliotenda hivi watuonyeshe ustaarabu japo kidogo
Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom