Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,733
- 40,846
Nimefuatilia kwa kina mwitikio wa watu mbalimbali na hususan wa viongozi wa CCM kufuatia the "walkout" a.k.a "kutoka nje" kulikofanywa na wabunge wa Chadema jana. Hata hivyo nimejitolea kutoa ushauri ufuatao kwa viongozi wa CCM maana mwitikio wao hadi sasa unalenga kukoleza (escalate) mgongano wa kisiasa nchini. Ninaamini katika hali iliyopo mzigo wa busara na hekima unawaangukia CCM zaidi kuonesha ukomavu wa kisasa na demokrasia. Nina mambo kadhaa ya kushauri kupunguza (diffuse) hali ya utete iliyopo:
1. CCM itambue mkorogano wa uchaguzi mkuu na hususan matatizo yaliyotokea katika utengazaji wa matokeo. Hadi hivi sasa inaonekana CCM hawajaonesha hata mara moja kutambua utata na mvurugano wa matokeo ya uchaguzi. Hii inawafanya waonekane hawajali jinsi gani uchaguzi unaendeshwa au matokeo yanatangazwa. Hivyo, jambo la kwanza ni kukubali kuwa utangazaji wa matokeo (hata kama umewanufaisha wao) haukuwa katika hali ya kujivunia. Wakubali tatizo ambalo mamilioni ya Watanzania waliliona kufuatia uchaguzi mkuu.
2. CCM ioneshe kutambua tatizo letu la Tume ya Uchaguzi ilivyoendesha utangazaji wa matokeo ya Ubunge na Urais kiasi cha kusababisha maelfu ya vijana wetu kurundikana katika vituo mbalimbali "kulinda kura". Kama Taifa hatuwezi kwenda kwenye uchaguzi mwingine na mfumo huu kwani haumnufaishi yeyote zaidi ya kuweka msukumo katika jamii wakati wa uchaguzi ambao ungeweza kuleta madhara makubwa. CCM ioneshe na yenyewe inataka Tume inayofanya kazi kwa ufanisi, uhuru na uwazi. Ni kwa maslahi ya vyama vyote kuwa na Tume iliyo huru, wazi na ya kisasa.
3. CCM ioneshe kutokana na 1 na 2 hapo juu kuwa ipo haja ya kufanyia mabadiliko ya Katiba hasa kwenye suala la kuzuia au kupinga matangazo ya kura za Rais. Kwa wakati huu mfumo uliopo unaonekana kuinufaisha CCM. Lakini ni mfumo mbaya siku hali ikiwa kinyume na CCM. Kumbe ni kwa maslahi ya CCM na vyama vingine vyote kuweka utaratibu ambapo kura za Rais haziwezi kuonekana zinapandikizwa au Tume kulazimika kutangaza kwa sababu ikishatangaza basi hakuna wa kuhoji na wote wanatakiwa kupiga magoti kukubali matokeo hata kama kuna dalili ya upotofu. Ninaamini kwa chama kikongwe kama CCM ambacho kinajivunia kuwa ni "Baba ya Demokrasia" ni muhimu kuonesha kuwa hakiogopi mfumo mzuri na wa kisasa wa utangazaji wa kura za Urais.
4. CCM isijaribu kwa namna yoyote kutekeleza tishio lake la kuwafukuza wabunge wa Chadema Bungeni. Tayari taifa limeshagawanyika na kitendo chochote kitakachoonekana kuwa ni cha kibabe (wengi tunakumbuka suala la Zitto na Buzwagi) kitakoleza mgongano wa kisiasa nchini. Kuwafukuza CHADEMA hakutasababisha watu wakubali isipokuwa kama watawapeleka mahakamani Watanzania wote ambao hawako tayari kutambua ushindi wa Kikwete na kuwalazimisha kukubali ushindi huo chini ya tishio la kifungo. Vinginevyo, hekima kubwa inatakiwa kutumika na mimi ninaamini hekima hiyo inaanzia na:
- Uongozi wa CCM uanzishe mazungumzo na Uongozi wa CHadema kujaribu kusikilizana. Nilitoa pendekezo la wagombea kukutana kabla ya uchaguzi kwani niliamini wakati ule ndio ulikuwa wakati muafaka wa kufanya hivyo kabla hatujafika hapa tulipofika, na wakiendelea kuringishiana mapembe watajikuta wanalazimishwa kukaa chini huku machozi yanatoka. Tusifike huko.
- Kanuni za makubaliano zitengenezwe ili maridhiano yaanze; lakini ni lazima ziwe kanuni zenye kukubali hali halisi na zenye msingi wa haki na uwazi. Mazungumzo yasifanyike katika masharti kabla ya mazungumzo (pre-conditions).
5: Endapo CCM haitaona ulazima wa kufanyia kazi mapendekezo hayo kwa sababu "wameshinda" na kuwa hawako tayari kukubali kufanya mazungumzo na Chadema kwa kisingizio au sababu yoyote ni wazi kuwa wanalazimisha watu wenye dhamira tofauti kutii dhamira zao kuliko vitisho. Vitisho, mikwara, au hatua ambazo zitaonekana kuwalazimisha watu kupiga magoti kwa kutii kunaweza kuwatisha baadhi ya watu lakini kamwe hazijawahi kufanikiwa mahali popote duniani kuwatiisha watu wote wakati wote. Ndio maana nasema hekima inahitajika kuliko nguvu au vitisho vya nguvu.
6. Ni matumaini yangu kuwa CHadema nao hawajafunga mlango wa mazungumzo na watakuwa tayari kuwasikiliza CCM katika hali ya udugu, na uelewano wa kisiasa. Vinginevyo kidemokrasia ninaamini mgawanyiko uliopo ni mzuri na unakoleza tofauti za kisasa na hivyo kutuletea mapendekezo tofauti kabisa ya mwelekeo wa taifa. Katika demokrasia hatuwezi wote kuimba wimbo mmoja, kucheza ngoma moja na wote kukubaliana mtazamo mmoja. Ni muhimu kutambua kuwa ni katika tofauti zetu ndio demokrasia hukolezwa, na kudumishwa. Lakini ni muhimu tofauti hizo zisifikie uhasama wa kisiasa (political hostility) kitu ambacho ninaamini kinategemea kwa asilimia 100 maamuzi yatakayofanywa na CCM.
Ndiyo hoja zangu na ninazisimamia.
MMM