Mapato ya mbunge wa bunge la Tanzania kabla ya kujiongezea posho

duh kumbe hawa mabwana hawapati hela 7.2m ni kidogo ukichukulia wanatoa hela yao mfukoni kwa sababu serikali yetu haina fungu la maendeleo ya kila wilaya/constituency kama vile Kenya...wanatakiwa angalau kulipwa 15mil ...kumbuka wabunge wengi wanahudumia miradi na matumizi ya kila siku ya familia huko majimboni

Red: Kazi za mfuko wa jimbo ni zipi, maana kila mwezi kuna pesa inayotengwa kwa madhumini hayo

Blue: Si kazi ya Mbunge kuhudumia familia za wana jimbo, kila mwananchi anajihudumia kwa kufanya kazi halali. Mshahara wa mbungu ni kwa ajili yake yeye na familia yake. Mbona sijasikia Rais akisema anahudumia familia zote za Tanzania kwa mshahara wake?
 
Hiyo namba 3 sijailewa vizuri, ina maana anapewa hy posho ya ml 1 bila kufanya chochote au!?
 
WABUNGE

1.Mshaharakwa mwezi tshs 2,300,000/=
2.Mafuta ya gari kwa mwezi 4,000,000/=i.e ltr 1000
3.Posho ya ubunge kwa mwezi 2,000,000/=
4.Posho ya kukaa bungeni kwa siku 80,000 X SIKU 16 KWA MWEZI/= 2,280,000/=
5.Posho ya kuendesha ofisi kwa mwezi 1,700,000/=
6.Simu ya mkononi kwa mwezi 500,000/=

hayo ni malipo akiwa mbunge tu akiwa waziri au naibu waziri si anaondoka na 20m, mi naona wabunge wasiwe mawaziri wala manaibu waziri au wakuu wa mikoa au wilaya, pili posho zote zifutwe walipwe mshara kama wengine kama hawataki waache tuone kama kweli wana uwezo huo. na mishahara yao ikatwe kodi. haiwezekani watu wanalipwa laki tatu kwa mwezi na bado wanaishi halafu wao wanapokea 7.2m bado wanaona ndogo huku si kuuana huku? waache dogodogo na nyama choma.
 
katiba mpya-kazi zauwakilishi ambazo sio za kuajiriwa hazina mshahara ziwe na posho tu tena ya vikao. Wapo wenye moyo wa uzalendo watazifanya tu.
 
Ndo maana sasa hivi watu wanaacha professional zao wanakimbilia ubunge, manake ndio unaolipa atii!

madaktari wameomba m3 wakaonekana wana tamaa.hebu fikiria daktari aliyesoma miaka 7 mpaka 10 na kazi anayoifanya halafu mlinganishe na profesa maji marefu.
 
Kiina cha kuongezwa posho ama mshahara ni good working performance.sasa hali ya Taifa kiuchumu ndiyo hivyo tena.Wanatakiwa waperform kwa kuibana serekali ya CCM ili mfumuko wa bei upungue. Hata kama wakiongezwa posho na mfumuko wa bei ukazidi kwenda juu.Bado hadithi itakue ile ile

Kuna vijana wasomi wanamaliza viatu barabarani kutafuta kazi zenye misharaha hata ya 500,000.Wakiambiwa wabunge wote wenye tamaa ya posho wameachia ngazi na nafasi zao ziko wazi!Patakua hapatoshi
 
spika kinda kasema hazimtoshi,na yaelekea tupo gizani upande wa kuheshimu taaluma za watu.ila yashangaza dr maji marefu tshs 86,400,000/mwaka,dr wa kweli anafika kiasi hicho?yaelekea maji matitu alifanya sana kazi wakat wa kampen 2010-15!
 
Wapo wengi ambao hicho kipato kinawatosha,tatizo la wabunge wetu wanataka kuwa wafadhili wa watu ili kesho wapigiwe kura,namna hiyo lazima hela yeyote itakuwa ndogo.badala ya kusimamia serikali vizuri ili kodi za wananchi zifanye kazi zake sawasawa wao wanapiga mabenchi hata kwa point za ajabu,Huwa nataka kulia wakati fulani nikiangalia Bunge.Jamani tuache mzaha 2015 hembu wapeni pasi CDM muonje angalau mema ya Nchi hii,na tuwe kama USA unakipa chama kisipo deliver unaweka kingine,hakuna kurembua katika keki ya taifa.
 
Hivi makinda anasema m.7 hazitoshi kwa mwezi je angekua mwalim si angejinyonga
 
maisha ni magumu kwa watanzania wote kwasasa ivo serikali sikivu inabidi kuangalia sekta zote kwa makini ili kuboresha posho za wafanyakazi wote
 
Naona sasa tunapoelekea itakuwa ni aibu mtu kuwa MBUNGE. Maana wanaacha majukumu ya kusemea wapiga kura na kujisemea wao wenyewe. Self serving!
 
Wapo wengi ambao hicho kipato kinawatosha,tatizo la wabunge wetu wanataka kuwa wafadhili wa watu ili kesho wapigiwe kura,namna hiyo lazima hela yeyote itakuwa ndogo.badala ya kusimamia serikali vizuri ili kodi za wananchi zifanye kazi zake sawasawa wao wanapiga mabenchi hata kwa point za ajabu,Huwa nataka kulia wakati fulani nikiangalia Bunge.Jamani tuache mzaha 2015 hembu wapeni pasi CDM muonje angalau mema ya Nchi hii,na tuwe kama USA unakipa chama kisipo deliver unaweka kingine,hakuna kurembua katika keki ya taifa.

Sawa kabisa mkuu.
 
1.Mshahara kwa mwezi tshs 2,300,000/=
2.Mafuta ya gari kwa mwezi 2,000,000/=i.e ltr 1000 kwa mwezi
3.Posho ya ubunge kwa mwezi 1,000,000/=
4.Posho ya kukaa bungeni kwa siku 80,000/=
5.Posho ya kuendesha ofisi kwa mwezi 700,000/=
6.Simu ya mkononi kwa mwezi 500,000/=
Jumla ya mapato hayo ni7,200,000/=ukiachilia mbali posho za vikao vya kamati mbali mbali na safari za nje. bado wameona pato hilo kwa mwezi halitoshi wamejiongezea posho ya vikao mpaka 200,000/= kwa kisingizio kuwa maisha ni magumu. madaktari walipogoma posho imeongezwa kufikia 25,000/=. waalimu wanalalamika hakuna anayejali. Hii imekaaje? na nini kifanyike?. Tafadhali changieni bila ghadhabu. Nawasilisha.

source: gazeti la mwananchi jumatano 29/02/2012 page 3

Hapo rangi ilipo ina maana mapato yao yanabadilika kutegemeana na mwezi...duuu...Acha tuone
 
Back
Top Bottom