Mapato ya Bandari kushuka, wengi sasa kupitia Mombasa

Nchi za Rwanda, Kenya, na Uganda lazima kuipongeza serikali ya magufuli kwani vita walioanzisha dhidi ya serikali ya Tanzania wanaelekea kushinda. Lengo la hizi nchi tatu ni kuimarisha bandari ya mombasa na hivyo kuikandamiza Tanzania kiuchumi. Kwa kutangazwa wazi kwamba bandari ya Dar ina uozo, wafanyabiashara wakubwa waliokuwa wanatumia wamepata taarifa hizo. Kusafisha uozo huo na kuweka mfumo utakaowawezesha wafanyabiashara kupita mali zao itachukua muda kutokana na nchi kukosa teknolojia ya kutosha na wataalamu wa uhakika. Kiuhalisia wafanyabiashara hao wataikimbia bandari yetu.
 
mfumuko wa bei ni mshtuko tu wa kiuchumi....tupeane muda...mambo yataaa vizuri...sukari itashuka hadi buku kwa kilo
nasikia baada ya kale ka command ka kupiga marufuku uingizaji wa sukari, mzigo umepanda tena ?!
naamini mwangaza huanza kuonekana asubuhi na si jioni.
 
Wahenga walisema kila jambo jema halikosi kasoro, baada ya mheshimiwa Rais na Serikali yake kutumbua majipu akianzia bandari, sasa maisha ni magumu kwa wafanya biashara, wafanyakazi wa bandari na TRA wanachelewesha mizigo kisa ukaguzi mzigo kwa mzigo, kifurushi kwa kifurushi hasa kwenye lose cargo. Biashara yetu imekwama bandari kwa miezi miwili sasa, meli ilifika tangu kati kati ya December 2015, lakini mpaka leo February hakuna hata Dalili, hata kulipa haiwezekani japo document zipo sawa.

Mimi kama mfanya biashara nafikiri kurudi kupitisha mizigo yangu bandari ya Mombasa, kwa sababu miezi miwili mzigo uko bandarilini, jumlisha mwezi mmoja wa kuusafirisha kutoka HONG KONG. Nani anaweza kufanya biashara miezi 4 unasubiri mzigo?

Ina maana kwa mwaka mfanya biashara asafiri mara 4 tu, kwa sababu ukilete mzigo kuutoa ni kuanzia miezi 2-4. Nchi itapoteza mapato makubwa muda si mrefu kwa either wafanyabiashara wengi kupitisha mizigo Mombasa au kwa mkufanya mizunguko midogo ya biashara.

Kwa sasa kila mfanyabiashara anatakiwa kuweka detail za mzigo, mfano km ni nguo uandike rangi, jina la muuzaji, na mambo mengine mengi, hivyo bandarini kila kipande kinakaguliwa km ni sawa na document, hivyo kuchelewesha mzigo kutoka.

USHAURI:
Serikali isimamie vizuri bandari ili kupunguza ukiritimba kwa sababu itapoteza wateja wengi, kama mteja amekamirisha kila kitu hakuna sababu ya kuzuia mzigo wake, alipe kodi aendelee na biashara ili arudi tena kuchukua mzigo.
mkuu nenda tu huko mombasa, kwa sababu hata mlivyokua mnapitisha hapo hela haikuonekana... sasa we hayo mapato yanayokosekana ni yapi
 
muda wa kenya kupiga pesa.kuinua miundo mbinu yao fasta.ss tunatumbua majipu
 
Sasa kama hii ndiyo sababu ya kuhamishia root za kibiashara bandari ya Mombasa RUKSA tu nenda. Sisi letu moja tu kwa sasa "KODI HALALI NA STAHIKI". Bandari tu inatosha kutulisha "in Gen. Paul Kagame's voice"
 
Hivyo vyeti vya UDSM vilikua vinatoka wapi..Tangu lini vyeti vikapitishwa bandarini?.na kama vinapaswa kulipa kodi kwanini visilipe....watu walizoea kufanyia clearance kariakor ndo mana leo kukaguliwa wanalia lia
Ukisoma sheria ya kodi ndio utaelewa haya maigizo
 
Attachments

  • IMG_20160209_104650.jpg
    IMG_20160209_104650.jpg
    162.9 KB · Views: 46
Wahenga walisema kila jambo jema halikosi kasoro, baada ya mheshimiwa Rais na Serikali yake kutumbua majipu akianzia bandari, sasa maisha ni magumu kwa wafanya biashara, wafanyakazi wa bandari na TRA wanachelewesha mizigo kisa ukaguzi mzigo kwa mzigo, kifurushi kwa kifurushi hasa kwenye lose cargo. Biashara yetu imekwama bandari kwa miezi miwili sasa, meli ilifika tangu kati kati ya December 2015, lakini mpaka leo February hakuna hata Dalili, hata kulipa haiwezekani japo document zipo sawa.

Mimi kama mfanya biashara nafikiri kurudi kupitisha mizigo yangu bandari ya Mombasa, kwa sababu miezi miwili mzigo uko bandarilini, jumlisha mwezi mmoja wa kuusafirisha kutoka HONG KONG. Nani anaweza kufanya biashara miezi 4 unasubiri mzigo?

Ina maana kwa mwaka mfanya biashara asafiri mara 4 tu, kwa sababu ukilete mzigo kuutoa ni kuanzia miezi 2-4. Nchi itapoteza mapato makubwa muda si mrefu kwa either wafanyabiashara wengi kupitisha mizigo Mombasa au kwa mkufanya mizunguko midogo ya biashara.

Kwa sasa kila mfanyabiashara anatakiwa kuweka detail za mzigo, mfano km ni nguo uandike rangi, jina la muuzaji, na mambo mengine mengi, hivyo bandarini kila kipande kinakaguliwa km ni sawa na document, hivyo kuchelewesha mzigo kutoka.

USHAURI:
Serikali isimamie vizuri bandari ili kupunguza ukiritimba kwa sababu itapoteza wateja wengi, kama mteja amekamirisha kila kitu hakuna sababu ya kuzuia mzigo wake, alipe kodi aendelee na biashara ili arudi tena kuchukua mzigo.
Ingekuwa ni enzi za Kikwete ungeweza kumtisha kwa gia kama hii na akatoa amri mizigo ipite bila kukaguliwa. Lakini sasa?
 
Walipe kodi halali hatutaki longolongo ya kukwepa ulipaji wa kodi, hata kama atabaki mmoja anaelipa kodi halali abaki majizi na makwepa kodi yasepe
 
H
Hivyo vyeti vya UDSM vilikua vinatoka wapi..Tangu lini vyeti vikapitishwa bandarini?.na kama vinapaswa kulipa kodi kwanini Havisilipe....watu walizoea kufanyia clearance kariakor ndo mana leo kukaguliwa wanalia lia
Haiwezekani visingizio vya kodi vikoseshe vijana ajira. Ni dunia ipi vyeti vinalipiwa kodi? Serikali ina mambo ya ajabu saana. Wale waliosoma nje nao wanalipa laki hadi laki na zaidi ili wahakikiwe. Hii ni dhulma na uonevu kwa vijana wetu.
 
muda wa kenya kupiga pesa.kuinua miundo mbinu yao fasta.ss tunatumbua majipu
acha wapige tu...kwa muda...watu wanatishia kuny*a moto wakati wanajua mamivu yake...ata huko kenya watu wasizani watapitisha bure kama walivyokua wanapitisha hapa dar...waende watarudi tu..wakishindwa waache biashara
 
H
Haiwezekani visingizio vya kodi vikoseshe vijana ajira. Ni dunia ipi vyeti vinalipiwa kodi? Serikali ina mambo ya ajabu saana. Wale waliosoma nje nao wanalipa laki hadi laki na zaidi ili wahakikiwe. Hii ni dhulma na uonevu kwa vijana wetu.
kila nchi inataratubu zake.....kama kunamatatizo kwenye hilo kunataratibu za kufuata kupeleka malalamiko...but siamini kama hizo kodi zimeanza sasa hivi wakati tunatumbua majipu
 
TRA imekusanya mapato ya December 2015 yalikuwa 1.2 trillions. na ya sasa imekusanya 1.7 trillions. Kwa takwimu hizo ni kweli kwamba mapato yanaongezeka kwa kuwabana wakwepa kodi bandarini. Sasa mtoa mada utatuambia nini hapo!
 
Wahenga walisema kila jambo jema halikosi kasoro, baada ya mheshimiwa Rais na Serikali yake kutumbua majipu akianzia bandari, sasa maisha ni magumu kwa wafanya biashara, wafanyakazi wa bandari na TRA wanachelewesha mizigo kisa ukaguzi mzigo kwa mzigo, kifurushi kwa kifurushi hasa kwenye lose cargo. Biashara yetu imekwama bandari kwa miezi miwili sasa, meli ilifika tangu kati kati ya December 2015, lakini mpaka leo February hakuna hata Dalili, hata kulipa haiwezekani japo document zipo sawa.

Mimi kama mfanya biashara nafikiri kurudi kupitisha mizigo yangu bandari ya Mombasa, kwa sababu miezi miwili mzigo uko bandarilini, jumlisha mwezi mmoja wa kuusafirisha kutoka HONG KONG. Nani anaweza kufanya biashara miezi 4 unasubiri mzigo?

Ina maana kwa mwaka mfanya biashara asafiri mara 4 tu, kwa sababu ukilete mzigo kuutoa ni kuanzia miezi 2-4. Nchi itapoteza mapato makubwa muda si mrefu kwa either wafanyabiashara wengi kupitisha mizigo Mombasa au kwa mkufanya mizunguko midogo ya biashara.

Kwa sasa kila mfanyabiashara anatakiwa kuweka detail za mzigo, mfano km ni nguo uandike rangi, jina la muuzaji, na mambo mengine mengi, hivyo bandarini kila kipande kinakaguliwa km ni sawa na document, hivyo kuchelewesha mzigo kutoka.

USHAURI:
Serikali isimamie vizuri bandari ili kupunguza ukiritimba kwa sababu itapoteza wateja wengi, kama mteja amekamirisha kila kitu hakuna sababu ya kuzuia mzigo wake, alipe kodi aendelee na biashara ili arudi tena kuchukua mzigo.
Wadau, nitapataje kitufe cha STYLE CHOOSER humu JF ili niweze kuondoka kwenye matumizi ya DESKTOP style niende kwenye WAP style? mbona kile kitufe cha kubadili STYLE sikioni tena? anayakiona tafadhali asaidie kunielekeza kilipohamisiwa tafadhali. hii desktop style inanizingua sana.
 
mi kinachoniuma huu mfumuko wa bei..
sijui hayo matrilioni wanayokusanyaga yanamsaidiaje fukara !
au ni takwimu tu za kisiasa ?
kampeni zinaendelea ?
hapa mtaisoma tuu !
Huoni wadogozako/wanao wanasoma bure?
 
Kaka bandari ya Mombasa yenyewe kuna fukuza fukuza na mabadiliko.. Sasa labda uende bandari ya Somalia
 
kila nchi inataratubu zake.....kama kunamatatizo kwenye hilo kunataratibu za kufuata kupeleka malalamiko...but siamini kama hizo kodi zimeanza sasa hivi wakati tunatumbua majipu
Ni uoga katika utendaji. Hivyo vyeti havijawahi na havipaswi kudaiwa kodi. VAT and import duty both of which should be exempt under para 17 of Part B to the 5th Schedule to the EAC, Customs Management Act
 
Naona Kuna watu wana chuki na wafanyabiashara humu, sio kila mfanyabiashara anae import bidhaa ni mkwepa kodi.
Jamaa ana lalamikia ucheleweshwaji wa kutoa mzigo wake bandarini Kwa sababu system ipo slow, hata mimi siungi mkono kusubiria mzigo zaidi ya mwezi ili utoke bandarini wakati Kuna storage charges.
Watu wana mikopo ambayo wanailipia kila mwezi na akikwamishwa kuleta na kuuza mzigo Kwa wakati biashara lazima iyumbe na wafanyakazi pia ajira zao zitakua mashakani.
Serikali ikusanye kodi yake ila I speed up process.
 
Hyo ni East african act..but tuna taratibu zetu sisi wenyewe ndani ya nchi...ofcoz mi sijui ni kwanini wanavitoza kodi...but iwish not them to do that,,,,otherwise labda kama kunawatu wananufaika navyo kimapato katika huo usafirishaji
 
Naona Kuna watu wana chuki na wafanyabiashara humu, sio kila mfanyabiashara anae import bidhaa ni mkwepa kodi.
Jamaa ana lalamikia ucheleweshwaji wa kutoa mzigo wake bandarini Kwa sababu system ipo slow, hata mimi siungi mkono kusubiria mzigo zaidi ya mwezi ili utoke bandarini wakati Kuna storage charges.
Watu wana mikopo ambayo wanailipia kila mwezi na akikwamishwa kuleta na kuuza mzigo Kwa wakati biashara lazima iyumbe na wafanyakazi pia ajira zao zitakua mashakani.
Serikali ikusanye kodi yake ila I speed up process.
subiri watu watumbue majipu kwanza speed na ufanisi vinakuja
 
Back
Top Bottom