shikulaushinye
JF-Expert Member
- Aug 29, 2014
- 828
- 456
Wahenga walisema kila jambo jema halikosi kasoro, baada ya mheshimiwa Rais na Serikali yake kutumbua majipu akianzia bandari, sasa maisha ni magumu kwa wafanya biashara, wafanyakazi wa bandari na TRA wanachelewesha mizigo kisa ukaguzi mzigo kwa mzigo, kifurushi kwa kifurushi hasa kwenye lose cargo. Biashara yetu imekwama bandari kwa miezi miwili sasa, meli ilifika tangu kati kati ya December 2015, lakini mpaka leo February hakuna hata Dalili, hata kulipa haiwezekani japo document zipo sawa.
Mimi kama mfanya biashara nafikiri kurudi kupitisha mizigo yangu bandari ya Mombasa, kwa sababu miezi miwili mzigo uko bandarilini, jumlisha mwezi mmoja wa kuusafirisha kutoka HONG KONG. Nani anaweza kufanya biashara miezi 4 unasubiri mzigo?
Ina maana kwa mwaka mfanya biashara asafiri mara 4 tu, kwa sababu ukilete mzigo kuutoa ni kuanzia miezi 2-4. Nchi itapoteza mapato makubwa muda si mrefu kwa either wafanyabiashara wengi kupitisha mizigo Mombasa au kwa mkufanya mizunguko midogo ya biashara.
Kwa sasa kila mfanyabiashara anatakiwa kuweka detail za mzigo, mfano km ni nguo uandike rangi, jina la muuzaji, na mambo mengine mengi, hivyo bandarini kila kipande kinakaguliwa km ni sawa na document, hivyo kuchelewesha mzigo kutoka.
USHAURI:
Serikali isimamie vizuri bandari ili kupunguza ukiritimba kwa sababu itapoteza wateja wengi, kama mteja amekamirisha kila kitu hakuna sababu ya kuzuia mzigo wake, alipe kodi aendelee na biashara ili arudi tena kuchukua mzigo.