Mapato siri Yanga, Simba, TFF-DILI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapato siri Yanga, Simba, TFF-DILI

Discussion in 'Sports' started by Pdidy, Oct 28, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,095
  Likes Received: 5,562
  Trophy Points: 280
  Mapato siri Yanga, Simba, TFF
  Mahudhurio Yanga, Simba yaficha vurugu


  Mwandishi Wetu


  WAKATI Shirikisho la Soka Tanzania, TFF likisubiriwa leo kutoa taarifa ya mapato ya mechi ya Jumapili kati ya Yanga na Simba, inakadiriwa kuwa Sh242,435,000 zitakuwa zimekusanywa katika mchezo huo wa kwanza kwa watani hao wa jadi ambao ulifanyika kwenye Uwanja Mkuu wa Tanzania.


  Katika mchezo huo ambao Yanga ilikuwa mwenyeji ilishinda bao 1-0, mashabiki lukuki walifurika kiasi cha kuvunja uzio wa uwanja huo wa kisasa baada ya kuelezwa kuwa tiketi za kushuhudia mchezo huo zilikuwa zimemalizika wakati wao walikuwa na dhamira ya kuona mpambano huo.


  Mwananchi iliyokuwa ikivinjari kabla ya kuanza kwa mchezo huo, ilishuhudia mashabiki hao kwa mamia wakivurumisha mawe, kuwatimua askari polisi ili waweze kuingia uwanjani.


  Hapo ndipo mashabiki hao walipopata mwanya huo ambapo baadaye askari wanadai nao kutumia nafasi hiyo kujichumia kiasi cha fedha huku wale waliokuwa kazini wakitumia mabomu ya machozi kuwatawanya.


  Pamoja na kupiga mabomu hayo, askari hao hawakuweza kumudu kasi ya mashabiki ambao waliingia uwanjani kwa nguvu, lakini hata hivyo wengi walisimama nyuma zaidi kutokana na kukosa nafasi kutokana na wingi wa mashabiki waliokuwa wamelipa na kuingia uwanjani.


  Kutokana na hali hiyo inayofanana na mechi kati ya Stars na Msumbiji, Septemba mwaka jana inakisiwa mashabiki 750 waliingia VIP A kwa kiingilio cha Sh20,000 na kupatikana Sh15,000,000, VIP B, watu 1,973 kwa Sh15,000, idadi inayoweza kukusanywa kwa Sh29,595,000.


  Katika eneo la VIP C kutokana na kujaa, idadi ya walioingia inaweza kufikia 2,242 na kupatikana Sh22,420,000. Viti vya rangi ya chungwa 12,326 kwa Sh5,000 kiasi kinachoweza kupatikana ni Sh61,630,000 wakati watu wa majukwaa ya kijani na bluu wanafikia 37,930 kwa Sh3,000 inaweza kukusanywa Sh113,790,000.


  Kutokana na kile kinachoelezwa kuwa kuwepo kwa gharama mbalimbali za uendeshaji, ambazo mara nyingi zimekuwa ni nusu ya mapato, kila klabu zinaweza kupata zaidi ama pungufu ya Sh70milioni ambazo wachezaji wa Yanga watakuwa wakifurahia ahadi ya viongozi wao waliowaahidi mapato yote kutokana na mechi hiyo.


  Mwenyekiti wa Yanga, Iman Madega aliwaambia waandishi wa habari juzi kuwa wamekubaliana kutogusa hata kiasi kidogo cha fedha za mlangoni na watawapa wachezaji. Kwa hali hiyo, wachezaji 30 waliosajiliwa, kila mchezaji anaweza kuondoka na wastani wa Sh2.3milioni.
   
 2. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2008
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwani hamjui uchaguzi wa TFF umebaki miezi tu? sasa hela za kununua wajumbe si zinabidi zitoke kama hapa? kwenye mpira kuna hela si mmeona mwenyekiti wa simba kapigwa hata mawe lakini hataki kuondoka.
   
Loading...