Mapambano yetu ni Madaraka au ni Maendeleo?

Ramark

JF-Expert Member
May 19, 2015
1,890
2,000
Hili ni swali fikirishi linaloniumiza kichwa kwa muda sasa kuhusiana na aina ya siasa ya nyumbani na wanasiasa wake.

Tangu tulipopata uhuru nchi yetu iligeuza siasa badala ya kuchagiza maendeleo likawa jukwaa la kupata vyeo kwa kigezo cha kuwa mwanachama wa TANU au ASP, ukiondoa ASP, TANU ilipata nafasi ya kuunda serikali kwa vyama vingi kutokana na chaguzi ambao ulitanguliwa na harakati nyingi za kuimarisha chama cha TANU kwa kwa uongozi, rasilimali na watu ambao walijitolea kwa uzalendo uliotukuka, hata Nyerere alipopewa uenyekiti wa chama, kina sykess na wenzake hawakumpa kwa kuwa alitaka madaraka au walitaka madaraka ya serikali baada ya kupata uhuru; wao walitaka maendeleo yaani kuhama toka uukoloni na kuwa huru katika maamuzi.

Nyerere alipenda madaraka baada ya kufika UNO na kugundua namna wengine hasa USSR na CHINA walivyoendesha mataifa yao kwa hoja ya kuungana ili kutawala ambako kulipelekea kubadilisha mfumo wa fikra za umma katika nyanja ya maendeleo.


Wakati huo wengi hawakuwa TANU lakini walilazimishwa kukata kadi na usipokuwa na kadi wewe utumishi wa umma ( kwenye chama au serikali au vyama vya ushirika)usahau, hali hiyo ilipelekea watu waanze kuwaza madaraka na si maendeleo na wote waliotaka mabadiliko waliteketezwa au kufungwa na wengine kukimbia, Nyerere na CC ya TANU kisha CCM waliamini huo ndio uzalendo na huwezi kujenga Babeli bila kuelewana lugha akasahau kuwa ujenzi wa nchi ni kazi endelevu tofauti na Mnara wa Babeli, kwani ni maisha ambayo yanabadilika kulingana na uwezo wa watu kufikiri sambamba na siasa ya ulimwengu na uchumi wake unavyobadilika; wote tukajengwa hivyo na baba yangu akawa mtumwa wa chama kwa cheo serikalini, mpaka leo utamuona akienda kupiga kura za maoni huku akilalamika moyoni na huku akinisihi nisije kwenda kinyume na CCM kwa kkigezo cha uzee wa chama(uzee) unajua sifa za uzee) hakika maisha ya utumwa wa Madaraka ni wa kijinga na ndiyo unaowashikamanisha wanaCCM ili wale kwa urahisi maisha yao huku wakikanyaga maisha ya wajukuu wao na baada ya kustaafu kama Msekwa au Benja wanaanza kujuta kwa sauti na moyoni ya heri wangeishi kama Mzee Mwinyi aliyeenda na Dunia bila shinikizo la chama.


Unapoitazama CCM au TANU na ASP usisahau ya NCCR na Mrema waliojikita katika mageuzi MAGEUZI ya uongozi wa nchi na si mabadiliko ya falsafa na muundo wa nchi, wote walioanzisha vyama nyakati hizo na sasa ni madaraka na Maendeleo kwani maendeleo hukaa na wema, wawazi, wanyenyekevu, watiifu, wenye kicho na kuheshimu nguvu ya Umma.

Mrema alipendwa lkn kwa ubinafsi yaani tamaa ya madaraka hakuona maendeleo ( mabadiliko) yaliyopaswa ili atawazwe kuwa Rais, ni ngumu nasema ni ngumu wakati ule kumpa Mrema nchi kwani kwa hakika hasingeiweza au ingemwangusha kupitia impeachment ya wabunge wengi ambao ni CCM( hawakudraw the big picture) kwa kuwa tamaa yao ilikuwa Madaraka hakika waligawana mbao kwa mkono (fedha) za CCM kupitia serikali( usalama wa Taifa). Maisha ya maendeleo si sehemu yao nasi umma hatukuona bali Mwalimu, kwani tulikwenda kwa hisia na harara kama wanawake wanavyopenda na kuziacha akili zikizubaa kwa kigezo cha furaha ya uhuru wa mfumo chama kimoja; mwalimu alisikika kututukana kwa kile kisa cha kusukuma gari la Mrema na ushabiki huo na ambao pia Benja alitutukana tena 2015 Malofa yaani hatuoni wala kusikia bali kuvutwa na hisia za makange ya kitimoto.

CUF nayo ikabebwa na hisia za upemba za kutaka madaraa ambayo yalikuwa yao baada ya mababu zao wa omani kuondoka wao wakatengwa na kujiona kama hawastahili kuongozwa na Waunguja aambao ni waswahili wasioijua dini na wasio na msimamo>>>> wakatufikisha kwenye vifo ambavyo vikapalilia chuki na mizizi ya CUF kwa kutaka madaraka na si maendeleo kwani walishaanza hayo toka 1993 walivyotaka kugomea uchaguzi ili tu wawe sehemu ya ushindi, 2000 haikugeuza tamaa ya Madaraka kwa Benja, Lipumba na maalimu pia Jumbe katika yote wakasahau kuboresha elimu kule Zanzibar, mmfumo wa afya uliobadilka na kuanza kudai fedha, mfumuko wa bei na mengine mengi ambayo waliona ni samba tu Maendeleo yanakuja ukiwa madarakani, na maendeleo yatakuja ukiwa husikii sauti za mabati ukiwa madarakani.

Wabunge tangu TANU bado hawakutaka mabadiliko ya nchi Tazama mabadiliko ya Vyama vya siasa mwaka 1963 na bado bunge 1965 halikumuhoji Nyerere wala wajumbe CC ya tanu kwa nn tunaenda kwenye Interim nawakati uwezo wa kuandika upo katiba yetu ambako kulipelekea Nyerere kuamua akiwa ikulu hiki kitaenda hivi, mimi nitafanya hivi, wabunge wafanye hivi ambako kulipelekea kuwa nchi tusiyoijua toka Ujamhuri mpaka Utanzania 1977; kwani kipindi hicho hakina muundo wa nchi.

Wabunge tena wakaonesha wao wanataka kushiba baada ya kukubali katiba ya CCM iwe katiba Ya Tanzania iliyoletwa na Msekwa bila maoni wala referundum bado wakaiita katiba ambayohaitambui madaraka ya Rais wa Zanzibar na kama nayo ni sehemu ya serikali kimuundo hivyo kuwalazimisha Zanzibar nao wajiandikie kijikatiba ili kukidhi matakwa yao ikumbukwe wakati ho zanzibar sheria hawaijui na wasomi wengi hakuna.

Wabunge wakaminya uhuru wa siasa kwa mabadiliko ya katiba kwenye vyama vya siasa, ugombea na tume ya uchaguzi pia viti maalumu ili watu wale na ruzuku ipatikane: pia sheria mbovu licha ya ushauri wa Jaji kipenka na Nyalali bado tuko ukoloni na chama kimoja Polisi na MaRC na DC wananguvu kuliko uhalisia wa kulinda watu.

CHADEMA wakaja vizuri tukawaona wanauchungu na rasilimali zetu kwa namna walivyojipambanua lkn bado katiba yao ikaandikwa malengo yao ni kushika madaraka ya nchi na si kuibadili nchi kwa falsafa ya chama na watu wake wakiwa madarakani au nje ya Madaraka ambapo juhudi hizo zipelekee kuaminika na kuongoza nchi au maeneo mengi, CHADEMA waliaminika na kila mtu hadi na marais wastaafu Benja na Kikwete lkn wakakosea kubeba mzigo ulioleta balaa la kukimbiwa na wanachama kwa kuonekana si mvuto tena( slaa alikuwa anavuta kwa historia, utashi, na uwezo).

Ukipoteza kiongozi kwa lengo la kukusanya ni balaa! Kwani mbinu nzuri ni kukusanya pasipo kutawanya yaani collect when you keep what you have, ili usurvive hapo ulipo ni uncertainty situation lakini wakapuuza. Migogoro ya ndani pia inawashinda kutatua mpaka watawanye ili waokote bora kama kuku badala ya kutambua chama ni universal organi inayomeza kama bata na ngumu kufa lkn inanepa kwa kasi, CHADEMA kwa mbinu ya Migogoro unaiona kama NCCR ya awali wapenda madaraka kuliko maendeleo kwani wanaamini kama wale kuwa maendeleo yanapatikana uliwa hausikii kelele za mabati ukiwa madarakani hivyo maendeleo CHADEMA ni ndoto isiyo na muotaji, tutawamini vipi kuwapa nchi nawakati mnavisasi, wasiowatiifu hata kwa nafsi zenu kwani mtageuza nchi kuwa mahali pa kulipa visasi na kunenepesha matumbo yenu.

CHADEMA wameacha sasa kutetea rasilimali zetu wamegeukia chama chao na mambo yao huku umma ukikosa wa kusemewa na kutetewa katika nyanja zote za nchi( kuna petitions ngapi mahakamani, bungeni na kwa rais katika kubadili sheria au katiba? Kuna hotuba ngapi za kuamsha hitaji la watu kutaka mabadiliko? Kuna miradi mingapi ya kuinua uwezo wa uongozi wa umma, civic edu, na civic reasoning hapa nchini? Nk)

Hapo unagundua CHADEMa nao wapo ili wapate Madaraka kama katiba yao inavyowaongoza na maendeleo ya nchi na watu wake.

Zitto na ACT na wezake bado wakajenga chama kipya ili wasimiss nafasi ya kuwa Madarakani ( chamani na kwa nchi) ili kukidhi takwa lao la ndani katika maisha ya hapa Duniani, licha ya kulalamika kuonewa Zitto hukuwahi kuonesha wewe ni mtiifu kwa CHADEMA na umma kuwa wewe ni wa kuaminika na wa kusafiri nasi safari ndefu licha ya barabara mbovu au gari bovu ukajali tumbo lako na falsafa yako na kutaka kutuaminisha kuwa wewe na sisi tunafikiri sawa kumbe sivyo.
Zitto na maalim seif na wenzake bado wanauendeleza upemba kwa madai ya madaraka hata kuhama vyama ili kuhakikisha dhamira yao inakuwa kubwa kkuliko umma wa watanzania wote.

Wabunge hasa CCM ya leo na baadhi wa upinzani wanaishi maisha ya madaraka ya kumsifu Rais badala ya kumsimamia na kumshauri vizur ili alete mabadiliko ya kweli ktk utendaji wa serikali lkn Bunge nalo limesahau kazi ya kutunga sheria nzuri na kubadili mbovu rejea ya TSSSF nk ambazo hazitoshelezi mahitaji hata kabla ya kutekelezwa, mmekuwa wabariki wa kila hoja ya serikali mtazameni bashe 2016/2017/2018 alivyoichachamalia serikali hata mabadiliko kutokea au lissu ili tuone kwa hakika Bunge linatuwakilisha lkn mnaokana kuchumia tumbo ndiyo maana mnasinzia na kujamba bungeni, mnakesha baa na tototz, matumbo makubwa, mnaishi Dar, ofisi zenu majimboni hazina watu, vikao vya bunge na halmashauri watoro licha ya magari mazuri ya kodi zetu hamuoneshi mnataka mabadiliko ya nchi bali tubaki kule kule kuwa maji, umeme, mmadarasa, zahanati nk ni hisani ya serikali na si michango yenu kwani Bajeti kuu kwenu ni kuipitisha tu: wabunge hawapeleki miswada binafsi, ( muswada 1 WA mbunge wa CCM) kamati za Bunge hazijihangaishi licha ya mamlaka hayo bado wanasubiri kupitisha miswada ya serikali tu.

Kwenu wwanasiasa wa nchi hii Madaraka ndiyo chanzo cha maendeleo au utumishi wa umma kizalendo ndiyo huleta maendeleo?

Tufikiri tuko wapi kati ya kumtumikia Madaraka au maendeleo!
 

Tz mbongo

JF-Expert Member
Mar 12, 2015
8,146
2,000
Ngoja niandae tende zangu hapa nikisubiri watu kuja kutetea vyama vyao na itikadi zao.
 

Ramark

JF-Expert Member
May 19, 2015
1,890
2,000
Ccm mtandaoni ni wapuuzi sana
Hawana lógica hata kidogo, tazama uchangiaji wao unadhihirisha makala hii kwa kuonesha tabía sahihi ya wanaccm kuwa wao bila ccm madarakani watakufa njaa au kupoteza utanzania wao
Wanaccm hasa vijana jitazameni upya hasa mnaandaa niñi kwa wajukuu wako? Unatamani watukanwe na kutweza kwa namna ya viongozi wanavyoongoza na bakshishi ya maendeleo kwa kigezo cha uchaguzi yaani ingekuwa hakuna General electiion amini tusingekuwa hapa tulipo


Ccm shetani wa sasa badilikeni
Wapinzani shetani wajao badilikeni
 

Noti bandia

JF-Expert Member
May 3, 2020
591
1,000
Si ajabu wameolewa na wazungu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mmesahau mlivyokuwa mnawagawia madini bure kwa mikataba ya kishenzi. Unajua vyama vya upinzani sioni km vnatatzo ht viongee nn tatzo lipo kwa wale ambao waliuza mali zetu bure kabisa kwa mkoloni afu sahivi wanajifanya upinzani unatetea wazungu. Hv kweli aliyegawa mali za nchi bure kwa wazungu na mpinzani nan wakulaumiwa. Shukuruni bado watanzania wengi uwelewa mdogo
 

Ramark

JF-Expert Member
May 19, 2015
1,890
2,000
Mmesahau mlivyokuwa mnawagawia madini bure kwa mikataba ya kishenzi. Unajua vyama vya upinzani sioni km vnatatzo ht viongee nn tatzo lipo kwa wale ambao waliuza mali zetu bure kabisa kwa mkoloni afu sahivi wanajifanya upinzani unatetea wazungu. Hv kweli aliyegawa mali za nchi bure kwa wazungu na mpinzani nan wakulaumiwa. Shukuruni bado watanzania wengi uwelewa mdogo
Kuna ushahidi uwepo mabeberu mifukoni kwa watanzania pasipo kupitia ubalozi au wizara na vyombo vya serikali
 

Noti bandia

JF-Expert Member
May 3, 2020
591
1,000
Kuna ushahidi uwepo mabeberu mifukoni kwa watanzania pasipo kupitia ubalozi au wizara na vyombo vya serikali
Aawapi mabeberu mlikula nao keki ikulu kabisa, lamda utawala huu ndio umewaweza kidogo mabeberu lakini too late coz walishatubana na mikataba mingi. Huwa nasikitika sn napoona wananchi tunashindwa ht kujikngeza, hv aliyesaini mikataba ya kijinga kbsa ya rasilimali zetu hasahasa serekali zilizopita ht hatuzipigii kelele tunakuja kupiga kelele kwa wakina Zito, Lisu n.k ambao habari zao n za kufikirika na hawana uwezo wa kuingia mkataba wwte ndani ya hii nchi na mabeberu. Fikiria issue ya gesi ilivyogawiwa bure kwa mabeberu hv hapo wa kulaumiwa ni chama pinzani au tawala. Tusiwe watu wepesi wa kugeuzwa km pamba jmn na hawa watawala.
 

Ramark

JF-Expert Member
May 19, 2015
1,890
2,000
Mmesahau mlivyokuwa mnawagawia madini bure kwa mikataba ya kishenzi. Unajua vyama vya upinzani sioni km vnatatzo ht viongee nn tatzo lipo kwa wale ambao waliuza mali zetu bure kabisa kwa mkoloni afu sahivi wanajifanya upinzani unatetea wazungu. Hv kweli aliyegawa mali za nchi bure kwa wazungu na mpinzani nan wakulaumiwa. Shukuruni bado watanzania wengi uwelewa mdogo
Tunazika corona jumapili
Suala la Corona nalo linaonesha tamaa yetu ni Madaraka kwani tukishasherekea ushindi jumapili tunakwenda sambamba na kzamisha Ustawi wa watu (afya) kwa propaganda aína ya Appeal to bad name; vita>>>ubabe na kuficha taarifa>>sheria ya usalama wa taifa 1971
 

Ramark

JF-Expert Member
May 19, 2015
1,890
2,000
Kuna NCCR ya Mbatia nayo inakuja kwa mfumo huu huu wa vyeo na maslahi huku vipaumbele vya umma vikisahulika
Mbatia grasp what u need and regret what u have failed
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom