Mapambano dhidi ya Mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapambano dhidi ya Mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Aug 23, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,413
  Likes Received: 81,452
  Trophy Points: 280
  Hawa kweli ni vigogo au vibua tu!!? IPPMEDIA ni aibu kwenu kwa kushindwa kuyaweka majina ya wahusika kwenye article hii.

  JK amwaga vigogo sita

  2008-08-23 15:43:59
  Na Mwandishi Wetu, Jijini

  Wale vigogo wanaotuhumiwa kuchota mapesa ya umma kwa manufaa yao, waliodhani Rais Jakaya Kikwete atawakingia kifua, sasa wameula wa chuya kwani JK kawanawa kama hawajui vile.

  Katika kudhihirisha kwamba hivi sasa kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe, imedaiwa kuwa, JK ameapa kutoingilia kwa namna yoyote mamlaka ya kisheria kuchukua mkondo wake, hata kama watuhumiwa ni watu walio karibu naye.

  Taarifa kutoka kwa chanzo cha gazeti hili, zinadai kuwa ni kutokana na msimamo huo ambapo JK ametoa baraka zake ili watuhumiwa wote wa sakata la ufisadi, waburuzwe kortini ili kukabiliana na tuhuma zinazowakabili.

  ``Hali sasa ni ngumu kwa baadhi ya waheshimiwa maana mzee (rais) amesema hatamlinda mtu yeyote, japokuwa baadhi ya watuhumiwa ni watu wanaofahamiana vizuri,`` kimedai chanzo chetu kutoka Serikalini.

  Kwa mujibu wa chanzo hicho, kila kigogo ambaye ushahidi utaonyesha zipo hoja za msingi za kumburuza kortini, JK hataingilia kwa namna yoyote.

  ``Wale watuhumiwa sita aliosema mzee katika hotuba yake juzi kwamba watafikishwa kortini, ni mwanzo tu, wengine watafuata,`` chanzo hicho kimedai.

  Kwa mujibu wa chanzo hicho, Rais Kikwete amefikia uamuzi huo wa kuacha watuhumiwa hata kama ni vigogo waumbuke mahakamani, kwa lengo la kufanikisha vita dhidi ya rushwa na kuiletea heshima Serikali yake.

  ``Unajua siku zilizopita kuna watu walidhani sheria inafanya kazi kwa watu wadogo tu, sasa hilo halipo. Yeyote ambaye kuna ushahidi wa kutosha wa kumburuzwa kortini, atabebwa tu,`` kimeongeza chanzo hicho.

  Akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juzi, Rais Kikwete alisema Taasisi ya Kupambana na Kuzuia rushwa nchini, TAKUKURU inakusudia kufikisha mahakamani kesi sita za rushwa kubwa.

  ``Kesi nyingine sita uchunguzi wake umekamilika... ziko mbioni kufikishwa kortini,`` alisema Rais Kikwete.

  Akizungumzia hatua nyingine za mapambano dhidi ya rushwa ambazo tayari zimeshughulikiwa na Serikali, Rais Kikwete alisema kesi zilizofikishwa kortini zimeongezeka kutoka kesi 50 mwaka 2005 hadi kufikia kesi 156 mwaka huu.

  Akasema TAKUKURU ambayo ndiyo inayosimamia kesi hizo tayari imeshinda kesi 35 kutoka kesi sita tu ilizokuwa imeshinda mwaka 2005.

  Aidha akasema ili kuimarisha vita dhidi ya rushwa, Serikali imeajiri vijana 442 katika Taasisi ya kupambambana na Kuzuia Rushwa, TAKUKURU kwa ajili ya kuwadaka wala rushwa.

  SOURCE: Alasiri
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Alasiri bwana .Yaani hili gazeti ni kwamba halina waandishi ama kuna matatizo gani hapo ?
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hawa waandishi wanajaribu kuzima moto kwa mabomu .
   
 4. w

  wajinga Senior Member

  #4
  Aug 24, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kama mali zimekamatwa hazina majina?????????????? unajua vitu vingine vinachekesha sana.
   
 5. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #5
  Aug 24, 2008
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mlimwona Slaa Jana aliposhusha Nondo kwenye Kipindi cha Tuongee Asubuhi cha Star Tv Jumamosi? aliingia hadi na nakala ya Ripoti ya uchunguzi wa Kasha ya EPA na kuonesha tuhuma za Kampuni ya Kagoda. Lakini mgeni wa pili Chitalilo yeye aliishia kumsifia JK na kumwita Baba akionya kuwa ni Utovu wa Nidhamu kumkosoa baba baada ya kutoa (Kuhutubia) maelekezo kwa wototo wake (Bunge).

  Kwa kauli hii ya Chitalilo - Mbuneg wa Buchosa - sikushangaa kusikia CCM wanaandamana kumpongeza JK kwa hotuba nzuri.

  end
   
 6. e

  eddy JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2008
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,361
  Likes Received: 3,762
  Trophy Points: 280
  yaani slaa na phd yake anafanya mdahalo na chitalilo! kweli ccm wajua kumdhihaki mtu.
   
 7. M

  MiratKad JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2008
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 294
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakika huko CCM kuna viongozi mabwege. Kwa nini anajaribu ku-patronise watu. Serikali inajihusisha na WIZI wa mali za umma, halafu anawaita wanaokosoa ni watovu wa nidhamu?? Na hao watu wa Buchosa, wenye Mbunge kama huyu, wana raha gani?
   
 8. M

  MiratKad JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2008
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 294
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Publicity yeyote anayofanya Dr. Slaa ni muhimu. Hawezi kumlazimisha Mbunge Chitalio asiwe Bwege wa kutupa.
   
 9. Augustoons

  Augustoons JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2008
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 410
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Sidhani kama Slaa ndio yeye anachangua nani ajadiliane naye,ni hao tv programmers ambao wanaandaa programs ndio wa kulaumu.Isitoshe Slaa kufanya mijadala na chitalilo sio kosa kwani unataka kusema mtu mwenye phd hana haki ya kujadiliana na mtu mwenye elimu ya bachelors,kidato cha nne, anu kidato cha sita au hata darasa la saba?kwenye siasa kila kitu kinawezekana.Pia walikuwa wamemweka chitalilo pale huwezi kujua azma yao,labda ilikuwa ni kuendelea kuwaonesha umma who chitalilo is.
   
 10. Augustoons

  Augustoons JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2008
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 410
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli mimi nanona mambo ambayo Rais Kikwete alipaswa kuwafanyia watanzania wakaridhika na utendaji wake na hivyo kuifanya kasi mpya ionekane kwamba ni dhahiri zaidi ya uwa ni dhana tu,yalitolewa kwa ufupi na Mheshimiwa Sitta mara baada ya Rais kumaliza hotuba yake. Yale mambo makuu matatu ambayo sitta alimweleza Rais kama yakichambuliwa na Rais kuyafanyia kazi,bas ndoto zake,za kukomesha ufisadi,kuleta maisha bora nk ingeweza kufikiwa hata kabla ya mwaka 2015

  Sio siri ukitaka kupambana na haya mambo ya ufisadi lazima kutumia multi-approach lakini la muhimu zaidi ni kwa kutumia legal reform,maana ni kwa sheria tu unaweza kukabiliana na mambo mengi, lakini iwapo sheria zilizopo bado zina mianya ya kukumbatia mafisadi hataubwabwaje vipi bado watakuwa na nafasi ya kupeta tu. Mfano halisi ni Rais mwenyewe ambaye amekiri wazi kuwa moja ana madaraka makubwa pili,kuwa vyombo vya dola havina uhuru kamili ndio maana anaweza kuviingilia kwa kusema "kamata Dr.slaa" wakishakamata wanarudi kwake kumuuliza "tumeshamkamata tumfanyeje?" yaani hii inaonesha zaidi hawawezi hata kumuuliza mkuu kwa nini Dr.slaa akamatwe. Kwa mtaji huu ndio maana kila mtuhumiwa wa ufisadi jina linapelekwa kwa Rais ili yeye aamue cha kufanya,hali inayotafsiriwa kuwa vyombo vyetu vya dola kila wakati vinasubiri kuambiwa na Rais nini cha kufanya.Haviwezi kwa vyenyewe kutumia utashi wao,lakini hii haiishii hao tu inakwenda hadi kwenye idara nyingine za utendaji,matokeo yake Rais anaonekana nafanya kazi peke yake,na sote tunajua kidole kimoja hakivunji chawa,je mkuu wa kaya kwa mtindo huu anadhani atafanikiwa?
   
 11. e

  eddy JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2008
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,361
  Likes Received: 3,762
  Trophy Points: 280
  Nadhani jf hamfahamu chitalilo, huyu alitumika kumwondoa mzee shindika kwenye ulingo wa siasa, ni huyuhuyu alitumika kuhakikisha dr.tizeba (mhandisi mipango miji) hakanyagi bungeni. Kumbuka star tv nimali ya diallo, Hivyo kuwepo kwenye mdahalo haikuwa bahati mbaya, dr.slaa hakuwa nasabubu ya kukaa mezamoja na huyu jamaa.
   
Loading...