Maonyesho ya kimataifa ya dar, mazuri na mapungufu yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maonyesho ya kimataifa ya dar, mazuri na mapungufu yake

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by CHASHA FARMING, Jul 1, 2012.

 1. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #1
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  WAKUU LEO NIMEWEZA KUTEMBELEA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA DAR NA NILI CHOMOKA KUTOKA ARUSHA ILI NIJE DAR KUHUDHURIA ANGALA SIKU MOJA,

  Kwa kweli Manonyesho ni Mazuri sana, na yanavutia sana na kama yakitiliwa manani yana weza sana kuwasaidia Watanzania kupiga Hatua za Kibiashara,

  SASA NIANZE NA MAZURI NILIYO YAONA KULE VIWANJA VYA SABASABA

  1. Idadi kubwa sana ya Watu wanaotembelea yale Mainyesho

  2. Makampuni mengi

  3. Makampuni ya Kitanzania kuonyeshaubunifu wa hali ya juu

  4. Ulinzi wa kutosha

  MAPUNGUFU NILIYO YAONA MIMI

  1. Maonyesho kugeuzwa kuwa SOKO AU GURIO, kinacho endelea pale ni mauzo kuliko manunuzi

  2. Makampuni ya Tanzania kuwa machache sana na mengi kurudia rudia bidhaa za miaka miatu iliyo pita- Ukiangalia kwenye Mabadna karibia yote ya Bidhaa za Tanzania utagundua ni zile zile za miaka minne mitatu iliyo pita, it means hatuna Ubunifu tena, ndo tumefikia mwisho wa kubuni

  3. Watanzania wengi wanao hudhuria maonyesho kujikita katika kununua kuliko kupata elimu- Kwa kweli idadi ya Wahudhuriaji wanaenda kununua na si kupata elimu, wengi wako bize kununua Vyombo vya Ndani na kazaila

  4. Makampuni ya Kitanzania na watanzania wanaoshiriki kuonyesha Bidhaa za kitanzania kujikita katika kuuza sana na si kutafuta wabia wakufanya nao Biashara
  - WATANZANIA WAKO BIZE KWENYE KUUZA NA SI KUONGEA NA WATU NA KUWAACHIA CONTACT ILI WAFANYE NAO BIASHARA


  5. Maonyesho kutawaliwa na Bidhaa za kichina zaidi

  HAYA MAONYESHO UNAWEZA ZANIA UKO CHINA MAKE BIDHAA ZA CHINA NI NYINGI SANA KULIKO ZA TANZANIA NA HATA NCHI ZINGINE


  6. Wachina Kuwa makini sana na kilicho waleta Tanzania

  WACHINA WAO WAMEKUKA KUTAFUTA MASOKO NA SI KUUZA NA UKIINGIA KWENYE YALE MABADA YAO HAKUNA KINACHO UZWA ILA WAKO BIZE NA MADAFUTARI YAO KUCHUKUA CONTACT ZA WATU ILI WAFANYE NAO BIASHARA


  7. SWALA LA CUSTOMER CARE- wachina na wahindi wako juu sana katika kuongea na Wahudhuriaji na kujaribu kuwafafanulia bidhaa na huduma wanao toa


  8 Watanzania CUSTOMER CARE YETU NI KAMA KAWAIDA TUKO BIZE KUSOMA MAGAZETI NA KUCHATI NA SIMU- Inasikitisha sana Watanzania badala ya kuja kupambana kwenye maonyesho tumekuja kuuza sura na kusoma magazeti, MIMI NILIINGIA KWENYE BAADHI YA MABANDA LIKIWEMO LA SIDO, sikupata mtu wa kunipa maelezo ya nilicho kuwa na taka kisa eti anaongea na simu huko nje, HEBU FIKILIENI WAKUU


  Kwenye Mabanda ya SERIKALI NDO USISEME, wanakutazama kama umefuata misaada pale wako bize wanapiga story za siasa kwenye maonyesho badala ya kutoa elimu,


  9. Watanzania wengi kujikita kutembelea MABANDA YA BIDHAA ZA KICHINA NA ZA ANASA KAMA MABANDA YA KUUZA FANICHA ZA KICHINA, VYOMBO, MIKUFU NA KAZALIKA, na kuacha MABANDA YENYE KUTOA ELIMU NZURI KAMA YA SIDO, MAGEREZA, VETA, JKT NA KAZALIKA


  10. Bidhaa nyingi za KITANZANIA KUJIRUDIA KWENYE MABANDA MBALI MBALI- Ukichunguza kwa umakini unaweza ingia banda la SIDO ukakuta Bidhaa ambayo utaenda kuikuta hiyo hiyo Banda la WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA NA MABANDA YA ANA MKAPA NA KAZALIKA


  na utaikuta na hiyo hiyo nembo na mwenye kuuza atakomaa yeye ndo anatengeneza,


  HAPA NI KWAMBA WAONYESHAJI WENGI WANANUNUA BIADHAA NA KWENDA KUUZA PALE UWANJANI NA SI KUONYESHA UBUNIFU WAO,


  Maoni Yangu ni haya

  1. Serikari na waandaaji wapige Marufuku kuuza bidhaa mule ndani na watu wajikite katika kutangaza na kutafuta masoko,

  2. Waandaaji wahakikishe wanaoshirika wana Uelewa wa kutosha wa bidhaa wanayo onyesha na si kwenda kuuza badala ya kuonyesha


  3. Watanzania wajitahidi kuja na vitu vipya kila maonyesho na si kurudia vitu ambavyo viko mitaani mida yote, KWA MABANDA YA WATANZANIA UTAGUNDUA VITU KAMA UNGA WA LISHE, SIAGI, SABUNI, VIKOI, SHANGA, NA KAZALIKA VIKO MITAANI KWA WINGI SASA KULE WANAENDA KUONYESHA KITU GANI WAKATI BIDHAA TUNAZITUMIA MITAANI?


  MWISHO KABISA

  TUJITAHIDI SANA KUNUNUA BIDHAA ZA KITANZANIA WAKUU MAKE ZINA VIWANGO HATA KUZIDI ZA WAZUNGU TATIZO NI UBUNIFU NA MITAJI NDO TATIZO

  BIDHAA KAMA ZA

  1. VETA- Wana bidhaa za ubora wa hali ya juu kabisa

  2. JKT

  3. MAGEREZA

  4. SODO

  KAMA SISI TUSIPO NUNUA WATAPATA WAPI PESA ZA KUFANYIA INOVATON ZAIDI?
   
 2. SIMBA mtoto

  SIMBA mtoto JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 208
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Sidhani kama yana sifa za kuitwa maonyesho ya biashara ya kimataifa, kwani washiriki wengi ni wachuuzi wa Kariakoo waliohamishia maduka yao na bidhaa zao sabasaba. Ndiyo maana shirikisho la wenye viwanda nchini Tanzania walisusia kushiriki zaidi ya miaka mitano iliyopita wakitaka maonyesho hayo yawe na hadhi ya kimataifa na siyo katika muundo wa sasa hivi wa umachinga, jambo ambalo BET wameshindwa kabisa kulitekeleza.
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  China wamejipanga kweli kweli kutuonyesha jinsi wanavyolitaka hili soko letu
   
 4. M

  MoneyMaker Member

  #4
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu KOMANDOO, kwani ubunifu wa hali ya juu ulioonyeshwa hapo kwenye namba 3 ni ubunifu wa nini?
  Am just questioning myself!
   
 5. M

  MoneyMaker Member

  #5
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli Mkuu. iwe wana bidhaa feki au laa! kifupi, ni China hiyo hiyo inayouza bidhaa ulaya na marekani. Hawa jamaa kwa kweli wanajua wanachokifanya.
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  Mkuu wachina wanatisha, wakati USA yuko bise na Propaganda za Vita wao wanapiga kazi tu, na hawadharau kitu, Maonyesho kama haya huwezi pata kampuni za kimarekani make zenyewe zinahudhuria ya kule south Africa tu, Ila wachina hata yakifanyika SOMALIA wao wataenda tu,

  Na jamaa wako siriasi sana na wako bise sana, INGAWA KWA SASA USA ANAJARIBU KUFANYA KILA MBINU KUMMALIZA MCHINA LAKINI ANASHINDWA, Na jitihada za hivi karibuni ni za USA kuitumia INDIA na kama mnavyo jua INDIA na CHINA haziivi freshi, na USA naitumia India ili kubalance nguvu huko ASIA, na anamtumia pia TAIWAN NA SASA PHILIPINE,

  Ila Mchina kwa sasa yeye anatafuta sana URAFIKI NA MRUSI NA WANA MPANGO WA KUUNDA UMOJA WAO WA KUJIHAMI KAMA WA NATO, Umoja ambao unaweza kuwa JIBU SAHIHI KWA USA NA WASHIRIKA WAKE
   
 7. afrique

  afrique JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 495
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  wadau mmenipa shule sana hapo,sikuyajua hayo yote b4,shukrani
   
 8. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2012
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Yes, the Chinese are coming. Uzuri wa Wachina wakija nchini kwenu kuchukua resources zenu wanawaachia na maendeleo pia si kama hao jamaa wa west wao kazi yao ni kutufanya tuendelee kuwa maskini tu. Na mbaya zaidi wakiona unawawekea ngumu kukuibia wanawatumia waafrika wenzenu kuwashambulia kivita au kufadhili kikundi cha waasi kuleta machafuko mpigane huku wakiwaibia rasilimali zenu. Chukulia mfano wa Kongo, wamarekani wanawatumia Rwanda na Uganda kuwashambulia waafrika wenzao na kuwaibia madini yao, too sad!
   
 9. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  KOMANDOO umemaliza kila kitu, nilishawahi kujiuliza hayo maswali lkn sikupata majibu. Nane nane yale ndio maonesho yanayoleta maana halisi, huwa nawakubali sana SUA, SIDO c'se ukienda banda lao ni lazima utoke na kitu.

  Hawa wenzetu wa TBL wanafuata kuuza bia zile zile kwa bei rahisi, makampuni ya simu kila mwaka wanakwenda kuuza blackberry na kuunganisha watu na line mpya, maliasili na utalii wanakwenda kuwachosha wanyama tu na isitoshe kila mwaka wanyama ni walewale..[nashauri wapeleke vepeperushi badala ya kubeba mnyama]. Kuna watu wana maduka ya vipodozi mjini lakini nao wamo kwenye msafara

  MWISHO naunga kabisa naunga mkono hoja kwa govt kuregulate maonesho.. na si kuigeuza 77 kuwa promotion center.. washiriki watume maombi then wafanyiwe rehearsal kama wanaqualify or not. Pia kuwe na limit ya kuuza/kununua quantity ya bidhaa [mtu mmoja kununua na kujaza lorry kutoka banda moja]
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nilishiriki mara moja tu na sikurudi tena. It was a waste of money and energy. Sijui Board inayohusika na na haya maonesho wanajua maana ya 'Trade Fair'. Si ajabu utakuta wanasafiri sana nje ya nchi lakini bado hajajifunza chochote. Haya maeonesho yangetakiwa yawe ndio chachu ya kuinua vipaji, ubunifu na pia kupanua masoko. Lakini imekuwa no mahali pa kuuza chip kuku, mabatiki kila mahali, maplastic tena. Kwa kifupi hakuna tofauti na masoko yetu ya kila siku kama kariakoo, mazenze etc.

  Nakumbuka mwaka nilioshiriki, kibanda cha jirani kilichukuliwa na kampuni toka Yemen, wamefika wakakuta hali ni tofauti kabisa na walivyozoea, hakuna umeme (ilibidi watafute fundi), kuchafu, space ndogo, walikaa kwa masaa machache na kwa hasira wakaondoka.

  Halafu kuna mgawanyo/arrangement mbaya sana. Utakuta kibanda cha sekta fulani kiko kwenye mchanginyiko wa sekta nyingine kabisa. Hakuna specialization kabisa.

  Bado tuna kazi.
   
 11. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kweli nimepata somo
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  nilienda kwa wachina nikakuta wana mashine za ajabu wanauza
  but wabongo wako bize kununua ma dera na jeans

  kingine ni lugha i guess
  wabongo lugha tatizo
   
 13. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #13
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni Kweli Yale Maonyesho hatuwezi kuyazarau kwa 100% na i hope ukienda pale huwezi kosa GOOD business Aidea pamoja na maonyesho kutawaliwa na Mananuzi kwa wingi,

  Ni kweli mashirika kama SIDO, VETA, MAGEREZA NA JKT wana fanya vizuri sana na sijui tatizo linakuja wapi, ILA NILIJARIBU KUWASHAURI MAGEREZA NA WAO WAWE NA SHOW ROOM YAO DAR NA NINA UHAKIKA WANAWEZA FUNIKA KAMPUNI ZOTE ZINAZO INGIZA FANICHA KUTOKA NJE YA NCHI,

  Tatizo Wamekuwa Maenyesho yakiisha na wao wanafunga kazi kusubiri tena maoenyesho mengine, the same kwa SIDO NA VETA,

  Na hawa Tan trade zamani BET wako kimapato zaidi ndo maana hushangai kuona makampuni ya SIMU HASA VODACOM NA AIRTEL WAKO KILA KONA NA WANA MABANDA MENGI KULIKO KAMPUNI YOYOTE ILE NA AKIJA MGENI ANAWEZA ZANI NI MAONYESHO YA KAMPUNI ZA SIMU NA KIBAYA WAMEJIKITA KWENYE KUUZA NA KUUNGANISHA
   
 14. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #14
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  No mkuu Tatizo si ruga kwani hata wachina nao wanaongea kingereza cha kuunga uunga, Tatizo Liko kwa WABONGO, Yale mabanda yenye vitu vya muhimu huwezi kuta watu, ila kule wanako uza MABESENI, FANICHA, VIKOMBE NA KAZALIKA HUKO WAKO WA KUMWAGA

  Maonyesho yanapoteza maana, na si mahali pa kutafuta wabia wa biashara tena bali ni mahali pa kwenda kununua, Cheki mabanda ya Watanzania wako bise sana na kuweka lebo za bei na hakuna hata mwenye BUSINESS CARD NA WAKO BISE KWENYE KUUZA,
   
 15. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #15
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  Mkuu nazani Waandaaji huwa wanahongwa na haya makampuni ya BIA NA SIMU, haiwezekani watawale maonyesho kihivyo, Na sijajua huwa wanatumia vigezo gani kuwapata washiriki,

  Mimi nazani Sheria ingekuwa kwamba ni lazima waonyeshaji wa Ndani ya Nchi waonyeshe Bidhaa zinazo zalishwa Tanzania na si vinginevyo na washiriki wajikite kwenye kutafuta watu wa kufanya nao biashara wakiwemo Supplier, Agent na watu wengineo
   
 16. F

  FJM JF-Expert Member

  #16
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Ukweli kama hawakuangilia upya tena sabasaba, tutaishia kuwa dumping ground. Hakuna ubunifu kabisa toka Tanzania. Kuna vijana wanafanya mambo makubwa sana huku mtaani, nenda pale gerezani (dar) au hata huko mikoani kuna watu wanajitahidi sana, wizara ya viwanda na biashara wangejitahidi kuwapa fursa ya kuonesha mambo wanayofanya. Lakini huu mtindo wa kugeuza sababasa disco na kurudia taifa nyuma.
   
 17. Kibwebwe

  Kibwebwe JF-Expert Member

  #17
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 797
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Wakuu wote mliochangia mmnifunza kitu.
   
 18. Masulupwete

  Masulupwete JF-Expert Member

  #18
  Jul 9, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 659
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  customer service ni tatizo kwa ofc nyingi hapa tz. Mimi yalinikuta nilipotembelea pspf,watoa ushauri wa masuala ya uzazi na uuzaji wa mipira ya kondom (nimewasahau jina) na benki inaitwa mkombozi.sense ya kuwa mteja ni mfalme haipo kabisa.mtu unaingia wao wanakuangalia tu kama sanamu!
   
 19. mito

  mito JF-Expert Member

  #19
  Jul 9, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,634
  Likes Received: 2,020
  Trophy Points: 280
  Tena mabanda ya serikali ndo hovyo kabisa, customer care sifuri, aliyewekwa mwenyewe hana uelewa wa kutosha na vilivyomo kwenye banda lake. Utakuta wako bize na simu, kusoma magazeti na kusubiri masaa yaende waingize posho yao. Ukichunguza zaidi utakuta wanawekana kwa kujuana.

  Maonyesho hayo yamegeuzwa kuwa mahala pa kuuzia kwa sababu wafanyabiashara wanatake advantage ya loopholes zinazofumbiwa macho na serikali. Hivi mnajua kwamba bidhaa zote za kwenye maonyesho hayo zinaingizwa bila kulipiwa ushuru kwa kisingizio kwamba wanakuja kuonyesha tu na siyo kuuza! Sasa wao wanatumia hiyo nafasi kuingiza bidhaa lukuki na kuishia kuziuza huku serikali yetu isiyokuwa makini imekaa kimya na kuangalia tu huku ikipoteza mapato
   
 20. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #20
  Jul 10, 2012
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mkuu hili halikwepeki kwani wengi wa waenda 77 ni watu wa kipato kidogo ambao huenda huko kutafuta bidhaa za kutumia majumbani mwao zinazouzwa kwa bei rahisi. Kumbuka pia waandaaji lengo lao kubwa ni kukusanya pesa wazotumia kwa mwaka mzima hivyo hawawezi watu kuuza bidhaa maana watakuwa wamepunguza idadi ya wahudhuriaji. Hiyo ndo Bongo mkuu.
   
Loading...