Maoni yangu kwa wenye mamlaka

Ntiyakama

Member
Sep 19, 2021
32
37
Ili kwajengea vijana na taiga kwa ujumla msingi wa kujitegeme na kujiajiri. Yafuatayo ni maoni yangu kwenu mnaoweza kusema iwe na ikawa.

1. Somo la Stadi za Kazi
; lifanyiwe marejeo na kutengenezewa mtaala mpya na maalumu. Mafunzo yaambatane na vitendo. Kuwe na msisitizo wa somo hili kuanzia ngazi za shule za msingi.

2. Waandaliwe walimu mahususi waliopitia mafunzo maalumu kwa ajili ya kufundisha soma hili (Stadi za Kazi)

3. Vipindi vya masomo ya Stadi za Kazi na Haiba kwa wiki viongezwe na vianzie madarasa ya chini zaidi.

Inasikitisha kuwa vimebakishwa vipindi viwili (2) tu vya Stadi za Kazi kati ya vinne (4) vilivyokuwepo kwa wiki. Mbaya zaidi vipindi hivyo sasa huanzia darasa la tano (5) tofauti na mwanzo ambapo vilianzia darasa la tatu (3).

4. Soma la Tehama lipewe msisitizo lifundishwe kwa vitendo na walimu walioandaliwa vyema. Hii ianzie kwa wanafunzi waliopo shule za misingi ili kuwasaidia ufahamu wa kutumia maendeleo ya sayansi na teknologia kwa manufaa yao.

5. Shule zifundishe mambo yanayotuhusu zaidi na yanayoendana na uhalisia wa mazingira tunayoyaishi. Historia ya kwetu zaidi, jiografia ya mazingira yetu kwanza ipewe kipaumbele.

6. Masomo ya ujasiriamali na kujitegemea yafundishwe kwa wanafunzi wote wa ngazi za vyuo na vyuo vikuu.

7. Vyuo vya ufundi (Veta) sambamba na ujuzi vinavyotoa, viwekeze nguvu nyingi katika kuandaa wavumbuzi, waundaji na si watu wa kufunga tu vilivyotengezwa nje.

8. Katika maktaba zote za vyuo na vyuo vikuu; viwepo vitabu vinavyoeleza na kuelekeza kuhusu; elimu ya fedha, ujasiriamali, kujitegemea, kujitambua, mahusiano na uongozi.

Haya yafanyike kwa wanafunzi wote pasipo kujali taaluma wanayoisomea; wanafunzi washauriwe na kuchochewa kusoma vitabu hivyo.

9. Kama ilivyo kwamba; nilazima kila mwanafunzi afanye utafiti (research) na atoe ripoti ya utafiti wake kwa mamlaka ya Chuo, kama kigezo kimojawapo cha kutunukiwa shahada anayosomea.

Vivyohivyo ufanyike utaratibu ambapo kila mwanafunzi kabla ya kuhitimu Chuo awasilishe wazo lake la kijasiriamali, lililo ambatanishwa na mikakati ya kulitekeleza wazo hilo, sambamba na taarifa muhimu zinazohusu au zinazoweza kuingiliana na wazo hilo kwa namna tofauti tofauti.

Mawazo haya yachakatwe na wahitimu hawa wapewe ushauri, maelekezo, rasilimali wezeshi, pale inapofaa kufanyika hivyo; kwa ajili ya manufaa yao na jamii kwa ujumla.

10. Soma la kilimo lifundishwe katika shule za msingi na sekondari zote nchini kwani kilimo huajiri watu wengi zaidi.

Ahsanteni sana.
 
Back
Top Bottom