Maoni yangu kuhusu waraka wa G55 ya CHADEMA

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,149
Reaction score
48,394
Nimeshangazwa kuwa andiko lenyewe kumbe lilikusudiwa liwe ni kwa ajili ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, lakini limekuwa ni nyaraka kwa umma (Public document)

Kwa mujibu wa andiko lenyewe, ni kwamba kundi la watu 55 liliandika barua hiyo kwenda kwa Katibu baada ya kuingia hofu kwamba maoni yao hayatasikilizwa kwenye kikao kilichokuwa kimeitishwa na Ofisi ya Katibu Mkuu na kutarajiwa kufanyika tarehe 03/04/2025, siku ambayo tamko lao lilitolewa.

Kitu ambacho sikielewi ni kwa nini watu wa G55 waliamini kuwa kwenye kikao kilichokuwa kimeitishwa hawatasikilizwa bali watasikilizwa kwa kuandika barua!?

G55 kama orodha ya waliomo ni ya kweli, wengi wao walikuwa ni viongozi wa makao makuu, hii hofu ya kutokusikilizwa inatokana na nini. Au ni picha gani wanayojaribu kuijenga kwa jamii?

Wenyewe kwenye waraka wao wanasema hofu yao ya kutosikilizwa inatokana na mambo makuu matatu.

1. Kauli ya Mwenyekiti Tundu Lissu aliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara Iringa kuwa "wote wanaoona No reforms No Election haiwezekani, ni wana-CCM na vibaraka wao"

2. Kauli iliyotolewa na mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema kwenye mkutano Arusha kuwa " wote wanaotaka ubunge na udiwani bila reforms waondoke CHADEMA ".

3. Maandiko ya Maria Sarungi yanaonesha kuna lengo la kushughulikia wale wanaopinga harakati za No reforms No Election.

Kwa hivyo hayo mambo matatu ndiyo sababu ya G55 kuandika waraka kwenda kwa Katibu Mkuu badala ya kwenda kuhudhuria kikao walichokuwa wamealikwa.

Hoja zao Kuu ni hizi.

1. Haiwezekani kuzuia uchaguzi.

2. Mchakato wa uchaguzi Mkuu umeshaanza.

Kwenye maelezo yao wanasema kuwa No reforms ilianzia kwenye Retreat ya Kamati Kuu huko Makuweni Kenya January 2020. Kwa maana nyingine kulikuwa na "reforms" bila ya neno "No Election" kuwepo.

G55 wanasema matatizo ya rasirimali na mikakati ndani ya CHADEMA yakirekebishwa na kutafutiwa ufumbuzi uhakika wa kushinda uchaguzi 2025 upo.

Wanasema kuwa chama kisiposhiriki uchaguzi wa mwaka huu 2025, chama kitakumbwa na mambo yafuatayo:

1. Kuondokewa na wanachama waliotaka kuwagombea kwenye uchaguzi 2025

2. Chama kitapoteza mvuto na kudhalilishwa Kwa propaganda za CCM

3. Chama kupoteza ruzuku

4. Wanachama wataona hakuna sababu ya kuchangia chama kama hakitashiriki uchaguzi.

5. Watia nia kuacha kuwekeza kwenye chama.

Pia kwenye waraka husika wamesema kuwa lengo la chama ni kushika dola na ni haki ya wanachama kugombea kwa kufuata Katiba ya CHADEMA hivyo kama CHADEMA isiposhiriki uchaguzi huo itakuwa inakiuka haki hiyo ya wanachama.

Mwisho aliyesaini (John Mrema) anasema kuwa wao wapo 55 ila wanawakilisha zaidi ya watia nia 200 Tanzania nzima.

Nitaichambua barua yenyewe kwa ujumla wake.

Kwanza maudhui ya barua ni kuonesha kuwa No reforms No election hakuwa ni mpango wa chama.

Kwa ivo awali chama kilikuwa kinawaza kuwe na " reforms" bila ya kujali kuwa zisipokuwepo chama kitapata athari gani?

Yaani lengo lilikuwa ni nini hasa walipotaka reforms? Walitaka zipatikane ama zisipatikane?

Wao hiyo January 2020 walipokutana huko Makuweni Kenya, walikubaliana reforms zisipopatikana wakae kimya? Sasa walitaka reforms za nini wakati hata zisipopatikana kumbe hakuna shida?

Lakini hivi hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa CHADEMA kutoshiriki uchaguzi? Kama tuliwahi kuamua kutoshiriki chaguzi kadhaa zilizopita, kwa nini Sasa kina Mrema wanasema itakuwa ni kukiuka haki za wanachama.

Wakati kina Mrema walipokuwa viongozi hawakuwahi kuhimiza wanachadema wasishiriki chaguzi mbali mbali kwa maamuzi ya chama. Wakati huo haki za wanachama zilikuwa hazivunjwi?

CHADEMA hatujawahi kuacha kushiriki chaguzi na vyama vingine vikashiriki. Hivyo vyama vimepata faida gani kwa kushiriki chaguzi hizo na sisi tulipata hasara gani?

Mara ngapi watu wanagombea kupitia CHADEMA na baadae kuhama chama. Leo inakuwaje tuwaze kuwa watu watahama CHADEMA kisa hatushiriki uchaguzi?

Hao kina John Silinde, Joshua Nassari, zitto Kabwe, Nusrat Hanje, mtela Mwampamba, Jesca Kishoa, Peter Msigwa na wengineo waliahama CHADEMA kwa kuwa hatukushiriki uchaguzi?

Nadhani waraka umejaa lugha zilizotarajiwa kutolewa na CCM dhidi ya CHADEMA na siyo mtizamo wa kutolewa na wanachadema.

Waraka mzima umejaa maelezo kuonesha kuwa tunao uwezo wa kuilazimisha CCM kuwa ya kistaarabu lakini haiwezekani kuilazimisha CCM hiyo hiyo kuona umuhimu wa kufanya uchaguzi baada ya kufanya marekebisho ya Sheria mbali mbalimbali za kiuchaguzi.

Mifano imetolewa kwenye waraka kuonesha inawezekana kushinda uchaguzi Kwa Sheria zilizopo lakini hawaelezi uwezo huo ulikuwa wapi wakati uchaguzi mzima unaibwa mwaka 2019, 2020, na 2024.

Nani asiyejua kuwa matendo ya kihuni ya CCM na watendaji wasimamizi wa uchaguzi yanalindwa kimfumo na Sheria za uchaguzi na za nchi zilizopo?

Muda wa kupambana kuzuia uchaguzi nje ya uchaguzi haupo ila kuzuia uchaguzi ndani ya uchaguzi inawezekana. Hapa Hawa jamaa wana mantiki kweli?

Kama kujaribu kuzuia uchaguzi nje ya uchaguzi ni jinai, ni kivipi kuzuia uchaguzi ndani ya uchaguzi isiwe jinai?

Waraka wenyewe unahitaji viraka vingi sana ile uwe na mantiki ya kueleweka
.
 
G55 ni akili kubwa wewe huwezi kuwaelewa
 
Wewe huyu ndiye ninayekufahamu sasa. Kule kwenye jukwaa la sipoti unakuwa tofauti sana. Asante kwa bandicoot Murray kabisa
Kina John mrema wanatumika na system hilo halinq kificho mana hawana wanacho lalamikia
Wanayoyasema na kuyaandika ndo hayo hayo makada wa ccm wanaandika humu. Mfno katiba na tume mbovu ya uchaguzi ndiyo iliyompa fulani ubunge mwaka 2015 na ujinga mw8ngine
 
Kumbe huwa una akili, kule kwenye mpira unakuwaga kama kigaragosi cha mudi....

No reform no election inajiuza haitaji nguvu kubwa kama wanayoitumia wao! Tz ina vyama zaidi ya 10 kwanini wasitafute fursa ya kugombea kwenye vyama vingine!. Kuipinga maamzi ya mikutano halali ya chama ni USALITI.
 
Nimeshangazwa kuwa andiko lenyewe kumbe lilikusudiwa liwe ni kwa ajili ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, lakini limekuwa ni nyaraka kwa umma (Public document)

Kwa mujibu wa andiko lenyewe, ni kwamba kundi la watu 55 liliandika barua hiyo kwenda kwa Katibu baada ya kuingia hofu kwamba maoni yao hayatasikilizwa kwenye kikao kilichokuwa kimeitishwa na Ofisi ya Katibu Mkuu na kutarajiwa kufanyika tarehe 03/04/2025, siku ambayo tamko lao lilitolewa.

Kitu ambacho sikielewi ni kwa nini watu wa G55 waliamini kuwa kwenye kikao kilichokuwa kimeitishwa hawatasikilizwa bali watasikilizwa kwa kuandika barua!?

G55 kama orodha ya waliomo ni ya kweli, wengi wao walikuwa ni viongozi wa makao makuu, hii hofu ya kutokusikilizwa inatokana na nini. Au ni picha gani wanayojaribu kuijenga kwa jamii?

Wenyewe kwenye waraka wao wanasema hofu yao ya kutosikilizwa inatokana na mambo makuu matatu.

1. Kauli ya Mwenyekiti Tundu Lissu aliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara Iringa kuwa "wote wanaoona No reforms No Election haiwezekani, ni wana-CCM na vibaraka wao"

2. Kauli iliyotolewa na mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema kwenye mkutano Arusha kuwa " wote wanaotaka ubunge na udiwani bila reforms waondoke CHADEMA ".

3. Maandiko ya Maria Sarungi yanaonesha kuna lengo la kushughulikia wale wanaopinga harakati za No reforms No Election.

Kwa hivyo hayo mambo matatu ndiyo sababu ya G55 kuandika waraka kwenda kwa Katibu Mkuu badala ya kwenda kuhudhuria kikao walichokuwa wamealikwa.

Hoja zao Kuu ni hizi.

1. Haiwezekani kuzuia uchaguzi.

2. Mchakato wa uchaguzi Mkuu umeshaanza.

Kwenye maelezo yao wanasema kuwa No reforms ilianzia kwenye Retreat ya Kamati Kuu huko Makuweni Kenya January 2020. Kwa maana nyingine kulikuwa na "reforms" bila ya neno "No Election" kuwepo.

G55 wanasema matatizo ya rasirimali na mikakati ndani ya CHADEMA yakirekebishwa na kutafutiwa ufumbuzi uhakika wa kushinda uchaguzi 2025 upo.

Wanasema kuwa chama kisiposhiriki uchaguzi wa mwaka huu 2025, chama kitakumbwa na mambo yafuatayo:

1. Kuondokewa na wanachama waliotaka kuwagombea kwenye uchaguzi 2025

2. Chama kitapoteza mvuto na kudhalilishwa Kwa propaganda za CCM

3. Chama kupoteza ruzuku

4. Wanachama wataona hakuna sababu ya kuchangia chama kama hakitashiriki uchaguzi.

5. Watia nia kuacha kuwekeza kwenye chama.

Pia kwenye waraka husika wamesema kuwa lengo la chama ni kushika dola na ni haki ya wanachama kugombea kwa kufuata Katiba ya CHADEMA hivyo kama CHADEMA isiposhiriki uchaguzi huo itakuwa inakiuka haki hiyo ya wanachama.

Mwisho aliyesaini (John Mrema) anasema kuwa wao wapo 55 ila wanawakilisha zaidi ya watia nia 200 Tanzania nzima.

Nitaichambua barua yenyewe kwa ujumla wake.

Kwanza maudhui ya barua ni kuonesha kuwa No reforms No election hakuwa ni mpango wa chama.

Kwa ivo awali chama kilikuwa kinawaza kuwe na " reforms" bila ya kujali kuwa zisipokuwepo chama kitapata athari gani?

Yaani lengo lilikuwa ni nini hasa walipotaka reforms? Walitaka zipatikane ama zisipatikane?

Wao hiyo January 2020 walipokutana huko Makuweni Kenya, walikubaliana reforms zisipopatikana wakae kimya? Sasa walitaka reforms za nini wakati hata zisipopatikana kumbe hakuna shida?

Lakini hivi hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa CHADEMA kutoshiriki uchaguzi? Kama tuliwahi kuamua kutoshiriki chaguzi kadhaa zilizopita, kwa nini Sasa kina Mrema wanasema itakuwa ni kukiuka haki za wanachama.

Wakati kina Mrema walipokuwa viongozi hawakuwahi kuhimiza wanachadema wasishiriki chaguzi mbali mbali kwa maamuzi ya chama. Wakati huo haki za wanachama zilikuwa hazivunjwi?

CHADEMA hatujawahi kuacha kushiriki chaguzi na vyama vingine vikashiriki. Hivyo vyama vimepata faida gani kwa kushiriki chaguzi hizo na sisi tulipata hasara gani?

Mara ngapi watu wanagombea kupitia CHADEMA na baadae kuhama chama. Leo inakuwaje tuwaze kuwa watu watahama CHADEMA kisa hatushiriki uchaguzi?

Hao kina John Silinde, Joshua Nassari, zitto Kabwe, Nusrat Hanje, mtela Mwampamba, Jesca Kishoa, Peter Msigwa na wengineo waliahama CHADEMA kwa kuwa hatukushiriki uchaguzi?

Nadhani waraka umejaa lugha zilizotarajiwa kutolewa na CCM dhidi ya CHADEMA na siyo mtizamo wa kutolewa na wanachadema.

Waraka mzima umejaa maelezo kuonesha kuwa tunao uwezo wa kuilazimisha CCM kuwa ya kistaarabu lakini haiwezekani kuilazimisha CCM hiyo hiyo kuona umuhimu wa kufanya uchaguzi baada ya kufanya marekebisho ya Sheria mbali mbalimbali za kiuchaguzi.

Mifano imetolewa kwenye waraka kuonesha inawezekana kushinda uchaguzi Kwa Sheria zilizopo lakini hawaelezi uwezo huo ulikuwa wapi wakati uchaguzi mzima unaibwa mwaka 2019, 2020, na 2024.

Nani asiyejua kuwa matendo ya kihuni ya CCM na watendaji wasimamizi wa uchaguzi yanalindwa kimfumo na Sheria za uchaguzi na za nchi zilizopo?

Muda wa kupambana kuzuia uchaguzi nje ya uchaguzi haupo ila kuzuia uchaguzi ndani ya uchaguzi inawezekana. Hapa Hawa jamaa wana mantiki kweli?

Kama kujaribu kuzuia uchaguzi nje ya uchaguzi ni jinai, ni kivipi kuzuia uchaguzi ndani ya uchaguzi isiwe jinai?

Waraka wenyewe unahitaji viraka vingi sana ile uwe na mantiki ya kueleweka
.
Uchaguzi mkuu uliopita Chadema ilishiriki kwa dhati, je, ilivuna nini? Mbona Mbowe akiwa mgombea alipewa za usoni na kiongozi wa uchaguzi wakati wa uchaguzi kuwa hatashinda! Mbona wagombea wote walipokwa kura zao zote! hilo linatofauti gani na kutoshiriki?
 
Binafsi endapo ikitokea ( ingawa haitatokea) serikali ikakubali kurekebisha baadhi ya mambo na CHADEMA wakaridhia kushiriki, basi hawa wote G55 ningewafyekelea mbali ktk mchakato wa kupewa ridhaa kugombea.
 
Uchaguzi mkuu uliopita Chadema ilishiriki kwa dhati, je, ilivuna nini? Mbona Mbowe akiwa mgombea alipewa za usoni na kiongozi wa uchaguzi wakati wa uchaguzi kuwa hatashinda! Mbona wagombea wote walipokwa kura zao zote! hilo linatofauti gani na kutoshiriki?
Yule Askari alimwambia Mbowe wazi wazi kuwa hatoshinda.
 
Ukubwa wa akili zao upo kwenye hoja ipi?
Hao jamaa wa G55 ni wajinga mno, wanasema hawawezi kwenda kwenye kikao cha cdm kwani walihisi hawatatendewa haki, na kwenye kikao cha cdm hakuna mtutu wa bunduki, ila wana ujasiri wa kushiriki kwenye uchaguzi wenye mtutu wa bunduki!
 
Nimeshangazwa kuwa andiko lenyewe kumbe lilikusudiwa liwe ni kwa ajili ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, lakini limekuwa ni nyaraka kwa umma (Public document)

Kwa mujibu wa andiko lenyewe, ni kwamba kundi la watu 55 liliandika barua hiyo kwenda kwa Katibu baada ya kuingia hofu kwamba maoni yao hayatasikilizwa kwenye kikao kilichokuwa kimeitishwa na Ofisi ya Katibu Mkuu na kutarajiwa kufanyika tarehe 03/04/2025, siku ambayo tamko lao lilitolewa.

Kitu ambacho sikielewi ni kwa nini watu wa G55 waliamini kuwa kwenye kikao kilichokuwa kimeitishwa hawatasikilizwa bali watasikilizwa kwa kuandika barua!?

G55 kama orodha ya waliomo ni ya kweli, wengi wao walikuwa ni viongozi wa makao makuu, hii hofu ya kutokusikilizwa inatokana na nini. Au ni picha gani wanayojaribu kuijenga kwa jamii?

Wenyewe kwenye waraka wao wanasema hofu yao ya kutosikilizwa inatokana na mambo makuu matatu.

1. Kauli ya Mwenyekiti Tundu Lissu aliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara Iringa kuwa "wote wanaoona No reforms No Election haiwezekani, ni wana-CCM na vibaraka wao"

2. Kauli iliyotolewa na mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema kwenye mkutano Arusha kuwa " wote wanaotaka ubunge na udiwani bila reforms waondoke CHADEMA ".

3. Maandiko ya Maria Sarungi yanaonesha kuna lengo la kushughulikia wale wanaopinga harakati za No reforms No Election.

Kwa hivyo hayo mambo matatu ndiyo sababu ya G55 kuandika waraka kwenda kwa Katibu Mkuu badala ya kwenda kuhudhuria kikao walichokuwa wamealikwa.

Hoja zao Kuu ni hizi.

1. Haiwezekani kuzuia uchaguzi.

2. Mchakato wa uchaguzi Mkuu umeshaanza.

Kwenye maelezo yao wanasema kuwa No reforms ilianzia kwenye Retreat ya Kamati Kuu huko Makuweni Kenya January 2020. Kwa maana nyingine kulikuwa na "reforms" bila ya neno "No Election" kuwepo.

G55 wanasema matatizo ya rasirimali na mikakati ndani ya CHADEMA yakirekebishwa na kutafutiwa ufumbuzi uhakika wa kushinda uchaguzi 2025 upo.

Wanasema kuwa chama kisiposhiriki uchaguzi wa mwaka huu 2025, chama kitakumbwa na mambo yafuatayo:

1. Kuondokewa na wanachama waliotaka kuwagombea kwenye uchaguzi 2025

2. Chama kitapoteza mvuto na kudhalilishwa Kwa propaganda za CCM

3. Chama kupoteza ruzuku

4. Wanachama wataona hakuna sababu ya kuchangia chama kama hakitashiriki uchaguzi.

5. Watia nia kuacha kuwekeza kwenye chama.

Pia kwenye waraka husika wamesema kuwa lengo la chama ni kushika dola na ni haki ya wanachama kugombea kwa kufuata Katiba ya CHADEMA hivyo kama CHADEMA isiposhiriki uchaguzi huo itakuwa inakiuka haki hiyo ya wanachama.

Mwisho aliyesaini (John Mrema) anasema kuwa wao wapo 55 ila wanawakilisha zaidi ya watia nia 200 Tanzania nzima.

Nitaichambua barua yenyewe kwa ujumla wake.

Kwanza maudhui ya barua ni kuonesha kuwa No reforms No election hakuwa ni mpango wa chama.

Kwa ivo awali chama kilikuwa kinawaza kuwe na " reforms" bila ya kujali kuwa zisipokuwepo chama kitapata athari gani?

Yaani lengo lilikuwa ni nini hasa walipotaka reforms? Walitaka zipatikane ama zisipatikane?

Wao hiyo January 2020 walipokutana huko Makuweni Kenya, walikubaliana reforms zisipopatikana wakae kimya? Sasa walitaka reforms za nini wakati hata zisipopatikana kumbe hakuna shida?

Lakini hivi hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa CHADEMA kutoshiriki uchaguzi? Kama tuliwahi kuamua kutoshiriki chaguzi kadhaa zilizopita, kwa nini Sasa kina Mrema wanasema itakuwa ni kukiuka haki za wanachama.

Wakati kina Mrema walipokuwa viongozi hawakuwahi kuhimiza wanachadema wasishiriki chaguzi mbali mbali kwa maamuzi ya chama. Wakati huo haki za wanachama zilikuwa hazivunjwi?

CHADEMA hatujawahi kuacha kushiriki chaguzi na vyama vingine vikashiriki. Hivyo vyama vimepata faida gani kwa kushiriki chaguzi hizo na sisi tulipata hasara gani?

Mara ngapi watu wanagombea kupitia CHADEMA na baadae kuhama chama. Leo inakuwaje tuwaze kuwa watu watahama CHADEMA kisa hatushiriki uchaguzi?

Hao kina John Silinde, Joshua Nassari, zitto Kabwe, Nusrat Hanje, mtela Mwampamba, Jesca Kishoa, Peter Msigwa na wengineo waliahama CHADEMA kwa kuwa hatukushiriki uchaguzi?

Nadhani waraka umejaa lugha zilizotarajiwa kutolewa na CCM dhidi ya CHADEMA na siyo mtizamo wa kutolewa na wanachadema.

Waraka mzima umejaa maelezo kuonesha kuwa tunao uwezo wa kuilazimisha CCM kuwa ya kistaarabu lakini haiwezekani kuilazimisha CCM hiyo hiyo kuona umuhimu wa kufanya uchaguzi baada ya kufanya marekebisho ya Sheria mbali mbalimbali za kiuchaguzi.

Mifano imetolewa kwenye waraka kuonesha inawezekana kushinda uchaguzi Kwa Sheria zilizopo lakini hawaelezi uwezo huo ulikuwa wapi wakati uchaguzi mzima unaibwa mwaka 2019, 2020, na 2024.

Nani asiyejua kuwa matendo ya kihuni ya CCM na watendaji wasimamizi wa uchaguzi yanalindwa kimfumo na Sheria za uchaguzi na za nchi zilizopo?

Muda wa kupambana kuzuia uchaguzi nje ya uchaguzi haupo ila kuzuia uchaguzi ndani ya uchaguzi inawezekana. Hapa Hawa jamaa wana mantiki kweli?

Kama kujaribu kuzuia uchaguzi nje ya uchaguzi ni jinai, ni kivipi kuzuia uchaguzi ndani ya uchaguzi isiwe jinai?

Waraka wenyewe unahitaji viraka vingi sana ile uwe na mantiki ya kueleweka
.
Kitu mnachotakiwa kujiuliza ni kwa nini CCM wanawaachia mfanye mikutano yenu bila bughudha yeyote? Wanaona jinsi kila siku inavyoenda mnavyojichimbia kaburi.
1. Mnawashughulikia wanachama wanaotofautiana nanyi.
2. Mnasema mtafanya uasi kama hayatakuwepo mabadiliko.
3. Mnasema mta andamana kuzuia ambayo mtawazuia wale ambao wanataka kupiga kura wasifanye hivyo.
Yote hayo ni wimbo kwa CCM maana wakorofi mtaonekana nyie.
Mnacheza checkers wakati wao wanacheza cheese. Mimi ndio maana siku zote CCM walikuwa wanataka Lissu ashinde maana sio mtu wa strategy kama Mbowe. Mbowe pia ameonyesha kuwa haogopi kitu. Ni kiongozi pekee wa CDM ameongoza binafsi maandamano yaliyozuiwa dhidi ya serikali. CDM imepigwa kwenye hili.
Siku zote kukitoa chama tawala kilichohusika katika kutafuta uhuru sio kazi nyepesi. PRI ya Mexico ilishika usukani kwa miaka 42 kabla hakijatolewa. Congress ilitamba kwa miaka 50. ANC ndio kwanza inatingishwa. Nyinyi mnakata tamaa baada ya miaka 30 tu!

Amandla...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom