James Hadley Chase
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 1,578
- 2,664
JANA nilipokuwa UTV (Azam TV), nikifanya mahojiano kipindi cha Morning Trumpet, niliulizwa maoni yangu kuhusu mabadiliko ambayo Rais Samia aliyafanya juzi (Mei 3), Ikulu na Idara ya Usalama wa Taifa (Tiss).
Nilijibu kuwa sikuona msingi wowote wa kumwondoa Diwani Athuman Tiss, alipokuwa Mkurugenzi Mkuu na kumhamisha kuwa Katibu Mkuu Ikulu.
Kama alikuwa tatizo Tiss, maana yake watu wangetafsiri yale matatizo yake yangehamia Ikulu. Tiss na Ikulu ni taasisi zinazofanya kazi kwa upacha.
Mwisho nilisema sikuona mabadiliko bali chekecheo. Wa huku anawekwa pale. Nikasema Rais Samia mwenyewe ndiye anajua msingi wa uamuzi wake. Sisi wa nje hatujui.
AMBACHO SIKUKISEMA
Diwani amekuwa Boss wa Tiss nyakati ambazo Tanzania ilikuwa gizani totoro.
Utekaji na upoteaji watu.
Dola ilikithiri ubabe na ukandamizaji.
Miili ya watu iliokotwa baharini.
Watu waliporwa fedha zao halali benki.
Wafanyabiashara waliporwa viwanda vyao.
Wafanyabiashara walifilisiwa.
Uchaguzi Mkuu 2020 ulivurugwa.
Kisisahaulike Kikosi Kazi kilichoundwa kukusanya madeni ya kodi. Kiliwabambikia kesi za uhujumu uchumi wafanyabiashara. Fedha zikalipwa akaunti za watu binafsi.
Kuna mzaha wa Covid-19. Maradhi yakaletwa siasa. Watanzania wengi wakapoteza maisha.
Ongeza na mengine mengi ikiwemo wabunge na madiwani wa upinzani kununuliwa kwa fedha nyingi, kisha uchaguzi kurudiwa. Rushwa na ufujaji mkubwa wa fedha uliofanyika kwa lengo la kumfurahisha mtu mmoja.
Mambo yote hayo yalitendeka Idara ya Usalama wa Taifa ilikuwa chini ya Diwani.
Kipindi ambacho nchi iliihitaji Tiss imara na yenye uthubutu mkubwa, Diwani hakuifanya idhihirishe uwepo wake kwa ajili ya usalama kamili wa taifa. Tiss haipaswi kuwa idara yenye kuchezewa na wanasiasa. Tiss ni moyo wa nchi.
Kwa muktadha huo, sikuona sahihi kumpeleka Diwani Ikulu. Alipaswa kuwekwa kando.
Leo, uteuzi wa Diwani Ikulu umetenguliwa kabla hajaapishwa. Binafsi nimeona ni sahihi kabisa.
Iwe aligomea uteuzi wa kuwa Katibu Mkuu Ikulu kutoka DG Tiss au Rais Samia amebadili uamuzi baada ya tafakuri (afterthought), vema Diwani akae pembeni.
Nchi inahitaji hewa safi.
Tiss inahitaji usafi mkubwa.
Mungu Ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Credit: Luqman MALOTO