Maoni yangu kuhusu sakata la uchaguzi wa TFF

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Mimi Binafsi nadhani huyu Hawa Mniga alikuwa mgombea wa Urais wa (TFF) avhunguzwe, Kwa nini achunguzwe.

Unaweza kusema huyu dada ndiye aliyezuia baadhi ya wagombea, kufanya wakose sifa ya kugombea kwa mujibu wa kanuni zilizotungwa na (TFF).

Rais Karia na huyu dada ndio waliopata udhamini (Endorsement) kubwa zaidi kuliko wagombea wengine. Karia alipata zaidi ya wajumbe 16+ na huyu dada akapata wajumbe zaidi ya 6+

Idadi ya wajumbe wanaotoa udhamini kwa wagombea una kikomo, hivyo kupelekea wagombea wengine kukosa udhamini wakiwemo Ally Mayai na yule wa Efm.

Hilo sio tatizo Ila Tatizo lilikuja baada ya wagombea kubaki (3) yaani

Karia
Hawa Mniga na
Mgeusa.

Baada ya wao pia kuenguliwa na kumbakiza mgombea (1) Karia, huyu dada alihojiwa akasema anakubali kuenguliwa kwa sababu ni kweli hakuwa na vigezo. Tujiulize kuhusu hata maswali

1). Alijua hana vigezo kwa nini aligombea?

2). Alipataje udhamini haraka haraka huku wagombea wengine tena wenye majina makubwa wakikosa?

3). Kuna uhusiano gani kati ya mgombea pekee aliyesalia na huyu dada?

4). Hakukuwa na makusudi ya kumuweka huyu dada ili wagombea wengine wenye Sifa zaidi yake wakose endorsement?

Hayo maswali majibu yake ndiyo uchunguzi unapotakiwa kuanzia.
 
Best laid plans!

Kama Karia alielekezwa afanye uhuru huo na wenye nguvu basi imeisha hiyo!! Karia atavuka hicho kiunzi!
 
Inawezekana huyo dada ni TISS wakiwa na lengo la kumnasa Karia. Au ni shushushu wa Karia akiwa na Lengo la kumvusha Karia.
 
Karia kajimaliza mwenyewe hana wa kumlaumu. Picha lake kacheza kishamba sana. Ali Mayai ndio mgombea pekee aliyejkuwa na nguvu ya kupambana na Karia na ndiye pekee aliyekuwa na uwezo wa kuongoza TFF. Yeye angepambana kumuengua Ali Mayai ningemuelewa (japo sikubaliani na hilo suala). Sasa yeye kaenda kuenguwa wagombea wote akaacha mamluki wake wawili ndio shida ilipoanzia hapo.

Hongera sanaAli Saleh kwa kwenda mahakakamani ili kupata tafsiri ya kisheria. N i uamuzi wa maana sana kuliko kuishia kupiga kelele mitandaoni na kwenye vyombo vya habari.
 
Naamini haki itatendeka! Haiwezekani mhamiaji haramu mmoja tu atuamulie watanzania milioni 60 mustabari wa soka letu kwa kutumia tu ujanja ujanja!

Yaani wenye mpira wao kama akina Ali Mayay eti wanapigwa zengwe na wapita njia tu! Too shame!!
 
Back
Top Bottom