Maoni ya waTZ kuhusu katiba angalia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni ya waTZ kuhusu katiba angalia

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by TIQO, Nov 15, 2011.

 1. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  #48 Moyo 2011-11-15 09:42 "alikiri kwamba aliwazuia wajumbe wa kamati hiyo siyo tu kwenda mikoani kukusanya maoni ya wananchi, lakini hata wale waliotaka kwenda nje ya nchi kwa lengo la kujifunza.
  “Katiba ni ya kwetu wenyewe, mnakweda nje kufanya nini?”alihoji Spika."...Mheshimiwa Spika kama alisema hivyo basi atakuwa anatufananisha wananchi na watu wa nchi za nje ambao katiba haiwahusu kabisa. Ni vizuri utafafanuzi kwa nini wananchi awahusishwi bila kuwaweka kapu moja na watu wa nje.
  Quote

  0 #47 Glory Ombeni 2011-11-15 09:41 Wantanzania tunashuhudia waziwazi Spika akikasirika sana wakati wapinzani wakitaka mwongozo kitu ambacho sio sawa kwa sababu jamani nchi yetu inatawaliwa kidemokrasia kama CCM ilijua haitataka kushirikiana na wapinzani katika kutekeleza majukumu yote ni vyema sasa warudi kwenye mfumo wa chama kimoja (Monopaty) kuliko kutudanganya tuko kwenye mfumo wa vyama vingi (Multpaty) wakati kwa macho yetu watanzania tunaona na kuelewa kinachoendelea. Jamani CCM wajifunze kusoma nyakati na waelewe kabisa kuwa watanzania wa sasa sio wa wakati uleeee!!!
  Quote

  0 #46 Robert 2011-11-15 09:35 Ndugu watanzania wenzangu na wapenda maendeleo binafsi nashindwa kuelewa kwa nini serikali ya ccm inaogopa kuuweka mchakato huu wa uandikwaji wa katiba mpya ktk hali tete namna hii, hapa nadhani wana hofu yakupoteza madaraka kwa sababu wanatambua kabisa kwa siku za leo ccm na serikali yake haitakiwi na wananchi,hivyo ni muhimu kudai kwa nguvu na kwa hoja maridhawa.
  katiba ni ndio uchumi wa nchi, siasa safi,jamii iliyo huru na sawa na pia ni mwongozo sahihi katika kumiliki ardhi kwa mwanachi na rasilimali zake kwa usitawi wa nchi yetu.
  Kwa kuwa mtu akizoea madaraka anasahau kutenda haki bali anajaa kiburi na majivuno ndivyo ilivyo kwa serikali yetu kwa sasa.
  Lakini napenda kuwakumbusha watawala kwamba,madai ya haki ya wananchi ambao ndio msingi wa utawala wa nchi ni muhimu sana kuwasikilza na kuyaweka mbele matakwa yao vinginevyo-dhambi inawaotea mlangoni!!Zambi a walidai katiba mpya kwa muda mrefu watawala hawakuwa tayari,uchaguzi mkuu ulipoitishwa watawala wakabwagwa chini ,siku yakukabidhi madaraka walilia machozi wakijua kabisa kwamba jamaa ataitumia katiba ileile mbovu kuwakandamiza wao, isije kuwa kwetu hapa pia!!!
  Quote

  0 #45 Deogratius Pius 2011-11-15 09:35 Katiba ni ya watanzania na si mali ya mtu yeyote wala kikundi fulani cha watu,sasa inashangaza kuona sisiemu na mwenyekiti wake kuona wao ndio m badala wa mawazo ya watanzania,hali kama hii yaweza kuleta vurugu zisizo za lazima watawala wlielewe hilo....
  Quote

  0 #44 MCHONGANISHI 2011-11-15 09:30 Nadhani hapa haihitajiki amani tena.Spika upendeleo uufanyao utakuponza.Kwanini CHADEMA waonekane wakorofi hata kwenye mambo ya msingi?
  Quote

  0 #43 taylor 2011-11-15 09:28 Kuhusu madai ya kuingilia utendaji wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, alikiri kwamba aliwazuia wajumbe wa kamati hiyo siyo tu kwenda mikoani kukusanya maoni ya wananchi, lakini hata wale waliotaka kwenda nje ya nchi kwa lengo la kujifunza.
  SIELEWI KAULI HII YA SPIKA MAKINDA “Katiba ni ya kwetu wenyewe, mnakweda nje kufanya nini?”alihoji Spika.
  Quote

  -11 #42 Babalao 2011-11-15 09:23 CHADEMA MNATUCHANGANYA HAKIJULIKANI NINI HASA MNATAKA...!!!! INAONEKANA MMEPOTEZA DIRA NA MUELEKEO.ACHENI WOGA KATIBA SIO YA CCM NI YA WATANZANIA WOTE. NINAMASHAKA INAWEZEKANA LENGO MBADALA MLILO NALO NI KUINGIZA NCHI KATIKA MACHAFUKO NA KUSHINDA KUTAWALIKA. DHAMBI HIYO MKIITENDA MUNGU HATAWASAMEHE...!!! WACHENI KUFANYA MAAMUZI YENYE LENGO LA KUPIGIWA MAKOFI NA WATU WACHACHE.
  Quote

  0 #41 magessa 2011-11-15 09:17 Hii ndio serikali sikivu ya CCM wanawasilikiliz a sana wanananchi na wanafanya maamuzi kwendana na maoni ya wananchi,kwahiy o mimi nawapongezeni sana kwa mnayoyafanya ila 2015 sijui mtapitia wapi nadhani mngeanza kununua majumba ulaya kwani bongoland pananweza pakawa hapatoshi kabisa lazima watu waning'inizwe kama SADAM
  God bless Tanzania,God bless the tanzanians
  Quote

  0 #40 Mkosa haki 2011-11-15 09:16 Nchi hii si ya Makinda wala Kombani timizeni matakwa ya wananchi kwanza ndo zifuatwe kanuni za Bunge.Mama Makinda tunakuheshimu sana lakini kwa hili umetukosea wananchi wa Tanzania na nakwambia kama utaendelea hivi dawa yako inachemshwa,Njo mbe sahau ubunge tena hakuna kwa mtu kama wewe.
  Quote

  -6 #39 Ally 2011-11-15 09:15 Tumewazoea nyie wazee wa kukimbia, hatutaki mambo ya Libya sisi wamemtoa Gadafi lakini sasa hivi wanapigana wenyewe kwa wenyewe tunashindwa kuelewa walichokuwa wakikitafuta, na nyie chadema ndo mnakoelekea sasa ( mh spika fuata kanuni za bunge sio kuwaogopa hawa [NENO BAYA]
  Quote

  +1 #38 Kimbatu 2011-11-15 09:12 Kwanini CCM hawataki kujifunza hata kwa Wakenya? Bila ya kuwa na tume huru ya uchaguzi bado tutakuwa tunachezewa shere na Katiba ya Tanu/ CCM . Haiingii akililini Wazanibari ambao hawazidi milioni moja na nusu kuwa na wawakilishi 180 katika bunge la Katiba huku Tanganyika ikiwa na watu milioni 43 na ushee wawe na wajumbe 360 huu AMA ni uhuni wa CCM au ni mbinu chafu ya kuendelea na hii Katiba inayoipa CCM kutawala hapa Tanzania mpaka kiama. Mpaka wafe watu Katiba mpya haipatikani kwa huruma ya CCM Kama anavyoiona mchovu Augustino Mrema. Aluta continua mpaka kieleweke Katiba ndiyo njia tuwakabe bila kuachia.
  Quote

  0 #37 Ngosha 2011-11-15 09:11 This is totally disappointing! Imefikia mahala hata spika wa bunge ambalo ndiyo nguzo pekee ya kutetea na kuwakilisha wananchi sambamba na kutunga sheria anaonyesha upendeleo wa wazi kwa serikali! au yeye ni spika wa selikari na si bunge! Kinachowafanya waogope kuusoma muswada kwa mara ya kwanza nini? na nani amewaambia kwa kufanya hivyo watakuwa wanapoteza muda? nani nini ajenda ya siri? Serikali hii inaonyesha wazi kuwa haipo tayari kusikiliza maoni ya wananchi japo JK huwa anajigamba eti serikali yake ni sikivu! mimi binafsi napinga hili openly.CCM ifikie mahali muone aibu na pia mnapaswa kutambua kuwa mnajichimbia kabuli wenyewe, maana hata majaji wastaafu wamekosoa baadhi ya vifungu ikiwemo ile ya hadidu za rejea kutolewa na rais. Mimi nasema kila kitu kina ALFA NA OMEGA.
  Quote

  0 #36 Mark TUMAINI 2011-11-15 09:07 HATA MCHANGA WA BAHARI HUOTA RUTUBA MUDA UKIFIKA! WAPINZANI WA KWELI][ BIG UP! WARAMBA NYAYO WANG'ANG'ANI WAKATI AMBAO SASA UMEPIGWA KUMBO TAYARI NA TUFANI YA MABADILIKO.KAMA HAO WAREFU HUKO MBELE HAWATAKI KUBADILIKA MABADILIKO YATAWABADILISHA !
  Quote

  +1 #35 Bugota 2011-11-15 09:07 Ombi: Viongozi wa Tanzania kuweni na utamaduni wa Kuwajibika. Angalieni nchi zingine Kiongozi akiona ameshindwa kazi anajiuzulu kiungwana. Mama Anne Makinda sasa tunajua kwamba kazi imekushinda, tunaomba jiuzulu ukae pembeni waachie wengine waongoze unaua Kizazi chetu Mama kuwa na HURUMA JAMANIIIIII.
  Quote

  0 #34 Kazwile Ntinginya 2011-11-15 09:05 Dharau na kibuli ndivyo viliuangusha utawala wa Roma, ndivyo vivyo hivyo vimemwangusha Gadafi, ni wakati sasa CCM na watu wake wakasoma alama za nyakati na wakaheshimu sauti za watu wao. Katiba hii siyo ya CCM na hatutaki mwenyekiti wa CCM ndiye aamue ni nini kiandikwe kwenye katiba.
  Mapendekezo mengi ya Kambi ya Upinzani ni ya msingi na hayastahili kupuuzwa eti kwa sababu yametolewa na Lisu

  Quote


  0 #33 Mark TUMAINI 2011-11-15 09:02 UFALME hadi lini nchi hii? SS ni muda muwafaka wa kuondokana nao!
  keep up wapinzani.Watanzania wanyonge wako nyuma yenu. Hata mchanga wa bahari huota rutuba muda ukifika!
  Quote

  -1 #32 paul sirma 2011-11-15 09:02 Hii nchi yetu jamani tunaipenda kweli? embu jamani tuwemakini haya mambo madogo madogo yatatufikisha pabaya. Tumeona yaliyotokea Libya, na Egypt. Tusipokuwa makini tutaingia kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe hivi karibuni na ni sisi wananchi ndio tutakao athirika. Umefika wakati wa kukubaliana kwenye mambo ya msingi na kuweka kando itikadi zetu
  Quote

  0 #31 mkereketwa 2011-11-15 09:01 Kuhusu madai ya kuingilia utendaji wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, alikiri kwamba aliwazuia wajumbe wa kamati hiyo siyo tu kwenda mikoani kukusanya maoni ya wananchi, lakini hata wale waliotaka kwenda nje ya nchi kwa lengo la kujifunza.
  “Katiba ni ya kwetu wenyewe, mnakweda nje kufanya nini?”alihoji Spika.
  sawa umewasuia wanotoka nje ya nchi kwa nini pia umewasuia kwenda mikoani kwani mikoa hiyo si iko ndani ya tanzania.
  Quote

  0 #30 ikingili 2011-11-15 08:59 huyu makinda ni [NENO BAYA] sana hana akili kabisa. mbona unataka kupelka wanaume unavyotaka wewe? jiheshimu hiyo katiba ni ya kwako? au unampelekea mumeo? acha kazi ifanyike acha upendeleo wa ki[NENO BAYA] kwa hao [NENO BAYA] wenzio ssm. au umetuona sisi wananchi hatuna elimue?cdm big up sana mpaka kieleweke!!!!!! !!!watachukua silaa za moto si tutachukua mawe,na 2kizipata silaha za moto wamekwisha
  Quote

  +1 #29 mark TUMA 2011-11-15 08:59 Si sahihi kudhani chama tawala ndicho chenye fikra sahihi kama ilivyokuwa enzi zake! Hoja za upinzani ni za msingi hasa mamlaka ya Rais! Ni muda muwafaka wa kuwasikiliza!
  Quote

  0 #28 steve 2011-11-15 08:44 Katiba ni ya watu wote na wala sio ya spika na wabunge wa "sisiem" hivyo spika usiwe dictator
  Quote

  +1 #27 oo 2011-11-15 08:42 All this won't solve a thing, but the only soln is gettin' these hypocrites (CCM) outta systeam. Actually whats goin on right now scares me,worse that dyin' broke. I don' blame Hon. Makinda, we all know she has no say at all, just fullfiling what shez ordered by those who kept her there, shez empty upstairs. 2015 gon be the end of all these nonsence.
  Quote

  0 #26 Tumethubutu 2011-11-15 08:31 Hivi, serikali inaona shida gani kutumia busara ya kuahirisha jambo hili ili kutoa muda wa kupata maoni zaidi hata kwa miezi mitatu tu. Lengo ni kuwafanya hata wale wanahoji uhalali wa uharaka wasiwe na kisingizio in future.
  Quote

  0 #25 enedy mrema 2011-11-15 08:28 Vyama vya upinzani kuweni na msimamo huo huo ndiyo, ccm itajua kuwa wananchi wameshawachoka.
  Quote

  0 #24 mtz 2011-11-15 08:12 KWELI TANZANIA HATUNA VIONGOZI FUNZA TUPU KICHWANI...
  SPIKA ALIHONGWA BIL1 NA MAFISADI ILI SITA ASIWE SPIKA... SI SHANGAI KUMTETEA KJ NA U[NENO BAYA] WAKE, CHELINA NAYE NI HAWARA TU NA SABABU ZA KUWA WAZIRI ZINAJULIKANA...

  KJ NA SERIKALI YAKO MNACHO KITAFUTA KWA WATANZANIA MTAKIPATA TUMEWACHOKAAAAA AAAAAAAA.... TUACHIENI WA TZ TUANDAE KATIBA YETU
  Quote

  +1 #23 KIMICHO 2011-11-15 07:59 KUMEKUCHA!!!
  Quote

  +1 #22 stephen john 2011-11-15 07:59 itasikitisha endapo wabunge ambao ndio wasemaje wetu wataamua kuupitisha mswaada wa mchakato mzima wa katiba wenye maslahi makubwa kwa wananchi na taifa kwa ujumla pasipokutoa fursa kwa wananchi kuujadili kwa kina. ukweli ni kwamba kinachoandaliwa sasa ni kwa maslahi ya taifa na wananchi pia. taifa linaelekea siko kuzuri enda lonashindwa kutoa fursa kwa wananchi linao waongoza pia ni aibu kwa mbunge katika karne ya sasa kuunga mkono kitu kisicho kisichokidhi haja za wananchi wake. ijulikane kuwa bungeni si sehemu ya kuonekana kuwa upo, kuafiki kila hoja isiyotoa fursa na manufaa kwa wengi, au sehemu ya kupumzika bali ni kuwa makini juu ya hoja na kuzijadili kwa kina kisha kuafiki au kutoafiki. wabunge mliobaki hapo bungeni mnaonyesha wazi mnakubali hoja yamswada kusomwa mara ya pili au mnanidham na utii kwa bunge au mnaogopa kuenguliwa kwenye vyama vyenu au hamjoi chochote ju ya mswada kusomwa mara ya pili. tunaomba fanyeni kazi yenu kwa makini na pia sikilizeni kilio cha watanzania na sio maslahi binafsi.
  Quote

  0 #21 Meshack M. Ma`Ntog 2011-11-15 07:22 Kwa HAkika na kwa Umakini sana.
  Tunakila hali ya Kupiga kelele na mayowe ya Kukumbusha Viongozi Waandamizi Wote.
  Taifa hili lote sio mali ya Chama Tawala, au Chama pinzani. ni Taifa la Watanzania kwa kila mmoja na Utashi na Maadili yake. Hivyo napenda kuelezea juu ya Hiyoo iliwafanya baadhi ya Viongozi "kulazimisha" kuwa ndio Dira ya kuelekea kupata Katiba ya nchi na ikumbukwe sio ya chama tawala au vinginevyo.Tunaomba Irudi kwetu sio kwa Viongozi na Wabunge fulani,Tumewatu ma pale Bungeni kutuwakilisha na sio Kutulazimisha na kutuandikia ngonjera kwa manufaa ya muda mchache,hiyo ni kwa Vizazi vyote vya hapo mbele. Wabunge tusipende kutoka na hoja zetu za Itikadi,Tuangal ie mbele!! Nchi ya Tanzania na Mstakabali wake. Jambo la muhimu kama hilo lisifanyiwe Mzaha.
  Spika ni chombo kinachotoa Mlio baada ya chombo kingine kuingiza sauti tu, na sio spika kuwa wa Kwanza kutoa Sauti,Ameitoa wapi? na ameunganishwa na nini?
  Tuache Utani na Chombo hiki.
  Mwankijiji-Isanzu-Isene.
  Quote


  0 #20 DISMAS MBAWALLA 2011-11-15 07:11 hakika kwa utaratibu Tanzania tutafika zaidi tusikilizane na kuelewana katika HALI YA UTULIVU tutafikia muafaka wa haki,TANZANIA BILA MALUMBANO HAKI INAWEZEKANA
  Quote

  +1 #19 jembe 2011-11-15 07:09 CCM KUWENI NA AIBU NA MUWEKE UZALENDO MBELE, VINGINEVYO NYINYI NDO MTACHOCHEA VURUGU NCHINI. HIZI SIYO ZAMA ZA KUBURUZANA, WA2 WANAUCHUNGU NA NCHI YAO NDIO MAANA WANAKUWA WAKALI WANAPOONA MAMBO YA KURUDISHANA ENZI ZA MWAKA 47 YANAANZA. MIAKA 50 SASA TANGU TUMEJINASUA KWNY MIKONO YA WAKOLONI. SASA NYINYI MNATAKA KUWA WAKOLONI WE2 WA NDANI. MWOGOPENI MUNGU, WEKENI MCHAKATO HUU UWE WA HAKI, USAWA NA UWAZI. KATIBA NZURI NDIO ENGINE YA MAENDELEO. AU MNATAKA 2ENDELEE KUIMBA WIMBO WA TZ NCHI MASKIN.


  +1 #18 matangila 2011-11-15 07:07 Spika tutendee haki watanzania vinginevyo unataka tuamini kwamba upo hapo kwa ajili ya kulinda maslahi ya Mafisadi, yapo maneno yanayosemwa kwamba katika mchakato wa kumpata SPIKA, Mafisadi walifanya jitihada za dhati hatimaye ukaupata uspika, katika hili la mchakato wa kupata katiba mpya unataka watanzania tuamini upo nyuma ya Mafisadi, soma alama za nyakati mnajidanganya mtahaibika bure.
  Quote

  0 #17 Hamis 2011-11-15 06:41 Tanzania tunacheza na katiba! Ndugu msiingize siasa kwenye katiba. Kama nchi inatumia kiswahili kwa nini katiba iandikwe kwa kiingereza? Kama tafsiri ya kiswahili imetolewa wiki mbili zilizopita, wape wananchi muda waisome!
  Quote

  +1 #16 Paul Valence mshanga 2011-11-15 06:28 big up chadema na nccr kwa kile wananchi tunakitaka
  Quote

  +1 #15 R.M.Ruzangi 2011-11-15 06:24 KATIBA MBOVU NA CCM

  CCM HAWAJAJIFUNZA TOKA ZAMBIA? WANATAKIWA WAJUE KUWA WAO NDO CHAMA CHA UPINZANI BAADA YA UCHAGUZI MKUU 2015. KUENDELEA KUKUMBATIA KATIBA MBOVU KUTAWANYIMA HAKI ZAO ZA MSINGI NA WANANCHI KWA UJUMLA. SIKIO LA KUFA...................
  Quote

  +1 #14 Mrnd608 2011-11-15 06:22 Mpaka kieleweke! spika gani anayegeuka kuwa waziri bungeni!
  Quote

  +1 #13 Sam 2011-11-15 05:15 Tutazidi kushuhudia mengi ya hovyohovyo kutoka kwa huyu spika Makinda. Makinda ni Spika aliyewekwa na mafisadi na siku zote atalinda maslahi yao mafisadi. Bora Samweli Sitta alisimama kidete kuwatetea wananchi.

  Huu mchezo wa kudharau maoni ya wengine ni dalili ya udikteta wa CCM. Tanzania siyo nchi ya chama kimoja, lazima bunge liwe huru na lifanye kazi kama bunge la vyama vingi.

  Simuelewi spika anaposema kuwa hakutaka wajumbe wa kamati ya katiba kuenda mikoani kuapata maoni ya watanzania na nje ya nchi kujifunza kwa kuwa katiba ni yao????

  MUNGU IBARIKI TANZANIA
  Quote

  0 #12 Mzalendo Hasa 2011-11-15 03:56 Huu mchakato wa katiba mpya utatufunulia mambo mengi. Utatuwezesha kuona ni kiasi gani wananchi wa kawaida wameguswa na mabadiliko ya kuweza kutambua au kutotambua haki zao na uwezo mkubwa walionao kutetea haki zao badala ya kuiachia CCM iwaamulie. Huu ni wakati mwafaka sana wa vyama vya upinzani, pamoja na mashirika yasiyokuwa ya serikali kuwaeleza wananchi kwa ufasaha mkubwa mambo yanavyopindishw a na hawa CCM na taasisi zake - kwa mfano bunge na spika wao. Wanaanchi watasikia, na wataona, na baada ya yote hayo wataamua.
  Quote

  +1 #11 Msemaji 2011-11-15 03:18 Haya watanzania tutawaona sasa ni watu wa kulalamika tu huku mkiburuzwa ama mna msimamo wa nini mnakitaka. kataeni, kwa kujitokeza kwa wingi hadi mswaada urudishwe kwenu maana si wa CCM ni wa Tanzania. Kazi kwenu garagabahoo!
  Quote

  +2 #10 fr. amos epimack nya 2011-11-15 02:44 KWA HILI LA MUSWAADA WA KATIBA. SPIKA WA BUNGE, WAZIRI KOMBANI NA SERIKALI KWA UJUMLA KUWENI NA BUSARA NA UVUMILIVU: TAFADHALI WASHIRIKISHENI WANANCHI.
  Quote

  +1 #9 VANPERSIE 2011-11-15 02:11 sisi Watanzania ama tuna laana ama kuna kitu tumemkosea mungu!! hivi inakuwaje tunagawanyika hivi katika swala la kitaifa kama hili??hii katiba inayotengenezwa ni ya ccm au ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania?? Anyway whatever will come out of this speaker will carry all the blames!!
  Quote

  +2 #8 mati 2011-11-15 02:10 Wapendwa sana wanatanzania wenzangu nawasihiini tuamke, wakati uliokubalika ndiyo sasa wa kulikomboa taifa letu huko linakoelekea ni kubovu kwani kunanuka.Hawa viongozi wetu ambao hawana uchungu na nchi yetu wapo kwa aili ya matumbo yao na si kwa ajili ya matumbo yote ya taifa. Hivyo wabunge wa ccm ambao mwafahamu kusoma alama za nyakati vema simameni kidete kufichua huo uovu na hata kwenda kinyume wa wachache wanaodhorotesha heshima ya nchi yetu.Igeni mfano wa bunge la italia namna lilivyo fanya mapinduzi kumuondoa mheshimiwa wa starehe zake binafsi Berlusconi madarakani.Kaeni chonjo msifikiri wananchi tumekaa tu hivi kuwaangaliani, tupo kimya kutafakari,sasa umefika wakati tutachukua hatua kufungua mlango bila hata kubisha hodi na kuchukua kilicho chetu kwa nguvu yetu maana tumekosa imani nanyi.Hivyo kabla hatujafanya hivyo twawapatia sekunde kwa ajili ya kutafakari na kubadilika.Nimefikisha ujumbe kwa aliye na masikio na anataka kubadilika basi aufanyie kazi ujumbe huu,zaidi ndugu zangu wapendwa wanaccm ambao tunashabikia mambo hata kama niyauozo.
  Quote

  +2 #7 paul lutonja 2011-11-15 01:59 maoni yangu ni kuwa, kutokana na habari hii ni wazi kabisa mchakato mzima ni batili hasa pale spika alipozuia utafutaji wa maoni mikoani. hivyo watanzania tusikubali kuburuzwa penye kosa tushirikiane wote bila kuogopa polisi wala kuoneana aibu tupinge vikali upotoshaji wa ukweli.
  Quote

  +2 #6 DENIS SILAS 2011-11-15 01:45 Nawapongeza sana wabunge wa upinzani(Chadem a na NCCR) kwa kuonesha ukomavu wao wa kisiasa kwa kutoafiki kilichofanywa na Makinda, Siku zote maslai ya umma ni lazima yafuatwe na sio mipaka ya vyama vya siasa. Jaman mbona Spika anataka kutupeleka pabaya katiba ni ya watanzania wotena sio CCM, wabunge ni lazima msikilize maoni ya wananchi waliowaweka madaraka na sio vikao vya kamati za wabunge wa CCM, wananchi tutawawajibisha kwa kuwaondoa madarakani tu.
  Taifa tunapaswa kuingia barabarani kudai mswada usomwe kwa mara ya kwanza mpaka kielewekeeeeeee ee.
  Quote

  +1 #5 joseph Masanja 2011-11-15 01:43 NILISHA SEMA CCM HAINA DHAMIRA YA KWELI KUWAPA WATANZANIA KATIBA MPYA YETU MACHO TUSUBIRI KIINIMACHO KINGINE
  Quote

  0 #4 Burton_sat 2011-11-15 01:23 Hii serikali inapotupeleka pabaya sana.


  Haya ni maoni ya wasomaji wa gazeti la Mwananchi
  Watawala jaribuni kupitia muone reaction za watu juu ya issue nzima ya katiba
   
 2. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Ni hao wenye uwezo wa kuandika na kusoma vipi ambao hata internet hawajawi kuiona
   
Loading...