Maoni ya wasomi juu ya mwitikio hafifu wa wapiga kura (low voters turnout)

Wakuu hali ya uzalendo na mwamko wa Watz kushiriki matukio ya kitaifa inazidi kuzorota sana,

Katika chaguzi zilizopita hali inakuwa mbaya siku hadi siku watu wamekata tamaa kushiriki chaguzi, mfano unaweza kukuta idadi ya waliojiandikisha ni milioni 20, lakini wanaojitokeza kupiga kura ni milioni 2 tu, hii inazidi kuporomosha mwamko wa umma kushiri matukio ya kitaifa hasa Chaguzi,


Sasa kuelekea 2015, ninikifanyike ili kuhakikisha Watz wanawajibika hili kwa mjibu wa sheria?

Tunaweza kuhuisha sheria zetu ili kutibu watu kusiopiga kura kwa kuweka ulazima kisheria na usipopiga kura unapoteza sifa yako ya uraia na hivyo kukosa mambo kadhaa, kama kitambulisho chako, pasport, kupewa visa za kusafiri nje ya nchi na pia kulipia huduma za matibabu.

Ninakazia kwakusema hili liwekwe kwenye Katiba mpya kabisa kuwa Mtz yeyote mwenye sifa za kupiga kura asipopiga kura sheria ichukue mkondo wake,

Maoni yako mdau,
 
Ndg yangu siyo kwamba watu wamekata tamaa, ni kwamba daftari la kudumu mara ya mwisho limerekebishwa mara ya mwisho mwaka 2009. Huu ni muda mrefu kwa watu wa vijijini kutunza kiparata wakati mara nyingi matumizi yake ni uchaguzi tu.
 
Ndg yangu siyo kwamba watu wamekata tamaa, ni kwamba daftari la kudumu mara ya mwisho limerekebishwa mara ya mwisho mwaka 2009. Huu ni muda mrefu kwa watu wa vijijini kutunza kiparata wakati mara nyingi matumizi yake ni uchaguzi tu.

upo sahihi mkuu, hilo tuhimize mamlaka zilifanyie kazi
 
Yericko,

Tunahitaji Tume huru na imara ya uchaguzi. Hii tuliyonayo sasa pamoja na sheria zake (ambazo ni za miaka nenda rudi. haukuwa umezaliwa wakati huo), haiwezi kuleta tija.

Elimu ya uraia inahitajika kwa wananchi ili wafahamu kuwa ni haki yao ya msingi kabisa kumchagua kiongozi wanaomtaka. Waelimishwe pia kuhusu kutunza shahada zao za kupigia kura.

Huwa nasikitika sana kuona kuwa, shahada ya kupigia kura imefanywa kama ndiyo kitambulisho kwa kila mtu ambaye hana kitambulisho. Matokeo yake, ni rahisi shahada hizo kupotea.
 
Hii tulishaijadili hapa JF Hakuna cha kusema mwitikio wa watu ni mdogo, tatizo ni wizi uliopangwa tangu mwanzo. Idadi ya walioandikishwa siyo ya kweli hata siku moja. na imewekwa makusudi ili kutoa mwanya wa kuiba kura.

Kwa sensa ya 2012 mgawanyo wa umri ktk nchi unaonyesha kwamba wenye umri kati ya 0-17 ni 50.1%. Kama hii ni sahihi ina maana Walio na zaidi ya miaka 17 au kuanzia 18 kwenda juu ambao ndo wanaweza kupiga kura ni takribani 50% ya population yetu. waliojiandikisha kupiga kura ni chini ya hiyo 50% sasa inakuwaje kila wakati Tume inatuonyesha kwamba waliojiandikisha ni zaidi ya hiyo 50%? wanachosema ni kwamba hata watoto wamejiandikisha!

Hii ni taarifa ya uongo Kabisa!
 
Ni kuwacharaza viboko kwa kwenda mbele

Siasa za kibongo zimegeuka kuwa kichaka cha walafi, hata umchague nani bado atafanya mambo kwa maslahi yake binafsi, hakuna nafuu kati ya aliyetoka na anayeingia, hakuna anayemjali mpiga kura isipokuwa kumpa pilau, kofia na tshirt, watu wamekata tamaa, pengo la kipato kati ya mpiga kura na mpigiwa linazidi kupaa. Kusema ukweli hata mi siwezi kupanga foleni na jua kali kwenda kumchagua mtu ambaye atajali maslahi yake binafsi, I HATE BONGO POLITICS! kama ni viboko njoo uanzie kwangu.
 
Mimi naona sababu zifuatazo;
-Idadi ya Wapiga kura ilikosewa sana kulingana na idadi ya watu Tanzania 40.m 35% ndio waliopaswa kuwa wapiga kura yaani 14.m
-Siku ya kupiga kura sio conducive inatakiwa isiwe Ijumaa,Jumamosi au Jumapili hizi ni siku za Ibada na wengi hawawezi kusucrifice ya Mungu kwa Kaisari.
-Vitisho,kama watu wengine wanatembea na Visu,Marungu,Tindikali ,Mikuki,Mapanga n.k nani ajitokeze
-Bado hajatokea mwenye kujua namna ya kushawisi ili wapiga kura wategemee mabadiliko
-Labda mfumo umejenga hisia kuwa ili upige kura ni lazima Ulambe,kama hakuna lamba lamba hakuna kujitokeza
-Wanaogombea wamezoeleka ni wale wale imagine mtu ni mbunge tokea mwaka 1970 hadi leo hii,na hata wasipompigia anashinda tu.
-Siasa za liwalo na liwe,watu wamechoka mpaka wamezoea wana ona ndiyo maisha yao,wamekata tamaa
-Uwezo wa wananchi wetu kuchambua mambo ni mdogo hata wakipewa elimu ya uraia hawawezi kuelewa,hawafundishiki wamejitoa ufahamu,wamemwachia Mungu yote.
-Tume ya Uchaguzi sio huru,wao wana wanaotaka washinde
Nihayo tu na mengine ni mengi mno.
 
Wanajamvi

Kwanza naomba ni declare interest yangu kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ndio ulikuwa wa mwisho kwangu kupiga kura kumchagua kiongozi yeyote wa kisiasa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya tume hii ya uchaguzi na sheria hizi/hii ya uchaguzi.

Mara kadhaa nimewaona na kuwasikia wanasiasa,wachambuzi na wananzuoni mbalimbali wakielezea sababu mbalimbali za watanzania kushindwa kujitokeza kupiga kura kuwa ni pamoja na

-Kutoboreshwa kwa daftari la wapiga kura
- Wananchi kukatishwa tamaa na viongozi wanaowachagua
-Vurugu kwenye mikutano ya kampeni.nk.

Mimi binafsi sikuamua kuacha kupiga kura kwa sababu tajwa hapo bali.Bali kwa kuamini haya yafuatayo hapa chini.

1.Niligundua kuwa kura yangu na may be ya Mtanzania mwingine haina value ya kuchagua kiongozi nimtakaye chini ya tume na sheria ya uchanguzi ya sasa.

2.Mwenye mamlaka ya kuchagua kiongozi wa nchi hii awe diwani,Mbunge au Rais ni Msimamizi wa uchaguzi wa eneo fulani au mwenyekiti wa Taifa wa Tume ya Uchaguzi-According sheria ya sasa ya Uchaguzi

3.Vyombo vya dola badala ya kusaidia watanzania kupata kiongozi bora bila kujari anatoka chama gani vimekuwa sehemu za kamati za ushindi wa chama fulani


Wanajamvi binafsi chini ya sheria yetu ya uchaguzi na tume yetu hii ya uchaguzi sitegemei kujitokeza kwenda kupiga kura katika uchaguzi wowote-Nisaidieni kama nimebugi.


Wanajamvi
 
pamoja na kwamba katiba kuonekana kushindikana teyari baada umoja wa katiba ya wanchi ukawa kususia hatutakubali kushiriki uchaguzi wowote chini ya tume yauchaguzi ya hivi sasa.
 
Back
Top Bottom