Njowepo
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 9,710
- 2,239
Kabla ya wananchi kupiga kura Oktoba 31, kulikuwa na malalamiko mengi kutoka kwa watu tofauti kuhusu uwezekano wa kutoshiriki kwenye zoezi hilo.
Malalamiko hayo yalianzia kwa vyama kutaka nakala za daftari hilo mapema, baadhi ya watu kutaka muda wa kuboresha daftari hilo uongezwe, wanafunzi wa vyuo kutoshiriki kutokana na vyuo kufungwa na majina ya watu kutoonekana kwenye daftari.
Maoni ya Profesa Lipumba dhidi ya Nec yanafanana na ya wasomi na wanazuoni waliozungumzia matokeo ya uchaguzi huo wa nne tangu kuanza kwa vyama vingi baada ya zaidi ya watu milioni 11 waliojiandikisha kupiga kura, kutojitokeza Oktoba 31 kutumia haki yao ya kidemokrasia.
Mhadhiri na mkuu wa kitengo cha sheria kwenye Chuo Kikuu cha Tumaini kilicho mkoani Iringa, Renatus Mgongo alisema ana wasiwasi kwamba daftari la wapigakura halikuhakikiwa ipasavyo na ndiyo sababu kuna idadi ndogo ya watu waliojitokeza kupiga kura ikilinganishwa na wale waliojiandikisha.
Mhadhiri huyo alisema kuwa huenda idadi ya wapiga kura iliyotangazwa na Nec haikuwa sahihi kutokana na ukweli kwamba hakukuwa na uhakiki thabiti wa wapiga kura, waliofariki na wale ambao wamehamishwa vituo ambao majina yao yalionekana na baadhi kukosekana.
"Mfano kuna mtu niliyemfahamu ambaye jina lake nililiona huku na yeye amehamishiwa Kigoma ambako pia alikuta jina lake, sasa hapa nilipata tabu kuelewa imekuwaje mtu mmoja kuonekana mara mbili wakati daftari limehakikiwa," alisema.
Alisema sababu nyingine ni kutojitokeza kwa wananchi wengi kupiga kura kutokana na utendaji kazi wa viongozi waliokuwa madarakani ambao haukuwaridhisha kutokana na vile walivyokuwa wakitarajia.
"Mambo mengi yamesababisha idadi ya waliojitokeza kupiga kura kuwa ndogo... wengi hawakuridhishwa na utendaji kazi wa viongozi ambao haukuwa na impact kwa maisha ya kawaida ya wananchi, hivyo wakaona kwamba hakuna umuhimu kwao kupiga kura," alisema.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro, Ali Nassor alisema matokeo ya tafiti zilizofanywa na taasisi za Redet na Synovet yalichangia kukatisha tamaa wananchi kujitokeza kupiga kura kwa kudhani kwamba mshindi ameshajulikana.
"Tafiti kama vile Redet na Synovet zilionekana kama matokeo halisi ya uchaguzi na wananchi kuona kuwa CCM ndio itashinda. Baadhi ya watu hawakuona umuhimu wa kwenda kupiga kura," alisema Nassor.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine(SUA), Clavery Tungaraza alisema ikiwa Tanzania ina wastani wa watu milioni 42, si rahisi waliojiandikisha kufikia watu milioni 19.8.
Alisema kuwa idad hiyo ni kubwa na inatia wasiwasi kuwa huenda takwimu za Nec zinakinzana na uhalisia uliopo katika maeneo ya kupigia kura.
Kuhusu vituo vya kupigia kura, Dk Tungaraza alisema kwa vijijini tume ilijitahidi kuwa na vituo vingi ili kukidhi ongezeko la wapiga kura, lakini bado ni tatizo kwa mijini ambako kumekuwa na vituo vichache na hivyo kusababisha baadhi ya watu kutojitokeza kupiga kura kwa hofu kuwa wangetumia muda mwingi vituoni.
Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Profesa Idrisa Kikula alisema miongoni mwa sababu hizo ni kukosekana kwa uhakika wa usalama wa raia.
Profesa Kikula alisema wananchi wengi waliingiwa na hofu wakati wa kampeni kutokana na jazba zilizokuwa zikisababishwa na kauli za baadhi ya wagombea pamoja na wapambe wao, jambo ambalo liliwajengea hofu na kuamua kutojitokeaa kupiga kura.
"Wananchi hawakuhakikishiwa usalama wao; wengi walikuwa na hofu ya kutokea machafuko kutokana na picha iliyojitokeza wakati wa kipindi cha kampeni; vyombo husika vilipaswa viwahakikishie wapigakura kuwa kutakuwepo na usalama wa kutosha, vinginevyo hali hii itaendelea kujirudia," alisema Kikula.
Kikula pia alisema kuwa baadhi ya watu walishindwa kwenda kupiga kura kutokana na kupoteza shahada zao, hivyo elimu ya kuhifadhi nyaraka hizo ilitakiwa itolewe na pia kutafutwa namna itayomwezesha mtu aliyejiandikisha kwenye daftari, apige kura hata kama atakuwa amepoteza shahada yake.
"Sio hapa Tanzania tu, hata huko Ulaya jamii ya watu wanaojiita wamestaarabika imekuwa haijitokezi kwenda kuchagua viongozi kwa visingizio kibao. Wengine wanaona kama ni kupoteza muda; wegine wanasema yeyote atakayechaguliwa ni sawa, lakini jambo kubwa hapa kwetu nasisitiza wananchi wahakikishiwe usalama wao, naamini watajitokeza vya kutosha kupiga kura," alisema Profesa Kikula.
Mkurugenzi wa kituo cha redio cha SAUT, Bulendu Dotto alisema kujitokeza kwa watu wachache kupiga kura kunaweza kuwa na sura tofauti, na kushauri ipo haja ya kufanyika utafiti wa kina.
Alitaja sababu mojawapo ambayo inaweza kuwa imechangia ni kuwepo kwa hofu ya kwa vurugu katika zoezi zima la upigaji kura ambayo ilijengwa na viongozi wa majeshi hapa nchini.
Alisema kauli ambazo zilikuwa zikitolewa na viongozi wa majeshi kuwa watadhibiti vurugu kwa nyakati tofauti, ziliwajenga hofu wapigakura ambao waliamua kutojitokeza kupiga kura kwa kuhofia vurugu.
"Ukiangalia takwimu za tume kuwa waliojiandikisha ni watu milioni 19, na waliopiga ni milioni 7, hapa mie napata shaka kuwa huenda takwimu za Tume zilikuwa zimepikwa na hazikuwa sahihi. Kama waliopiga kura ni milioni 7 ina maana jumla ya watu milioni 12 hawajapiga kura, hii inaweza kuwa takwimu za Tume si sahihi," alieleza mkurugenzi huyo.
Naye mratibu wa uchaguzi wa CCM wa mikoa ya Tanga, Arusha na Kilimanjaro, Stephen Mashishanga alisema kilichochangia kuwa na idadi ndogo ya wapigakura ni ukosefu wa elimu ya uraia.
Alisema kuwa ni wajibu wa Nec na vyama vya siasa kutoa elimu hiyo kabla ya uchaguzi. Alisema vyama vilieleza sera zao tu majukwaa na kusahau kuwa jukumu la kutoa elimu ya uraia pia linavihusu vyama vyote.
Naye mwanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE), Charles Daud tatizo hilo linatokana na Nec kuwa na takwimu zisizo sahihi na kushauri kuwa na kipindi cha maboresho ya daftari wa wapigakura wakati wa kampeni kwa vile wapo ambao walijiandikisha katika maeneo mengine na inapofika wakati wa kupiga kura wanakuwa wamehama.
"Mfano wakati Tume inafanya maboresho, mimi nilikuwa Musoma, lakini wakati wa uchaguzi nilikuwa Mwanza, sasa ningepiga vipi kura wakati nimebadilisha makazi," alieleza.
Naye mkazi wa Mwanza, Fatuma Saidi alisema tatizo hilo linatokana na Nec na serikali kutojali elimu ya uraia kwa wapigakura.
Alisema watu wengi walijiandikisha kwa ajili ya kutumia shahada za kupigia kura kama kitambulisho, lakini hawajitokezi kutokana na kutotambua umuhimu wa kupiga kura.
"Nilijiandikisha lakini sikuona umuhimu wa kupiga kura, kwa vile mara zote mbili nilizompigia kura mtu niliyemtaka, aliangushwa na mgombea wa CCM. Mfano mwaka huu nilimpenda sana mgombea urais wa Chadema, lakini nilijuwa kuwa hata akipigiwa kura, atashinda wa CCM sijui kura tukipiga wanazifanyaje... bora sikupiga," alisema mwanafunzi huyo wa CBE.
Mhadhiri katika Mt Tumaini, Dk Fairles Ilomu alitaja sababu zilizofanya wananchi kutojitokeza kwa wingi kuwa ni sheria mbovu za nchi na kufungwa mapema kwa usahihishaji daftari la kupigia kura.
Imeandaliwa na Petro Tumani, Hidaya Omar, Israel Mgussi, Dodoma, Tumaini Msowoya, Iringa, Frederick Katulanda, Mwanza na Venance George, Morogoro