Maoni ya wananchi: Suluhu ya msongamano wa magari jijini Dar es Salaam

Planning tu ni mbovu hapa kwetu,hao wataalam wa mipango miji hawatumii ipasavyo hizo elimu zao na sio wabunifu kabisa.Pia serikali inamchango mkubwa katika hili tatizo,ina waweka hao wataalum maofisini tu kula mishahara ya bure,hawawapati hata vijisafari kwenda nchi zingine kuangalia jinsi gani wenzao wanapanga miji yao.kwahiyo tukiwa na watu na mfumo wa namna hii tusitegemee kabisa kwamba tunaweza kuona mabadiliko tunayo yategemea.

Nimepita mahara furani leo asubuhi,pale Kigamboni kama 2 0r 1.5 km kutokea kwenye Ferry kuna watu wanajenga Mtalo wa maji pembeni ya barabara huu sasa ni mwezi wa 2 au 3 hawajafika hata mita 500,nikajiuliza "huku si ndio kwny mradi huo wa MJI MPYA sasa hiki nini kinaendelea?" nilikua nategemea labda watakua wanachimba kuweka underground train for that matter,kumbe mtaro!!

Sasa namna hii sidhani kama tunania za kweli na yale tunayo yasema au kusemwa na Viongozi wetu
 
Jamani tatizo kubwa la DAR ni poor planning,Sioni sababu ya kutoza watu pesa kwani sio kosa lao, asilimia kubwa ya magari binafsi ni ya mkopo na wenye nayo wamejitahidi kutokana kero za public transport (daladala).

Ukitoka nyumbani umevaa tai kama unatumia daladala tai inaeza kuwa kitanzi chako,wajawazito ni mateso makali wanapata, all in all mjini katikati kunatakiwa kujengwe parkin za gorofa ambazo zinaweza kuhifadhi magari kama 3000 hadi elfu saba.

Na inatakiwe kuwe na sheria kila goirofa inayojengw iwe na sehemu ya kupark magari,barabara zinatakiwa zipanuliwe, nyingine za katikati ya mji zinatakiwa zigeuzwa one way, na huo mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi ukamilishwe kama kweli serekali ina nia,

From there hata kama unagari utaona ni hasara kulitumia na watu wengi wataacha magari nyumbani na kutumia public transpsort
 
Ndugu,

Umekuja na wazo zuri sana, ila kama jamaa alivyosema solution ni kuwa na reliable massive public transport. Hii ndio chanzo cha mradi unaousikia kuhusu mabasi yaendayo haraka (BRT).

Hii concept niliwahi kuiandikia lakini ni ngumu kuingia katika vichwa vya watu. Mradi huu ninaufuatilia kwa karibu sana. Unamwelekeo mzuri ingawa kwa waliowengi wangependa kuyaona hayo mabasi.

Kwa kifupi mradi huu ulianza tangu 2004 ambapo mpaka sasa ni takriban miaka sita. Tulivyozoea sisi waTanganyika ni kuwa tukisema lete mradi tunataka UWE. Hali hii imepelekea miradi mingi kufa baada ya muda mfupi kwa kukosa systematic analysis and planning.

Cha ajabu sisi tunasema ni mradi hewa ila huko duniani wanasifia ni mradi unaoenda systematic kuliko BRT Systems zote Africa. Kwa sasa South Africa wako mbioni kuuendesha wakati wa world cup (South Africa). Kwa Tanzania kama ni mfuatiliaji kuna matangazo yanatolewa na TANROADS kwa ajili ya ujenzi wa DART Infrastructures ambayo DART ndio haswa mradi wa mabasi ya haraka dar es salaam (DAr Rapid Transit).
 
Mradi wa DART muda si mrefu utakuwa ndoto. Kama tutawahi sana Basi la kwanza litakuwa njiani mwaka 2015 vinginevyo ni mpaka mwaka 2020. Haya ni makisio yangu na yanatokana na hali halisi. Je tunafanya nini sasa iwapo hasara itokanayo na foleni ni zaidi ya shilingi bilioni 120 kila mwezi?
 
Mimi hapa pia nimeuona huo mchoro kwenye ippmedia.com, unapendeza kwa kweli, i'm not proficient in architectures but i really do think that there are much simpler drawings,cheaper and more efficient plans than what has just been unveiled today by UCLAS in solving the same problem.

SteveD.
Roundabouts a.ka. keeplefts
 
SteveD na wengine,

Flyovers ni ndoto. Kama kweli tunataka kuondoa foleni Dar la muhimu zaidi ni kufikiria ni kwa jinsi gani tutapunguza magari binafsi katika barabara zetu. Hilo ndiyo tatizo letu kuu. Tukumbuke kuwa ukileta gari za abiria 5,000 ambapo kila moja ina uwezo wa kubeba abiria 30, ni sawa na kuondoa barabarani gari binafsi zaidi ya 100,000. Uzuri wa mkakati huu ni kuwa gharama yake ni ndogo sana. Kimsingi ni suala la uamuzi na kuweka utaratibu mzuri.
 
Kuna njia nyingi na za uhakika kuondoa tatizo la msongamano wa magari. Unaweza kutumia trams au kutumia treni kama wanavyofanya kwenye miji ya Tokyo na London. kwa sababu sisi Tanzania tumeuwa shirika la reli hii ni ndoto lakini ndio mkakati wa kuondoa tatizo hilo sugu kimsingi.

Hii miradi mingine ni ya Pwagu na Pwaguzi.
 
nina uhakika wazee wa mji wakiamua kushirikiana na JF watapata ufumbuzi.........maana hapa nimeona kuna ma-Civil/Highway Engineers, Transportation Engineers and Planners etc etc............Wazee wa Mji toeni Traffic Data na Network ya DSM muone wana JF watakavyowashukia masolutions..............ila at the end muwe serious kwenye utekelezaji...........

Mkiwapa akina kamanda wa trafiki polisi Kombe na Mwaibula watu wasio na deep elimu ya kunyumbulisha mamboya transportation na traffic demands.........mtakuwa mnatwanga maji........
 
FM, heshima mbele mkuu..... Kwa kweli hapo umesema ambacho nilikuwa nakifikiria.... Unakumbuka matatizo ya umeme?? tumezoea kufanya vitu ki- "fire fighting fire fighting", na kwa vile mkuu amesema jengeni tungoje kuona matokeo....

Mungu Ibariki Tanzania na watu wake......
 
Siku yakijengwa wataitwa mapadri na mashehe ili kuyabariki maana hata daraja la waenda kwa miguu Manzese, lilifunguliwa na Rais Mwinyi!

Kweli jambo kama hili linahitaji Research fellow atoe makala maalumu kwenye gazeti! Ni sawa na kuweka makala eti unataka kuweka traffic lights mji wa Arusha.

Hilo ni jambo jipya Dunia hii ya 2010? Faida zake zinahitaji researcher aseme? Naye kakosa kazi ya kufanya maana siamini kwamba Wizara ya miundo mbinu haina injinia wa kusema hilo.

Wanasiasa wetu kila siku wako majuu au huwa wanakwenda macho pembeni wakiangalia magorofa na miniskirts?

Si ulaya tu, Lagos ina flyovers nyingi kuliko hata London. Cairo nayo iko juu na yalijengwa miaka ya 50's na 60's.

Potezeni muda kumuonyesha Waziri mkuu na Rais njia bora za kupita.
 
ile foleni ya kufa mtu miaka nenda rudi lakini hawa watu plan yao ni porojo tuu,maji hakuna,umeme kiduchu wa bei mbaya,barabara ndio balaa tena...hivi hawa wanafanya kazi gani?
 
..tatizo hilo linahitaji multiple approaches and solutions.

..wasije wakajikuta wanasababisha congestion hata kwenye fly-overs!!!
 
nina uhakika wazee wa mji wakiamua kushirikiana na JF watapata ufumbuzi.........maana hapa nimeona kuna ma-Civil/Highway Engineers, Transportation Engineers and Planners etc etc............Wazee wa Mji toeni Traffic Data na Network ya DSM muone wana JF watakavyowashukia masolutions..............ila at the end muwe serious kwenye utekelezaji...........

Mkiwapa akina kamanda wa trafiki polisi Kombe na Mwaibula watu wasio na deep elimu ya kunyumbulisha mamboya transportation na traffic demands.........mtakuwa mnatwanga maji........

Manabii huwa hawakubaliki nchini kwao. Hata Yesu alipigwa mawe itakuwa Bongo!
 
Hatuna wataalam kama hii ndiyo proposal yao.

Amandla.........

FM, that proposal is from UCLAS these guys are not engineers!!!

Solutions can be found at COET and chuo cha usafirishaji not this crap! I find disgusting for someone to write this stupid in our society; u can easily see

1. lack of multidiscplinary inputs
2.Focus
3.his solution; is neither feasible nor viable
4. Future plan of our country

Jamaa katokota kabisa

Mkuu wataalamu wapo, tafiti nyingi sana zinaoza kwenye makabati UDSM, nani anajali
 
Sorry to digress,

Neno "suluhu" linatumika kama "solution"?

Ninavyojua mimi "suluhu" ni makubaliano, kama vile wapinzani wanaweza kukutana ili kutafuta suluhu, suluhu ya "agreement" is not necessarily a solution.

Kwa mfano, timu za Simba na Yanga zikitoka suluhu 0-0 zinakuwa bado hazijatoa solution ya nani mkali zaidi ya mwenzake.

Mimi sielewi matumizi haya ya neno "suluhu" kwa maana ya "solution" yanakujaje.

Tujibu hili tukiwa na nia ya kuendelea kwenye mjadala huu muhimu.
 
Yote yanawezekana ila tunahitaji viongozi wenye utashi wa kweli kuhusu maendeleo ya taifa letu. Kuendelea kuwa na wafanya biashara katika uongozi tutaendelea kuimba ngojera hapa bila mafanikio yoyote. Nchi inaendeshwa ki siasa kwenye kila nyanja hata zile za kitaalamu bado siasa tu, kuwe na mipaka kati ya wataalamu na hawa watawala wetu.
 
stori zote hizi huwa zinaeleweka vizuri tu kwa wahusika...sasa ngoma iko katika utekelezaji...na je kuna dili au hakuna???
 
Flyover?
Shame on u who is sugesting that thing plus your boss (president)
shule zimewashinda hata kununua madawati tu ya hali ya chini..then u still think nonesense! R u serious guys?
Barabara ziko wapi za kuweka flyover hapa nyinyi! Hizi one way kama njia za panya (barabara kuu utadhani barabara za kuingia uswahilini manzese!)...
Utaweka flyover gani..acheni siasa zisizo na maana hapa!!!!panueni hizi hizi barabara zenu na kutakuwa hamna foleni..bongo kuna gari ngapi hapa, sema tu hamna barabara bali vichochoro! Stop thinking that shit
 
Narudia tena maneno yangu, huyo research fellow wa UCLAS kaongea kinadharia zaidi kuliko kimatendo. Kama barabara za ardhino tu zinatushinda je itakuwa hizo flyovers na underpasses? Njia pekee ni kuanzisha miji mpya ambako sheria za kikoloni zitatumika kuhusiana na upangaji wake na ukazi.
 
Back
Top Bottom