Tetty
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 26,356
- 21,390
Mbunge anawajibika kwa maslahi ya makundi manne mpiga kura wake, kwa chama chake kilichompa ridhaa, kwa taifa lake na yeye mwenyewe binafsi. Hivyo mbunge anabaki kuwa ni mwenye kuangalia maslahi yote hayo. Akiona swala husika linalengo la kukiathiri chama chako hawezi kuliunga mkono. Pia ikiliona swala ni la maslahi kwa taifa hata kama linakiathiri chama chake ataliunga mkono.
Kwa hiyo mifano ya ufafanuzi michache utakuwa umeelewa. CCM wamekuwa wakifanya uamuzi mbalimbali ambao ulikuwa kwa maslahi ya taifa na ulikuwa unakiathiri chama. Mfano sakata la Richmond na Escrow. Uamuzi ulitolewa na wabunge wengi wa ccm ambao ndio wafanya uamuzi. Ukibisha kwa hili nitajua nawasiliana na mtu gani. Wabunge wa ccm wanaongoza kwa kuangalia maslahi ya taifa.
Siwezi kukubishia na nadhani ndiyo sababu nimemjibu huyo jamaa yangu.Wabunge wa CCM wanafikiria MATUMBO yao zaidi kuliko TAIFA.Ni bora nimchague mbunge anayeangalia TAIFA kwanza then JIMBO baadaye Chama kuliko Chama kwanza Taifa mwisho