(1)Watanzania ni waoga mno wa mabadiliko ya kisiasa na hawaoni mbele sana kutokana na fikra mgando.
(2)Wananchi wanategemea serikali iwatoe kwenye umasikini wakati uzalishaji na upokeaji wa kodi ni mdogo.
Watanzania wengi ni wavivu wa kazi na wakwepaji wa kodi. Starehe tumeiweka mbele.
Kila siku tunazalisha aina mpya ya pombe badala ya kuzalisha kompyuta na madawa ya kujikinga na magonjwa.
(3)Sisi bado tunasubiri kuonyeshwa na serikali jinsi ya kuzalisha kama wakati wa ujamaa.
Kuna wengine hapa JF pia wanadai sera za Ujamaa ndio nzuri zaidi kwa Watanzania.
Wameshasahau njaa na shida za ukosefu wa bidhaa chini ya siasa ya ujamaa na kujitegemea ya Nyerere. Tunasubiri kulishwa, kuvishwa, kuelimishwa na kutajirishwa na serikali yetu badala ya kujituma wenyewe.
(4)Wakati wenzetu na nchi nyingine duniani wameruhusu Uraia pacha, sisi bado tunang'ang'ania eti itaathiri usalama wa taifa. Sababu kubwa ya kupinga sio usalama wa taifa bali ni kutoona mbele kutokana na fikra mgando. Upingangaji wa uraia pacha unaenda kinyume na mambo ya dunia ya kileo. Mbingu hazijashuka Kenya wala Uganda waliporuhusu uraia pacha!
(5)Swala la ardhi ndio kabisa usilishike. Jamii ya Tanzania inategemea kuwa wakulima wadogo wadogo, masikini na wenye elimu duni ya kilimo ndio njia pekee ya kuilisha jamii. Kuna ardhi kubwa tunashindwa kuitumia kwa kuwa hatuna uwezo wa kulima kitalaamu kwa kutumia matrekta na mbegu za kisasa. Ndio maana mpaka leo tunanunua matunda nje badala ya kuzalisha nchini. Watanzania watailalamikia serikali kwa ujinga huu lakini ukweli ni kuwa hawako tayari kumpa bepari ardhi ili alime kwa wingi. Wako tayari kumlipa bepari mwingine anayoishi Afrika Kusini asiowapa ajira wala kodi, ili mradi asiiguse ardhi yao.
(6)Tusifikiri ukubwa wa watu na ardhi, pamoja na rasilimali ndio itatuletea maendeleo zaidi ya wenzetu. Utajiri ni elimu bora, kwenda na wakati katika mambo ya Uzalishaji, utamaduni wa kuchapa kazi na siasa bora. Mfano hai: Singapore.
Ndugu yangu naona umejibu kwa jazba zaidi kuliko kuangalia uhalisia wa mambo. Naomba nikujibu nukta zako kama nilivyo zianisha hapo juu.
1. Ni kweli Watanzania ni waoga katika hii EAC. Je, uoga wao ni wa kipuuzi au una maana?
Mwaka 1967 ilianzishwa EAC. Tulikubali kila kitu kiwe cha EAC bila kuwa na msingi wa umoja uliojengwa na wananchi na wala si viongozi. Asubuhi moja Charles Njonjo akaaamua kuzuia kila kitu.
Tanzania hatukuwa na kitu, thanks to China, Bulgaria, na marafiki zetu kama Msumbiji waliokuja kutuokoa. Je huoni kuna kila sababu ya kuchukua tahadhari. Fool me once you, shame on you. Fool me twice, shame on me.
2. Hakuna wananchi wa taifa lolote duniani waliojikomboa katika umasikini bila serikali za nchi au maeneo yao kuwa na mipango mizuri. Jana, Rais wa Marekani Obama alitoa state of the union speech.
Alichokiongelea kama asilimia 85 ni jinsi ya kupunguza umasikini kule Marekani kwa masikini ambao wao wanawaita middle class.
Hao Kenya, Uganda n.k. hawaamki tu kama kondoo, kama yapo mafanikio, hayo ni matokeo ya mipango ya serikali zao.
Kuna maendeleo ya mtu mmoja mmoja, lakini huwezi kukwepa mipango ya pamoja. Ndio maana tuna serikali na si zizi la ng'ombe
3. Kenya waliwahi kukabiliana na njaa, si mara moja au mbili. Hawakuwa wajamaa.
Malawi wamekabiliana na njaa, si mara moja au mbili. Hawakuwa wajamaa
Nchi zote zina matatizo, hivyo ujamaa usiwe kisingizio.
Mapigano ya Kenya hawakusababishwa na ujamaa, huoni kama hilo ni tatizo kama mengine. Rwanda hawakuwahi
Na muhimu katika hoja ni kuwa, hebu tueleze ni taifa gani duniani lisilotekeleza ujamaa? Tutajie moja tu.
4. Kuruhusu Urais pacha si tatio ni suala la kutangaza tu. Tatizo ni matatizo yatakayotokana na hilo.
Sijui mwenzangu una mtazamo gani, hata mimi ningependa Uraia pacha.
Inapotokea hakuna hata nationa ID kama mataifa mengine unayosema dunia huoni kuna walakini.
Au labda ungeruhusu tu kila mtu wa taifa lingine awe raia kwavile hatutumii akili zetu bali kufanya mambo kama wengine.
Hao waliopo tayari wana matayarisho yao. Suala hapa ni kuwa jambo hili umeliangalia kutoka angle zote au ni kwa vile Uganda wanayo basi ni kudandia treni, utaamua unakwenda wapi baadaye.
5. Ardhi, leo unasema hivyo kwavile unayo. Waulize Kenya, wanachinjana kwasababu gani?
Nenda Kilosa na Arusha uone nini kinaendelea kwa wakulima na wafugaji. Wewe bado huoni tatizo unataka tatizo zaidi
Kama Nyerere angeitoa kama njugu pengine leo wewe usingekuwa na hatahatua kumi.
Lazima utembee duniani uone matatizo ya ardhi. Si suala la kulima, ni zaidi ya hapo
Zimbabwe kuna ugomvi wa ardhi. Waulize Rwanda kwanini wanakuja kuishi Tanzania.
Waulize Kenya, asilimia 10 ya population inapomiliki asilimia 90 ya ardhi maana yake ni nini.
Kama unadhani ardhi si muhimu, iweje wenzetu waone ni umuhimu katika EAC. Kwanini basi wasiache tu kwa vile si muhimu.
Waulize Waisrael na Wapalestina, na fuatili migogoro ya dunia ukue chanzo chake ni nini.
Hapo middle east wanapigana binamu ambao wote wamepokea manabii na mitume.
Ugomvi mkubwa si imani, ni ardhi.
Hapa huna hoja kabisa, walioishi wakati wa masetla ya kigiriki na ukoloni wanjua.
Wewe huoni maana ya ardhi kwasababu unayo au inawezekana ni Mkenya huna.
Kwa wenye kutumia vichwa, hapa watakuwa wabatabasamu kama si kukucheka
(6) well la elimu ni sawa, lakini hayo si mambo ya ndani?
Na hao wenzetu wa EAC elimu imewasaidiaje kumaliza umasikini.
Unaweza kutueleza ubora wa masikini wa Uganda/Kenya Vs Tanzania ili tujue?