Maoni ya CHADEMA juu ya katiba mpya ya Tanzania

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573

Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba (kulia) wakiongozwa na Dkt. Salim Ahmed Salim wapokea maoni kuhusu Katiba Mpya kutoka kwa uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ulioongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Freeman Mbowe katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo Januari 7, 2013.

A. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MUUNDO WAKE

1. Kutakuwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo itakuwa ni shirikisho lililoundwa na nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar.
2. Kutakiwa na haki kamili ya kila nchi inayounda Jamhuri ya Muungano kujitoa katika Muungano lakini haki hiyo itatumiwa kwa masharti kwamba uamuzi wa kujitoa katika Jamhuri ya Muungano lazima upate ridhaa wa upande husika kwa kura ya maoni…

2. Kutakiwa na haki kamili ya kila nchi inayounda Jamhuri ya Muungano kujitoa katika Muungano lakini haki hiyo itatumiwa kwa masharti kwamba uamuzi wa kujitoa katika Jamhuri ya Muungano lazima upate ridhaa wa upande husika kwa kura ya maoni (referendum/plebiscite) kwa idadi isiyopungua theluthi mbili ya kura zote halali.
3. Kutakuwa na Serikali ya Muungano ambayo itakuwa na madaraka juu ya mambo ya Muungano pekee. Mambo ya Muungano yatakuwa yafuatayo:
(a) Mambo ya nje yanayohusu masuala ya diplomasia lakini yasiyohusu ushirikiano wa kimataifa;
(b) Ulinzi na usalama isipokuwa kwa masuala ya polisi na magereza;
(c) Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano (Supreme Court of the United Republic);
(d) Uraia na uhamiaji;
(e) Sera za fedha na sarafu;
(f) Sera za biashara ya kimataifa na masuala ya forodha;
(g) Masuala ya ithibati ya elimu ya juu.
4. Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa Mkuu wa Serikali ya Muungano, Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano.
5. Rais wa Jamhuri ya Muungano atachaguliwa na Wajumbe wote wa Bunge la Muungano, Bunge la Tanganyika, Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wenyeviti, mameya na magavana wote.
6. Rais wa Jamhuri ya Muungano atachaguliwa kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na anaweza kuchaguliwa kwa kipindi kingine kimoja cha miaka mitano, na atachaguliwa kwa msingi wa kuachiana zamu ya kushikilia madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Kati ya nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano.
 
Ritz me najua unaikubali sana CDM ndani ya nafsi yako, ila kikwazo mawazo yako yamefungwa ndugu. Ipo siku uki achiwa huru utatambua jinsi gani wana Tanzania wanavyo pata shida kutokana na hao wenzako, kua huru kwa ukombozi wa Tz badae usije beba zambi kutokana na maumivu na machungu ya wa Tz wengi sasa ivi, ujue wana lia na machozi yao hayato enda ivi ivi yatapita na wote mlio changia wao walie. Usiku mwema brother Ritz
Hongera JK kwa kuipigania Katiba mpya.
 
Last edited by a moderator:
Hongera JK kwa kuipigania Katiba mpya.
We jichanganye,mwenzio anajua kama asingeridhia hii kitu saa hizi angekuwa uhamishoni,mtu asiyejua nchi yake ni masikini kwa sababu gani anaweza kuwa na fikira za kutengeneza katika mpya,kamuulize yeye angependelea katika izingatie mambo gani,kama hautamkana.
 
A. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MUUNDO WAKE
1. Kutakuwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo itakuwa ni shirikisho lililoundwa na nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar.
4. Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa Mkuu wa Serikali ya Muungano, Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano.
5. Rais wa Jamhuri ya Muungano atachaguliwa na Wajumbe wote wa Bunge la Muungano, Bunge la Tanganyika, Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wenyeviti, mameya na magavana wote.
Hapa sijaelewa kidogo kama kuna mwenye ufahamu zaidi anieleweshe,

Inamaana kutakuwa na Marais watatu? ( Rais wa Tanganyika, Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya muungano)
 
A. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MUUNDO WAKE
1. Kutakuwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo itakuwa ni shirikisho lililoundwa na nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar.
2. Kutakiwa na haki kamili ya kila nchi inayounda Jamhuri ya Muungano kujitoa katika Muungano lakini haki hiyo itatumiwa kwa masharti kwamba uamuzi wa kujitoa katika Jamhuri ya Muungano lazima upate ridhaa wa upande husika kwa kura ya maoni (referendum/plebiscite) kwa idadi isiyopungua theluthi mbili ya kura zote halali.
3. Kutakuwa na Serikali ya Muungano ambayo itakuwa na madaraka juu ya mambo ya Muungano pekee. Mambo ya Muungano yatakuwa yafuatayo:
(a) Mambo ya nje yanayohusu masuala ya diplomasia lakini yasiyohusu ushirikiano wa kimataifa;
(b) Ulinzi na usalama isipokuwa kwa masuala ya polisi na magereza;
(c) Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano (Supreme Court of the United Republic);
(d) Uraia na uhamiaji;
(e) Sera za fedha na sarafu;
(f) Sera za biashara ya kimataifa na masuala ya forodha;
(g) Masuala ya ithibati ya elimu ya juu.
4. Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa Mkuu wa Serikali ya Muungano, Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano.
5. Rais wa Jamhuri ya Muungano atachaguliwa na Wajumbe wote wa Bunge la Muungano, Bunge la Tanganyika, Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wenyeviti, mameya na magavana wote.

Ikiwezekana tupate hicho kijarida cha maoni ya CDM maana nyama muhimu ili kuchangia.

Kwa uchache tu naona hii ni sera ya serikali tatu lakini kwa upande wa ZNZ mambo kama ya biashara ya kimataifa, na masuala ya forodha ni utata kidogo.

ZNZ inataka kuwa huru kibiashara mfano kuanzisha bandari huru. Kwa hiyo mambo ya ushuru bora kila upande uwe na mfumo wake wa forodha.

Kwa waZanzibar naona bado ni changa tu hili.
 
Tunaona ni section A tu, kama kuna mwenye rasimu yote tunaomba aiweke hapa ili tuone masilahi ya Tanganyika kama ilivyo Zanzibar yamelindwa vipi, kwa faida gani na kwa namna gani.
 
R.B Kumbe Viongozi wa CHADEMA hawajui Zanzibar wanachokitaka!. ZNZ wanatakakuwa huru hasa kibiashara na kujitawala kwa ujumla bila kubanwa ama kuwekewa pingamizi, iwe Nchi kama Nchi zingine.
 
Last edited by a moderator:

3. Kutakuwa na Serikali ya Muungano ambayo itakuwa na madaraka juu ya mambo ya Muungano pekee.

4. Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa Mkuu wa Serikali ya Muungano, Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano.

5. Rais wa Jamhuri ya Muungano atachaguliwa na Wajumbe wote wa Bunge la Muungano, Bunge la Tanganyika, Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wenyeviti, mameya na magavana wote.
.

Nadhani Rais wa Jamhuri ya Muungano anakuwa reduced to non-political figure (possibly kama ilivyo kwa Italy). Tunaweza kupata more details hasa kuhusu 'title' ya viongozi wa juu wa Zanzibar na Tanganyika. Mfano wataiwa rais, waziri mkuu or what?
CC @Nguruvi3 JokaKuu
 
inafurahisha somehow lakini hawakuongea vipi nchi mbili hizi zitaongozwa kama ni magavana ama raisi.hapo watuweke wazi.
 
Nadhani ni haraka mno, Mnyika anaweza kutuanikia hapa, tunachotakiwa ni kum-pm atatuletea uhondo wote.
 
1. Muungano mnautaka wa nini wakati watu wa visiwani (Pemba na Unguja) hawautaki?
2. Muungano ulitakiwa uwe ulishavunjika tangu Uamsho na viongozi wengi na wanachama wengi wa visiwani kuukataa waziwazi. Hii ina maanisha mawaziri kama Nahodha, yule mama wa Fedha, Mwinyi na Makamu wa Rais na wengineo walitakiwa wawe wameondoka kwenye nyadhifa wanazoshikilia kwakuwa dhahiri muungano hautakiwi na kwa maana hiyo nafasi wanazotumikia hazitaleta tija kwa wa Bara.
3. Muungano ulitakiwa kuwa umeshavunjika, lakini kwakuwa Bado, Katiba mpya iuvunje na itamke waziwazi kuwa wapemba na waunguja wote waondoke haraka huku Bara waende kwao visiwani na mali walizochuma wabebe, viwanja watuaachie na wale wakuu wa idara mbalimbali huku bara ambao ni wa zanzibar warudi kwao mara moja na watakuwa wanakuja huku kwa taratibu maalum kama ambavyo mtu toka bara anavyoweza kwenda Rwanda ama nchi yoyote nyingine
TUNABEMBELEZA NINI TOKA KWA HAWA UAMSHO?
 
Wabara walioko zanzibar ni wasiwasi mtupu na sidhani kama wanatanua kama wapemba huku wanavyoweza kusumbua mtaa kwa mapikipiki ama kufunga mtaa kisa wanasherehe. Wabara wakifanya hivyo huko visiwani naamini tutawakuta washakuwa majivu
 
Nguruvi3, MrFroasty, FJM,

..mimi sikubaliani na mapendekezo ya CDM.

..ukiyasoma hayo na mapendekezo ni kana kwamba wameziba masikio kabisa kuhusu madai ya ZANZIBAR HURU.

..ushauri wangu ni kuwa na Tanganyika huru, na Zanzibar huru, ambazo zitashirikiana kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki.

..zaidi mapendekezo yao ni kama vile wametutukana wa-Tanganyika. Eti wanapendekeza Tanganyika iwepo, lakini Raisi wake hatakuwa na majeshi ya ulinzi, wala uwezo wa kutangaza vita.

..suala la URAIA na UHAMIAJI nayo imependekezwa yawe chini ya muungano. Miaka 48 tangu tuungane ni wa-Tanganyika wangapi wanataka kuishi Zanzibar?? Hivi CDM wamefanya utafiti gani kujiridhisha kwamba kuna wa-Tanganyika wa kutosha wanaotaka kuishi Zanzibar?

..pia wanapendekeza Uraisi wa muungano kwa utaratibu wa kupokezana!! sasa tukianza kupokezana kwenye muungano, kwanini tusipokezane huku Tanganyika wanakopendekeza sera ya majimbo, au Zanzibar kati ya Unguja na Pemba??
 
Mkuu, ndiyo maana nimeomba rasimu nzima. Niliposoma tu hayo ya hapo juu nikaona hawa CDM wanataka kufanya mambo ya ajabu sana. Wao ni washiriki wazuri sana wa forum mbali mbali za jamii. Nilitegemea waone mambo kwa mtazamo tofauti, inaonekana wamekuja na mambo ya kutaka kuwapendeza watu milioni 1 ambao nusu yao wanaishi kwetu.

Hivi ulinzi na usalama tubnashirikiana nini hasa?
Halafu madai yote ya ZNZ huru inaonekana wanayakataa. Mfano, ZNZ inadai kiti UN ambacho kwa mfumo wa CDM hakipo.
Elimu ya juu kwanini iwe muungano tukijua gharama zake kwa Tanganyika.
Ushuru na forodha ndio kwanza ZNZ hawataki sasa kwanini wasiachiwe wawe huru kabisa

CDM inaonekana kukubaliana na dhana ya kumtwisha Mtanganyika zigo tena

Na kibaya CDM ilipaswa ieleze kwanini muungano au kwanini hapana.
 
Nguruvi3,

. Zitto anadai muungano ni tunu yetu wa-Tanzania, na kwamba unatupa heshima na fahari ya kukataa mipaka iliyowekwa na wakoloni.

..wenzetu wako busy na kuona fahari kwa mambo ya ubunifu, ugunduzi, uundaji, pamoja na mambo mengine, sisi tunataka ku-settle score with our former colonial masters.

NB:

..kwa mapendekezo ya CDM, Tanganyika ikivamiwa hakuna ruhusa kutangaza vita mpaka Baraza la wawakilishi ZNZ watoe kibali.
 
Last edited by a moderator:

Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba (kulia) wakiongozwa na Dkt. Salim Ahmed Salim wapokea maoni kuhusu Katiba Mpya kutoka kwa uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ulioongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Freeman Mbowe katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo Januari 7, 2013.

A. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MUUNDO WAKE

1. Kutakuwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo itakuwa ni shirikisho lililoundwa na nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar.
2. Kutakiwa na haki kamili ya kila nchi inayounda Jamhuri ya Muungano kujitoa katika Muungano lakini haki hiyo itatumiwa kwa masharti kwamba uamuzi wa kujitoa katika Jamhuri ya Muungano lazima upate ridhaa wa upande husika kwa kura ya maoni…

Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba (kulia) wakiongozwa na Dkt. Salim Ahmed Salim wapokea maoni kuhusu Katiba Mpya kutoka kwa uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ulioongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Freeman Mbowe katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo Januari 7, 2013.

A. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MUUNDO WAKE
1. Kutakuwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo itakuwa ni shirikisho lililoundwa na nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar.
2. Kutakiwa na haki kamili ya kila nchi inayounda Jamhuri ya Muungano kujitoa katika Muungano lakini haki hiyo itatumiwa kwa masharti kwamba uamuzi wa kujitoa katika Jamhuri ya Muungano lazima upate ridhaa wa upande husika kwa kura ya maoni (referendum/plebiscite) kwa idadi isiyopungua theluthi mbili ya kura zote halali.
3. Kutakuwa na Serikali ya Muungano ambayo itakuwa na madaraka juu ya mambo ya Muungano pekee. Mambo ya Muungano yatakuwa yafuatayo:
(a) Mambo ya nje yanayohusu masuala ya diplomasia lakini yasiyohusu ushirikiano wa kimataifa;
(b) Ulinzi na usalama isipokuwa kwa masuala ya polisi na magereza;
(c) Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano (Supreme Court of the United Republic);
(d) Uraia na uhamiaji;
(e) Sera za fedha na sarafu;
(f) Sera za biashara ya kimataifa na masuala ya forodha;
(g) Masuala ya ithibati ya elimu ya juu.
4. Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa Mkuu wa Serikali ya Muungano, Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano.
5. Rais wa Jamhuri ya Muungano atachaguliwa na Wajumbe wote wa Bunge la Muungano, Bunge la Tanganyika, Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wenyeviti, mameya na magavana wote.
6. Rais wa Jamhuri ya Muungano atachaguliwa kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na anaweza kuchaguliwa kwa kipindi kingine kimoja cha miaka mitano, na atachaguliwa kwa msingi wa kuachiana zamu ya kushikilia madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Kati ya nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano.

Mi nimeshangaa kipengele cha mwisho kuhusu kupokezana urais. Nafikiri humu humu jf wanachadema ndio waliokua wa mwanzo kupinga hili swala na kusema kuwa rais wa muungano badala ya mwinyi hatikei mwengine, haya sasa imekuaje wakayi wapiga kura milioni 40+ ni watanganyika? ( kama mnavosema)

Pia niliskia kuwa chadema wanataka kuwe na majimbo, kila jimbo lijitegemee, jamani hii kitu hatuoni kama ni kukwamisha maendeleo ya sehemu moja na kuimarisha kwengine? Majimbo yatakuwa manne, north south west na east, sasa tuseme kila jimbo likiambiwa litoe fungu la milioni 100 je majimbo yenye ukame na yalokua hayana nyenzo za uchumi yatazipata wapi pesa? Mimi binafsi naona hii sera ni kuanza kuigawa nchi kidogo kidogo, naona wanataka kuwaiga mabwana zao wamarekani kiwa na majimbo wakayi wenzetu walikua nayo kabla ya kuanzishwa USA.

Jengine nlosiki hili limenichekesha sana, na kama kweli hapa ndipo nnapoona wanachadema wamekosa mtazamo wa mbali!
Eti wanataka ardhi iwe mali ya mwananchi na sio serikali, khah! Hii kitu duniani hamna kabisa. Leo tujiulize, nyumba ngapi zimevunjwa ili kupisha miundombinu? Sasa ikiwa ardhi ni mali ya mwananchi, huoni kama patazua balaa ukitaka kupitisha miundo mbinu? Maana mwananchi atakuwa na haki ya kukataa kuvunja na kuondoka, si ushasema ni mali yake? Au mtu ana kibamda cha makuti anasema yeye mpaka alipwe milioni 500 ndo ahame, ni haki yake coz ni mali yake, pamekaaje hapo? Kama haya mambo kweli basi nishaona hakuna maendeleo zaid ya kuzidi kurudishana nyuma. Bora CCM ivo ivo
 
Back
Top Bottom