Maoni: Watu hawa wapewe Udaktari wa heshima

Maoni: Watu hawa wapewe Udaktari wa heshima

WAFUATAO WAPEWE UDAKTARI WA HESHIMA HARAKA SANA.

Leo nami nimeona nitoe maoni yangu kuhusu hili suala la watu kutunukiwa udaktari wa heshima kwa mambo waliyoyafanya kwenye jamii. Gumzo kubwa ni baada ya Mheshimiwa Musukuma kupata udaktari wa heshima siku za hivi karibuni. Huenda kuna mambo makubwa Mh Musukuma kayafanya huko Geita hadi maeneo ya jirani Chato ndo maana wasomi wakaona wamtunuku.

Sasa mimi leo nimekuja na majina ambayo naona yanastahili kupewa udaktari wa heshima kwa mambo makubwa waliyoyafanya hapa nchini, haya majina yataambatana na ufafanuzi mfupi;

1. FILBERT BAYI

Huwezi kutaja riadha Tanzania bila kulitaja jina la Filbert Bayi. Huyu mzee alikuwa mwanariadha mashuhuri duniani aliyevunja rekodi kwenye mbio fupi za mita 1500 na maili moja. Sifa alizoziletea nchi sio za kubahatisha au za ku-boost na kiki kama vijana wa leo wanavyofanya. Hata baada ya kustaafu bado ameendelea kujihusisha na mchezo wa riadha huku pia akiwa katibu mkuu wa kamati ya olimpiki. Kimsingi huyu mzee ni miongoni mwa wazalendo wachache waliopo hapa nchini. Nadhani anastahili kuitwa Dr. Filbert Bayi.

2. Leodger Tenga

Huyu mzee kama ilivyo kwa Bayi pia naye alikuwa mwanamichezo wa mpira wa miguu aliyekuwepo kwenye timu iliyoshiriki kombe la Afrika. Pia kwenye uongozi wake TFF alileta mabadiliko makubwa baada ya kupokea uongozi uliokuwa chini ya Muhidin Ndolanga. Apewe udaktari maana hakuna namna.

3. Mr II "Sugu"

Huyu aliubeba muziki wa Bongo Fleva mabegani. Kupitia uvumilivu wake na kujituma aliweka misingi ya hii Bongo fleva ya leo. Apewe PhD

4. Master Jay, P-funk na Mika Mwamba.

Hawa watayarishaji wa mwanzo wa muziki wanastahili tuzo kwa kazi kubwa waliyoifanya. Kupitia ndoto zao wakaleta matumaini kwa vijana wengi.

5. Zitto Kabwe

Huyu kwa upambanaji wake alisababisha vijana wengi wajihusishe na siasa. Pia kupitia hoja zake bungeni ilibidi baadhi ya sheria zifanyiwe marekebisho hasa zinazohusu madini. Nadhani Zitto apewe tu hiyo PhD.

6. Mbwana Samatta

Mtanzania wa kwanza kucheza ligi kuu ya England. Haina haja ya kujadili sana kuhusu Samatta. Apewe PhD haraka sana.

7. Augustine Lyatonga Mrema

Mzee wa Kiraracha apewe tu hiyo PhD kwa sababu ni mmoja wa waasisi wa upinzani Tanzania walioleta mabadiliko makubwa kwenye siasa za nchi hii.

8. Haji Manara
Sikubali mbona umewaacha Masanja na Steve Nyerere, hawa wameionesha dunia Tanzania ni ya watu wa aina gani.
 
Mi napendekeza jina la marehmu Shabani robert litunukiwe Phd japo mwenyewe kafa kitambo.
 
Unampaje Sugu Unamuacha Diamond role model wa vijana wengi wakizazi kipya
 
Msipompa Mzee Mpili basi na hao wote wasipewe
 
Usimsahau Jumanne Kishimba mbunge huyu ana madini yakiwa fanyiwa Kazi tutasonga mbele
 
Unampaje Sugu Unamuacha Diamond role model wa vijana wengi wakizazi kipya
Sugu aliutuliza moto wa machinga na police Mbeya ambao ungesambaa nchi nzima,ccm isingekuwepo madarakani.
 
Labda waendelee kupewa PhD za kina Dr. Msukuma na bogus universities.....
 
Kabisa,
Sasa mtu anapewa PhD wakati Hana hata cheti cha form four....
Hii PhD ya Dr. Msukuma haina tofauti na tusua mapene ya vodacom, tunachojua ukifaulu vizuri degree ya kwanza unaweza kuwa recommended kufanya research ambayo unaweza kuwa awarded PhD badala ya Masters, sasa ndugu yetu msukuma kutoka la saba B hadi PhD hii pasi siyo ya dunia hii....
 
Back
Top Bottom