Maoni: Watu hawa wapewe Udaktari wa heshima

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,202
22,244
WAFUATAO WAPEWE UDAKTARI WA HESHIMA HARAKA SANA.

Leo nami nimeona nitoe maoni yangu kuhusu hili suala la watu kutunukiwa udaktari wa heshima kwa mambo waliyoyafanya kwenye jamii. Gumzo kubwa ni baada ya Mheshimiwa Musukuma kupata udaktari wa heshima siku za hivi karibuni. Huenda kuna mambo makubwa Mh Musukuma kayafanya huko Geita hadi maeneo ya jirani Chato ndo maana wasomi wakaona wamtunuku.

Sasa mimi leo nimekuja na majina ambayo naona yanastahili kupewa udaktari wa heshima kwa mambo makubwa waliyoyafanya hapa nchini, haya majina yataambatana na ufafanuzi mfupi;

1. FILBERT BAYI

Huwezi kutaja riadha Tanzania bila kulitaja jina la Filbert Bayi. Huyu mzee alikuwa mwanariadha mashuhuri duniani aliyevunja rekodi kwenye mbio fupi za mita 1500 na maili moja. Sifa alizoziletea nchi sio za kubahatisha au za ku-boost na kiki kama vijana wa leo wanavyofanya. Hata baada ya kustaafu bado ameendelea kujihusisha na mchezo wa riadha huku pia akiwa katibu mkuu wa kamati ya olimpiki. Kimsingi huyu mzee ni miongoni mwa wazalendo wachache waliopo hapa nchini. Nadhani anastahili kuitwa Dr. Filbert Bayi.

2. Leodger Tenga

Huyu mzee kama ilivyo kwa Bayi pia naye alikuwa mwanamichezo wa mpira wa miguu aliyekuwepo kwenye timu iliyoshiriki kombe la Afrika. Pia kwenye uongozi wake TFF alileta mabadiliko makubwa baada ya kupokea uongozi uliokuwa chini ya Muhidin Ndolanga. Apewe udaktari maana hakuna namna.

3. Mr II "Sugu"

Huyu aliubeba muziki wa Bongo Fleva mabegani. Kupitia uvumilivu wake na kujituma aliweka misingi ya hii Bongo fleva ya leo. Apewe PhD

4. Master Jay, P-funk na Mika Mwamba.

Hawa watayarishaji wa mwanzo wa muziki wanastahili tuzo kwa kazi kubwa waliyoifanya. Kupitia ndoto zao wakaleta matumaini kwa vijana wengi.

5. Zitto Kabwe

Huyu kwa upambanaji wake alisababisha vijana wengi wajihusishe na siasa. Pia kupitia hoja zake bungeni ilibidi baadhi ya sheria zifanyiwe marekebisho hasa zinazohusu madini. Nadhani Zitto apewe tu hiyo PhD.

6. Mbwana Samatta

Mtanzania wa kwanza kucheza ligi kuu ya England. Haina haja ya kujadili sana kuhusu Samatta. Apewe PhD haraka sana.

7. Augustine Lyatonga Mrema

Mzee wa Kiraracha apewe tu hiyo PhD kwa sababu ni mmoja wa waasisi wa upinzani Tanzania walioleta mabadiliko makubwa kwenye siasa za nchi hii.

8. Haji Manara
 
Sasa hii taaluma ya udaktar msihifedheheshe kiasi hicho master j hapo wakaxi gani
 
Wengine wapewe diploma za heshima, vyeti vya heshima vya form four na six kwa mambo ya kimaendeleo waliyoyafanya kwenye kwenye jamii. Heshima kwa kila level ya elimu kwa asiyenayo kutokana na ukubwa wa jambo la kimaendeleo alilolifanya kwa jamii
 
Hebu mtoe manara hapo ,basi huo udaktari ni watching.. hivi manara kafanya nn cha maana kwenye soka la nchi hii?zaid uropokaji na kejeli kwa watu
 
Tunasubiri na udaktari (Phd) wa dharau maana penye heshima pia pana dharau kama ilivyo watu ulimwenguni huibuka kidedea kwa ulimbwende wao na wengineo kwa ubaya wao
 
WAFUATAO WAPEWE UDAKTARI WA HESHIMA HARAKA SANA.

Leo nami nimeona nitoe maoni yangu kuhusu hili suala la watu kutunukiwa udaktari wa heshima kwa mambo waliyoyafanya kwenye jamii. Gumzo kubwa ni baada ya Mheshimiwa Musukuma kupata udaktari wa heshima siku za hivi karibuni. Huenda kuna mambo makubwa Mh Musukuma kayafanya huko Geita hadi maeneo ya jirani Chato ndo maana wasomi wakaona wamtunuku.

Sasa mimi leo nimekuja na majina ambayo naona yanastahili kupewa udaktari wa heshima kwa mambo makubwa waliyoyafanya hapa nchini, haya majina yataambatana na ufafanuzi mfupi;

1. FILBERT BAYI

Huwezi kutaja riadha Tanzania bila kulitaja jina la Filbert Bayi. Huyu mzee alikuwa mwanariadha mashuhuri duniani aliyevunja rekodi kwenye mbio fupi za mita 1500 na maili moja. Sifa alizoziletea nchi sio za kubahatisha au za ku-boost na kiki kama vijana wa leo wanavyofanya. Hata baada ya kustaafu bado ameendelea kujihusisha na mchezo wa riadha huku pia akiwa katibu mkuu wa kamati ya olimpiki. Kimsingi huyu mzee ni miongoni mwa wazalendo wachache waliopo hapa nchini. Nadhani anastahili kuitwa Dr. Filbert Bayi.

2. Leodger Tenga

Huyu mzee kama ilivyo kwa Bayi pia naye alikuwa mwanamichezo wa mpira wa miguu aliyekuwepo kwenye timu iliyoshiriki kombe la Afrika. Pia kwenye uongozi wake TFF alileta mabadiliko makubwa baada ya kupokea uongozi uliokuwa chini ya Muhidin Ndolanga. Apewe udaktari maana hakuna namna.

3. Mr II "Sugu"

Huyu aliubeba muziki wa Bongo Fleva mabegani. Kupitia uvumilivu wake na kujituma aliweka misingi ya hii Bongo fleva ya leo. Apewe PhD

4. Master Jay, P-funk na Mika Mwamba.

Hawa watayarishaji wa mwanzo wa muziki wanastahili tuzo kwa kazi kubwa waliyoifanya. Kupitia ndoto zao wakaleta matumaini kwa vijana wengi.

5. Zitto Kabwe

Huyu kwa upambanaji wake alisababisha vijana wengi wajihusishe na siasa. Pia kupitia hoja zake bungeni ilibidi baadhi ya sheria zifanyiwe marekebisho hasa zinazohusu madini. Nadhani Zitto apewe tu hiyo PhD.

6. Mbwana Samatta

Mtanzania wa kwanza kucheza ligi kuu ya England. Haina haja ya kujadili sana kuhusu Samatta. Apewe PhD haraka sana.

7. Augustine Lyatonga Mrema

Mzee wa Kiraracha apewe tu hiyo PhD kwa sababu ni mmoja wa waasisi wa upinzani Tanzania walioleta mabadiliko makubwa kwenye siasa za nchi hii.

8. Haji Manara
Tayari thread imeshaingia doa
 
Back
Top Bottom