MAONI: Mawaziri wa wizara wapatikane kwa kinyang'anyiro maalumu

Mwalupale

JF-Expert Member
Apr 29, 2012
1,049
672
Habari zenu wana jamvi.

Nimekaa nikawaza sana namna ya utendaji kazi wa hizi wizara zetu za serikali za kiafrika na "KUTAMANI" mambo yangekuwa kama ifuatavyo..

1. Kila wizara apatikane waziri ambae sio wa kuteuliwa. Wasomi mbalimbali waliobobea kwenye masuala nyeti yahusuyo maendeleo ya wizara husika waandike proposal za kuvutia zenye strategic plans za maendeleo chanya zilizo na tija kwa taifa na kisha jopo la independent and credible selection commitee zisome na kufanya shortlisting, proposal hizo ziwe disseminated kwa umma (kwa njia maalumu) na kupigiwa kura na wananchi wenyewe kwa mfumo maalum ambao hauna upendeleo. (Wananchi ndio waamuzi wa mwisho wa kujua nini wanataka kifanyike kupitia wizara flani)

2. Proposal/strategic plan itakayopita iwekewe memorandum of understanding na mkataba kati ya malengo yaliyoadhimiwa kufikiwa na zitungwe sheria mahsusi zitakazowabana (ikiwamo kufunguliwa kesi na kufungwa kabisa) watendaji kazi watakaoshindwa kufikia malengo yaliyopangwa. Malengo hayo yawe tangible na sio ya kusadikika na kudhania dhania. Wananchi wa kawaida waweze kuyang'amua na kushiriki katika utekelezaji wake kikamilifu.

3. Wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na makatibu wa wizara, mikoa na wilaya wasiteuliwe. Wasomi wenye experience weledi katika masuala ya planning and administration waombe kazi na kuchujwa kwenye interview maalum isiyo na bias ya aina yoyote ile. Kiufupi vyeo hivi viwe huria na vitoe nafasi kwa watu wote wenye uwezo wa kufanya kazi kisawasawa. Ifike mahala wenye vyeo hivi wasifanye kazi kwa kusujudia watu flani au kwa milengo ya kisiasa pia sheria ziwabane wasipowajibika kwa kufuata malengo makuu ya wizara mbalimbali zilizoshinda kinyang'anyiro (kama nilivyobainisha hapo juu).

4. Raslimali za nchi yetu mfano madini, ardhi yenye rutuba kwajiri ya kilimo, maziwa na bahari, maliasili na vivutio vyote vya watalii kama vile mbuga za wanyama vitumike kwa weledi wa hali ya juu na kutoruhusu mikataba ya kinyonyaji. Wizara huzika zitakazopita kwenye kinyang'anyiro cha uwaziri zihakikishe zimeeleza vizuri plans zao kuhusu utajiri huu wa taifa.

5. Mahakama na vyombo vya ulinzi vifanye kazi kwa haki na kwa kuzingatia utu. Vyombo vya uchunguzi wa makosa mbalimbali vifanye kazi kwa weledi wa hali ya juu na bila upendeleo. Ikibidi teknolojia itumike wanapokuwa wanalinda raia na mali zao. Inapobidi wananchi washirikishwe kunapokuwa jambo hatari ili wachukue tahadhari na waotoe ushirikiano basi na ifanyike ivyo.

6. Raia wawe na uhuru wa kujieleza na kutoa maoni pamoja na kukosoa inapobidi. Lakini wapotoshaji na wajanja wajanja wanaojali maslahi yao binafsi au maslahi ya watu/mtu flani wakati wanatumia haki yao ya kujieleza/kutoa maoni/kukosoa wasiachwe bila kushughurikiwa. Kiufupi kuwa na mutual dialogues ambazo zina tija kwa taifa pale mambo yanapoenda mrama au ukakasi wowote unapojitokeza unaoweza kuyumbisha mustakabali wa taifa.


Mwisho kabisa napenda kusema kwamba mambo ninayotamani yafanyike ni mengi sana ambayo naamini taifa lolote likiyachukua basi hata Rais Trump hawezi kunyanyua kinywa chake kulitusi. Je wewe unatamani nini kifanyike nchini mwako ili raia wake wapate maendeleo na waishi kwa furaha na amani?

Naomba kuwasilisha.
Ndimi nduguyo kutoka somalia.
Ahsante
 
Mimi natamani utoke huko somalia uje Bongoland ugombee Urais na uupate, hakika hayo yote uliyosema yatawezekana na tutaishi kwa furaha na amani. Ahsante.
 
Huu ushauri unautoa kwa nchi gani? Kama ni Tanzania you are lost. Tanzania ni nchi ya vyama kwanza ndiyo maana nunua ya wanasiasa imepamba moto. Maendeleo ya kiuchumi na kijamii si priority...
 
Ni Sawa na kumpa kazi Kocha then Timu nzima unamchagulia Halafu unamuajibisha Timu ikifungwa
 
Back
Top Bottom