Maoni kipindi cha Mkasi

Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
5,680
2,000
Mkasi kila nikijaribu kuangalia show yenu on Youtube ili kuwa updated na habari za nyumbani nazidi kuwa disappointed, badala ya kwenda mbele mnarudi nyuma. Mwishowe sitakua na budi ila kuacha kuangalia hiki kipindi.

Matatizo yale yale kila siku, mpangilio wa maswali, kuingiliana kwa waulizaji na kumuingilia anaehojiwa. Hii inatutoa watazamaji nje ya hamu ya kuendelea kuangalia kipindi

Utambulisho. Hamtoi utambulisho wa kutosha kuhusu wageni, mfano Chegere, huyu jamaa yawezekana wengi wanamjua ila naamini tuliowengi hatumjui. Kama ni uwezo wake kielimu ilibidi mtoe utambulisho wa kina ili muweze kwenda sambasamba na watazamaji. Ilibidi aulizwe alama zake ili watu wajue uwezo wake na mambo kama hayo

Mpangilio wa maswali yenu ni hovyo sana yani mnauliza hili mnaenda huku mnarudi kule mnaruka tena sijui mnatumia mfumo gani wa kuuliza maswali. Pamoja na kwamba theme ya kipindi ni kimtaa/kijiweni/maskani zaidi ila professionalism lazima izingatiwe since mnarusha kwa TV.

Nipende kutoa rai pia juu ya maswali yaulizwayo, uzito wa maswali uongezwe hasa kwa watu ambao ni "Public figures" na wageni wote kwa ujumla. Baada ya utambulisho, maswali mepesi na maswali ya kizushi ulizeni maswali mazito ambayo yataacha mchango katika jamii. Boresheni maswali yenu. Kujua maisha binafsi ya wageni kiundai isiwe main focus ya kipindi. Sio mbaya kama mtakua mnafanya research kidogo kabla hamjawahoji wageni wenu

I wonder kama hizi ni extended versions hizo short versions kwenye runinga zinakuaje smh
 

Jaslaws

JF-Expert Member
May 31, 2011
6,036
2,000
Utangazaji ni ubunifu,wao wamebuni kuandaa kipindi cha namns hiyo,mi sion kms kuna ubaya.!
 

Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
5,680
2,000
Utangazaji ni ubunifu,wao wamebuni kuandaa kipindi cha namns hiyo,mi sion kms kuna ubaya.!
Come on! Huwezi sema umechagua utaratibu mbovu ili uwe tofauti

Huwezi leta Mgeni bila kutoa utambulisho kwa kudhani kila mtazamaji anamjua Hakuna utangazaji wa namna hiyo

Hata katika mazungumzo ya kawaida kuna utaratibu wa kuongea hii Ni common sense tu sio Lazima uambie. Mara ngapi Salama anamnyamazisha Muba asiingilie flow ya convo! Inamaana hata wao wanajua sasa kwanini wasifanyiwe marekebisho watu wanachoka kasoro hizo hizo
 

maedson

Senior Member
Sep 7, 2012
151
225
Umeongea kitu chenye busara sana

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom