Blue Bahari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,230
- 1,141
Habarini wadau!
Kwa kuwa jana (17/05/2020) Mh: rais katupa matumaini ya hali nzuri ya nchi yetu na kwamba anafikiria kufungua vyuo na michezo mda si punde.
Sasa mimi nikiwa kama mdau mmojawapo wa elimu, nina pendekezo lillilo na namna mbili za kufanya:
(1) Aidha walimu na wanafunzi wapimwe covid-19 kabla hata ya shule kufunguliwa, kisha wapeleke vyeti vyao (kwa Mwalimu mkuu/Mkuu wa shule) kuthibitisha wako salama. Kisha Masomo yaendelee.
(2) Shule ikishafunguliwa, kabla ya masomo kuanza, walimu na Mwanafunzi wote wapimwe covid-19 ili kubaini nani yuko salama au ni mgonjwa.
Utaratibu wa upimaji uwe unafanyika kila baada ya wiki moja kwa kila Mwalimu na Mwanafunzi.
Nimetoa maoni hayo, kwa kuwa wanafunzi (wakiwemo na walimu) wamekuwa mtaani kwa mda mrefu wakiwa wamechangamana na watu wa aina tofauti. Hivyo, kama tutaruhusu tu wanafunzi na walimu waanze masomo kienyeji, Nina wasi wasi yanaweza kutokea kama yaliyiyotokea kule Ufaransa ambapo baada ya shule kufunguliwa, kuna bahadhi ya shule zililazimika kufunga tena baada ya bahadhi ya wanafunzi kupimwa na kugundulika kuwa covid-19 ktk shule hizo.
Hivyo, kwa usalama zaidi ya watoto wetu, ni vyema mamlaka zikashughulikia upimaji wa Mara kwa Mara kwa wanafunzi ili kuepusha balaa zito zaidi la kuambukizana covid-19 kwa kuwa kwa kiwango kikubwa kutoka ktk shule za kata, idadi ya wanafunzi ktk darasa ni 50+.
Nawasilisha.