Mimi ni Kijana ambaye nimekulia Arusha na ninajua watu wengi wa Arusha wanavyofikiria. Arusha ni mji wa wafanya biashara wadogowadogo na kitu kimoja ambacho watu wa Arusha hawapendi ni maisha yao kuingiliwa. Kwa uamuzi wa Judge kutengua ubunge wa Lema wana Arusha hata wale waliokuwa hawampendi Lema hawatafurahishwa na uamuzi kwasababu ni kama vile wameingiliwa kwenye maisha na maamuzi yao ya Arusha. Kwa hasira hizi watu wengi waliokuwa CCM watapigia kura Chadema. Watu wa Arusha hawaamini watu wa Dar kabisa hata wa CCM. Huyu Jaji ameisadia Chadema kwani sasa watu wanaona wenyewe wazi jinsi Mahakama inavyotumia kisiasa maana juzi tu wameona Lusinde wa CCM alivyotukana waziwazi lakini hakuna mahakama wala mwana CCM aliyesema chochote. Sisi watu wa Diaspora tunawashauri Watanzania wote kuleta maendeleo na kupinga rushwa. Tanzania ni nchi ambayo huwezi kamwe kulazimisha demokrasia na muda wa kudanganya wananchi hata wa vijijini umekwisha. Itafikia wakati wa Majaji kupigwa mawe! kama ikiendelea hivi