Sijui nisemeje hapa, na huo mfano wa Zanzibar.Zanzibar wamewahi jaribu Kwa njia ngumu zaidi ya hizi za kwetu katika chaguzi zao lakini wakaendelea kupotea Ushindi Kwa mabavu.
Mikakati thabiti ndiyo inayohutajika, maandamano yakiwemo.
Nashukuru sana kukumbushia mfano huo, huo ni mchango muhimu wa kutafuta majibu kwa CHADEMA na sisi wote.
Lakini nadhani kuna tofauti kubwa sana kati ya hayo ambayo hufanyika Zanzibar, na yanayoweza kufanyika hapa Tanzania Bara kukiwa na maandalizi mazuri.
Kumbuka pia, mazingira yatakuwa ni tofauti sana wakati huu, hata huko huko CCM kwenyewe.
Ngoja tuzidi kukuna vichwa.
Na katika "mikakati thabiti", binafsi ule wa kutoshiriki uchaguzi kwa kususa tu, huo siyo mkakati hata kidogo.
"Maandamano" yakihusu nini, kudai Katiba Mpya, huku CCM akiendelea na maandalizi yake ya kufanya uhalifu kwenye uchaguzi?
Historia ya waTanzania inaonyesha siyo watu wa maandamano sana. Sijui CHADEMA watafanya juhudi zipi za ziada kuwatoa watu wa kutosha barabarani, tena bila kikomo. Hii itakuwa kazi ngumu sana!