Maongezi vijana wa Tanzania; 96% ni pumba

Vijana wengi wa kitanzania (Sehemu za miji mikubwa ikiwemo Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya) 96% ya maongezi yao ni pumba tupu na vitu visivyowasadia katika kujikwamua kimaisha ikiwemo mpira wa Ulaya (FA, EPL, UEFA n.k.), Wasanii wa bongo na skendo zao, namna mheshimiwa anavotumbua majipu. Ni ngumu kumkuta kijana wa miaka 18 - 35 akiongea vitu vya maana vya kujenga uchumi (binafsi, jamii na taifa) kwa muda unaozidi dakika 5 mfululizo bila kuchomeka Tusi.

Hivi interview/kazi huwa mnapataje aisee? na bomba la mafuta tumeambiwa linapita Tanzania kweli namna hii mtapata kazi kweli? au ndio watajaa wa Kenya kama kawaida?

NB: Fuatilia kwa wauza magazeti, vijana wengi hununua magazeti ya michezo, udaku n.k. na kuacha magazeti yenye fursa na habari za maana kwa mustakabali wa nchi. So Disgusting !
Legendary!
 
Mkuru umesema kweli,
Ngoja nilifuatilie Kwa ukaribu
 
Mtanzania ataongea kutokana na anaongea na nan.so ukiona mtu anaongea pumba mbele yako ujue kakuona you are in that level/class
 
Binafsi mimi ni kijana wa miaka 20+
Mtoa post umesema ukweli kabisaa
Mara nyingi huwa sina point za kuchangia na kudevelop story ya maana niwapo na vijana wenzangu kwani utakuta unakinzana na story zao hasa za kipuuzi na kipumbavu zisizo na manufaa yoyote kwa maisha yao binafsi zaidi ni habari za mademu magetoni, mpira na umbea tupu,
Bahati mbaya hata kwa watoto wa kike ni vile vile story za kipuuzi puuzi tu yaani inafikia hatua unashindwa hata kumutongoza mtoto wa kike kisa huna story azipendazo yeye dah!
In short sisi vijana hatuna muda wa kujadili yenye manufaa na maisha yetu binafsi bali tumeendekeza sana ushenzi na kukosa fact za kujadili dhidi ya nn tunapaswa kufanya kuyafanya maisha yetu yaboreke zaidi.

Bahati mbaya ukiingizia mada ihusuyo vitu vya msingi ndio utajua sasa kuwa vijana hatuna habari kabisa na mambo ya msingi
Ila ingiza mada ya uchebe, zari ze boss, shilole aaaah utajiona nawe umetoa mada ya maana mbele ya vijana na wachangiaji watakuwa wengi hatarii
Au mada ya demu kuwa ulimuingiza gheto na kumnyandua, kijiwe kitachangamka hatarii
Au jamaa alipata vijihela kidogo vya bodaboda na kujiona don kijiweni kwao na kuwanyandua mademu kisa pesa ila bahati mbaya kafulia ghafla hahahahaa, wachangiaji watakuwa kama wote eee,
Kimsingi vijana hatuna tujualo zaidi ya umbea na ujuaji tupu

Njoo mavyuoni sasa,
Huko ndiko tunakojua tunapata wataalamu wa fani mbali mbali,
Vijana hawana hili wala lile zaidi ya kutegemea slide za lecture na kutengeneza formation za test hahahaa,
Hatusomi kabisa ila tunapenda kupendeza pamba kali na njumu kaliii
Unakuta mwana chuo hajui library toka first year to last year, hajui ata e-library asome vitabu aongeze maarifa zaidi ya masomo ayasomayo 😂😂 dah
Bahati mbaya unakuta mwanafunzi mwaka wa tatu anasoma lakini hajui ata field of work za masomo yake duh! Yaan anajiendea tu ili mradi ana faulu test na UE lakn in real hajui akfanyacho baada ya kuhitimu 😂😂

Tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana lipo lakni upande mwingine sisi vijana hatuajiriki kabisaa kwa sababu tuko empty vichwani mwetu hasa kwenye professional zetu,
Tuna pata Ma GPA makubwa lakini in practice tuko empty
Hatupendi kusoma na kutumia resources za vitabu mavyuoni kujifunza zaidi
Tubadilike tuache manunguniko yasiyo na tija, tusome sana vitabu sio slide za kufaulu mitihani ijapo skatai kutosoma hayo madesa ila tusome vitabu tujue zaidi
Unakuta mtu ana soma UDSM hajawahi iingia library hadi anamaliza, so unategemea nini hapo sasa,
Usomi wa siku hizi ni ili mradi nafaulu tu mitihani ila sio kupata maarifa na kuyaweka katika vitendo.

Tunadilike vijana, tujadili mambo yenye tija na sio umbea tupu
Tuzijue nafasi zetu kwa jamii inayotunguka na kuitumikia ipasavyo.
Inakera sana kuona vijana tunakosa ueledi hata wa kuchangia mada yenye mantiki ngazi ya familia na badala yake unakuta kijana yupo upstair na siimu aina ya iphone anachangia maada za hovyo kwenye group fulan la whatsapp, shit sana dah!
Wazazi endeleeni kutufunza majumbani kwetu ili kuokoa taifa
 
Huko tuendako wenye hela watakuwa wachache sana, maana vijana wengi ni watu wa kuridhika sana,akipata laki tu anakimbilia kwenye pombe,umalaya na kubeti,hawazi tena namna ya kuiongezea wenzake hiyo laki
 
Back
Top Bottom