Maongezi vijana wa Tanzania; 96% ni pumba

and 300

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
26,325
36,121
Vijana wengi wa kitanzania (Sehemu za miji mikubwa ikiwemo Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya) 96% ya maongezi yao ni pumba tupu na vitu visivyowasadia katika kujikwamua kimaisha ikiwemo mpira wa Ulaya (FA, EPL, UEFA n.k.), Wasanii wa bongo na skendo zao, namna mheshimiwa anavotumbua majipu. Ni ngumu kumkuta kijana wa miaka 18 - 35 akiongea vitu vya maana vya kujenga uchumi (binafsi, jamii na taifa) kwa muda unaozidi dakika 5 mfululizo bila kuchomeka Tusi.

Hivi interview/kazi huwa mnapataje aisee? na bomba la mafuta tumeambiwa linapita Tanzania kweli namna hii mtapata kazi kweli? au ndio watajaa wa Kenya kama kawaida?

NB: Fuatilia kwa wauza magazeti, vijana wengi hununua magazeti ya michezo, udaku n.k. na kuacha magazeti yenye fursa na habari za maana kwa mustakabali wa nchi. So Disgusting !
 
Zamani kabla ya uhuru...kulikua na upigaji kura za kuchagua mabaraza na wabunge.
Moja ya masharti ni kuwa huwezi kupiga kura kama hukusoma na huna kazi ni mzururaji.
Tulipinga sana wakati ule..kumbe wazungu wale walikua na maana yao...ndio sawa na haya unayosema.
 
Nadhani kuna tatizo katika akili za vijana waliozaliwa miaka ya themanini kwenda juu.......

Yaani unaweza ukadhanj ni wendawazimu......kwani ukiyatazama mambo wanayojishughulisha nayo ambayo yanachukua asilimia kubwa ya maisha yao ya kila siku na ukiutazama ulimwengu unavyokwenda kasi na mabadiliko kiuchumi basi unabaki kuwaonea huruma huku wao wakikushangaa wewe na kukuona ni mjinga kuliko.....

Kitu kingine kikubwa kinachowaangamiza vijana wa sasa ni ubishi....na kutokupenda kushaurika.....

Watu wazima wazima ni watu waliowahi kuliona jua kabla yako kwa hiyo wakati wewe bado upo kwenye viungo vya uzazi vya wazazi wako wao wanaishi duniani kwa hiyo wanayafahamu mengi ya dunia.....anapokuambia kuwa jambo fulani usifanye sio zuri kwako ni kwamba limemkuta yeye mwenyewe kwani hata yeye alikuwa kijana kama wewe au la kuna mtu wake wa karibu limemkuta....kwa hiyo si vyema kupuuzia ushauri au makatazo ya watu wazima.......

Vijana wa miaka hii hawana subira hata chembe kwenye mioyo yao.......wanataka kuyafanya mambo ya miaka kumi kwa siku moja tu......wanapenda starehe na utajiri wa haraka lakini hawapendi kufanya kazi na hata wakipata kazi hawana nidhamu ya matumizi ya pesa zao.....mwisho wanakuwa vibaka tu.......

Utandawazi nao umewafanya vijana waishi maisha ya kufikirika kuliko uhalisia wenyewe......

Kwa kifupi kuna tatizo kubwa kwa vijana wetu wa sasa.....
 
Aisee umegusa "Ikulu" hawatachangia hapa kabisa.............................. Yaani ukikuta wanaongelea mpira wa Ulaya dah huwa nachoka kabisa yaani siwaelewi kiukweli yaani utasikia ooohhh kuna "Demu" japo hilo neno huwa silipendi sana kulisikia kaja kwa fulani, ooohh yule jamaa aliuwa na pesa sasa kafulia, yaani majungu full huwa nawachukia mpaka saa nyingine nawamwagia maji kwa makusudi nikipita na gari................. yaani umbea umbea tuuuu
 
Back
Top Bottom