Maongezi vijana wa Tanzania; 96% ni pumba

Aman iwe nanyi wapendwa katika bwana

Kama kichwa cha habar kinavyosomeka hapo juu


Mimi ni kijana mmoja wapo kati ya vijana ambalo ndo kundi kubwa zaid lenye watu wengi sana tanzania ulinganisha na wazee ambao ni wachache


Vijana ndo taifa la leo na ndo nguvu kaz ya taifa

Vijana wa sasa ni taifa la leo sawa lakin si nguvu kaz ya taifa tena, vijana wa sasa ni wazembe kupitiliza wasio taka kufanya kaz had kidogo ndo maana wengi wao wameolewa na mama na ndo yanayo waweka mjin, wengine sasa wamegeukia mapenz ya jinsia moja hii ni hatar sana aisee inatia huruma sana


Vijana wamekuwa watu wa kujipodoa na kupaka poda na kuvaa nguo za kubana mapaja za wadada HASA WANAUME WA DAR


maongez yao ni pumba sana aisee unatawakuta wapo kijiwen wakinywa kahawa na kashata maongez yao ni story za mademu tu na si vinginevyo, wakichoka kuongelea mademu wanamugeukia anko magu na kuanza kumlaumu kuwa kabana, wamesahau hata kipind cha kikwete maisha yao yalikuwa vile vile


hawanaga hata mda wa ibada kidogo japo mara moja kwa week


Bora hata vijana wa mikoan bado hawajakengeuka kama wa dar sizan kama kuna mwanaume wa mikoan anayepaka poda

WAZAZ NYIE NDO WA KULAUMIWA HAMJUI KULEA AISEE NYIE NDO CHA CHANZO CHA KUPOLOMOKA KWA MAADILI HASA WAZAZ WA KIKE


ni hayo tu


LONDON BABY
 
Ukiweka picha haitadhuru na wewe ukiwa mvulana wa Dar itapendeza zaidi.
tapatalk_1509729925162.jpeg
haka hapo ka picha unakokataka
 
Vijana wengi wa kitanzania (Sehemu za miji mikubwa ikiwemo Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya) 96% ya maongezi yao ni pumba tupu na vitu visivyowasadia katika kujikwamua kimaisha ikiwemo mpira wa ulaya (FA, EPL, UEFA n.k.), Wasanii wa bongo na skendo zao, namna mheshimiwa anavotumbua majipu. Ni ngumu kumkuta kijana wa miaka 18 - 35 akiongea vitu vya maana vya kujenga uchumi (binafsi, jamii na taifa) kwa muda unaozidi dakika 5 mfululizo bila kuchomeka Tusi.

Hivi interview/kazi huwa mnapataje aisee? na bomba la mafuta tumeambiwa linapita Tanzania kweli namna hii mtapata kazi kweli? au ndo watajaa wa kenya kama kawaida? (Mfano STRABAG, Nakumatt?)

NB: Fuatilia kwa wauza magazeti, vijana wengi hununua magazeti ya michezo, udaku n.k. na kuacha magazeti yenye fursa na habari za maana kwa mustakabali wa nchi. Sad!
ungekua unajua watu wana ishi vipi na hiyo mitaji,na fursa zilizo kaliwa na wachache na zinazo taka uwezo usinge kuwa una ropoka kama na wewe humo humo kwenye asilia 98.

wanasema mwenye shibe ajui mwenye njaa.

maisha ya vijana wanaoyo pitia familia zao ni zashida na mazingira maisha yetu hayana unafuu.

sehemu gani benki kikakupa pesa ukafikilia kufanya jambo la maana kama huna nyumba au gari ndio upate mkopo kuanzia biashara kubwa.
zaidi ya hapo ni pesa mtu anaye tafuta kwa jasho lake aliwezi hata kukizi maitaji yake na biashara yake.
wachache ndio watakao weza timiza ndoto zao kutokana na walipo toka maisha mazuri,watoto wa matajiri na viongozi.

hivi ni kuulize kitu uliye kwenye asilimia 98
ndo umemaliza chuo au ndo una anza kutafuta,mawazo yako kutaka kutengeneza vitanda na makabati,na vitendea kazi vyote vinataka milion 6.huna hata mia au mtaji hukizi
unazani hapo kutakuwa na ndoto hewa au malengo kuzeeka

kumbuka mawazo mazuri bila pesa ni sawa na pesa bila kuwa na mawazo
 
Back
Top Bottom