MAOMBI YA KAZI.

MAOMBI YA KAZI.

Msaga_sumu

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
341
Reaction score
367
Habari wakuu,
Utangulizi:
Awali yayote nipende toa shukrani kwa Mungu na kwa yeyote atakae wiwa na maombi yangu.
Mimi ni kijana umri miaka 24, nina degree ya accounting with information technology,graduate of 2024, naishi dar es salaam,,,.

Uzoefu:
1. Utafutaji wa masoko na kudeal na wateja: nilipomaliza chuo baada ya kukosa ada kujiendeleza na CPA nilijiunga katika harakati za mtaa na kuanza kama freelancer wa azam pesa, kwa kuzunguka kutafuta wateja na kuwaunganisha na huduma hio iliokua imeanza karibu mwaka tu,mda mwjngine tukizunguka na magari na wasanii mbalimbali katika promotion,, hii ilinifungua kiakili namna mitaa ilivo na sekta nzima ya masoko..
Kwa sasa nashukuru ni freelancer wa bet moja hapa tanzania nipo chini ya mkuu mmoja nashukuru nilimpatia humu walau hela ya chakula sikosi. Kwenye msafara wa mamba kenge pia wapo niliwahi pia fanya kazi katika store moja ya uuzaji wa majiko ya gas na mitungi, jamaa yangu yupo humu JF ntahifadhi jina kwa yote alinifanyia nashukuru maana alinijenga sana kutoka hapo nikawa kidogo hard na mtaa,ushule ukatoka.

2. Uzoefu na kazi za stationery na matumizi ya computer, uandishi wa stories, typing, kuandaa research na project na kazi nyingi kama hizo. Niliwahi fanya katika stationery ya jamaa yangu mmoja kigamboni feri ila kwa kumshikia akiwa safari huko mkoani,pia niliwahi mwandalia stories jamaa mmoja wa kenya japo alikua na kazi zilizohitaji mtaji kuandaa bila malipo hivo nikashindwa endelea fanya naye kazi ili niweze pata nafasi kufanya vitu vingine.

3.Uzoefu katikabl biashara za ufugaji na kilimo: kwa miezi kadhaa nilikua nikijihusisha na ufugaji wa kukubchotara huko kijijini pamoja na ulanguzi na uuzaji wa nafaka,, kwa kununua moja kwa moja kutoka mashambani kwa wakulima kwa bei ndogo na kusubiri pale bei itapanda ili kupata faida,kwetu kule tunaitwa chomachoma.

4. loan officer and call center agent, ukusanyaji wa madeni na utoaji wa mikopo katika online microfinance moja hapa Tanzania.

5.Uhasibu, ukaguzi na tax fields: kwa sasa nafanya kazi na kampuni moja ya ukaguzi na uandaaji wa hesabu inayoitwa PPA (premium plus Association) auditing and accounting consultant firm,,,changamoto ni upande wa malipo ni mwezi wa 5 sasa tunafanya kazi kwa kujitolea bila namshukuru boss amekua akitupa walau pesa ya chakula na nauli, ila kwa mahitaji yangu imekua ikinipa tabu sana kwani nahitaji kodi na mahitaji mengine kwan naishi mwenyewe. Nauzoefu katika kazi za uhasibu kuandaa reports, kufanya tax returns, ukaguzi wa hesabu,stock management, reconciliations, cash management na shughuli zingine za kihasibu kwa sasa tunadeal na 4 electric clients wetu hapa dar hvo nauzoefu na hesabu kampuni kubwa na ndogo.

Hitimisho: kwa mwenye connections na kazi full time au part time hata kwa mda wa ziada kwa jioni na usiku naomba,,,unisaidie nikiwa kama kijana ili kuweza kufikia malengo. Ntashukuru sana.
0768842034
richjohnmashauri1@gmail.com
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom