Maombi kwa Mbunge wangu Kigwangalla

ANDREW JOSEPH

JF-Expert Member
Jul 17, 2017
422
405
Mheshimiwa pole na majukumu yako ya kila siku ya kulitumikia taifa ila huku kwenye jimbo lako kuna mambo hayajakaa sawa.

Kata ya Ndala ndio kata kubwa kuliko kata zote kwenye jimbo lako hoja yangu nini?

Wakati nikiwa mdogo niliona mama yangu akienda bombani kuchukua maji lakini leo huwezi kuona haya nani aliihujumu mladi muhimu kama huo?

Jambo la pili ni senta yenyewe ilivyokaa kuna shilika hapa ni chanzo kikubwa cha kuigawa Ndala kihuduma hasa umeme Roman catolic wanaeneo kubwa sana kutoka chuo cha ualimu mpaka balabala ya kwenda Igunga na kinachouma zaidi hawajawahi hata kujenga kibanda cha kuku zaidi ya kuhifadhi majambazi maana limegeuka poli katikati ya senta lisilokuwa na faida yeyote kwa jamii husika.

Kama kuna malengo ya serikali kuwakabidhi Roman hilo eneo basi waambieni wanze kulifanyia kazi na kama ilishashindikana liludishwe kwa wananchi waendelee na maisha yao kama kawaida..

Hii inachosha mtu unazaliwa unakuta vichaka nawewe unazaa watoto wanakuta vichaka na ukiuliza ni eneo la watu fulani na halifanyiwi kazi yeyote. Asante
 
Back
Top Bottom