Panthera 1
Member
- Dec 30, 2014
- 50
- 9
Kwanza nikupe hongera kwa kukamilisha jukumu zito la kuirudisha ardhi ya Madira kwa wakazi wa Sing'isi,big up kwa hilo.
Yalitokea mengi wakati wa nyuma na risasi zilipigwa sana wakati watu wakililia ardhi yao ya madira.
Leo napenda kukupa ushauri wa bure nikiwa kama mmoja wananchi wa jimbo lako.
Eneo la Madira limepitiwa na mito miwili jambo ambalo ni neema na baraka kubwa kwa wakazi wa Sing'isi.
Mito hiyo ikitumika vyema inaweza kuzalisha ajira ya kudumu na kudumu kwa miaka mingi kwa vijana wa Sing'isi na watanzania kwa ujumla.
Tambua kwamba,eneo la Madira ni sehemu nzuri kwa kilimo na kwa muda mrefu watu wamekuwa wakitumia eneo hilo kwa ulimaji.
Kumbuka hata wewe umesoma kwa ajili ya kilimo.
Bila ya kilimo,ni wazi mama yako asingeweza kuzunguka na kapu la nyanya kuuza ili akosomeshe,mshukuru sana kwani juhudi yake imekufanya leo uwe mbunge.
Bila ya kilimo asingefanikiwa kukufikisha hapo ulipo.
Ni vyema eneo la madira likaendelea kutumika kama sehemu ya kilimo,kupitisha greda ni kufanya dhuluma kwa wakazi wa Arumeru,kupitisha greda ni kuashiria kwamba mwisho wa maendeleo umefika,kupitisha greda ni sawa na kuwazuia wananchi wako kula.
Kilimo ndio kila kitu,kilimo ndio nyenzo kuu ya maendeleo katika dunia ya leo.
Ukiwa kama msomi,litazame hili kwa makini sana,tazama kwa jicho la tatu utatambua kwamba bila ya kilimo kinafaida ngapi,utatambua kwamba ajira ngapi zitatengenezwa kupitia kilimo.
Ni ushauri wangu tu,ukiona unakufaa uchukue,ukiona hukufai basi uache.
Ila kumbuka,BILA YA KILIMO LEO USINGEKUWA MBUNGE.